JokaKuu,
Kuhusina na kuwepo kwa taarifa kwamba ZNZ ilitoa 11% ya mtaji wa kuanzisha BOT, sio taarifa bali hata serikali imekubali hili. In fact, kuna mgogoro wa muda mrefu tuu kati ya serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuhusiana na shares za Zanzibar BOT. Hili suala lilibbuka bungeni hivi karibuni ambapo kama sijakosea Mh. Hamad Ali Hamad (CUF) aliuliza swali la nyongeza kutaka ufafanuzi kuhusiana na asilimia 11.5 ya shares za Zanzibar BOT. Swali lake la nyongeza lilitokana na kutoridhika na majibu ya Naibu Waziri wa Fedha kwa swali la msingi lililoulizwa na Rashid Omar (CUF).
Katika swali lake la msingi Rashid Omar alisema kulikuwa na taarifa kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni shareholder wa kwanza kabisa wa BOT. Then, akataka kujua kama Zanzibar ilishawahi kufaidika na matunda ya shares zake BOT. Aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha wakati huo Pereira Ame Silima (sasa ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani) alimjibu kuwa BOT ilianzishwa na Bank of Tanzania Act 1965 kama chombo kilichokuwa chini ya Serikali ya Muungano wa Tanzania.
Ni kweli kabisa BOT ilianzishwa na Bank of Tanzania Act 1965 to take over the functions and operations of the then East African Currency Board (EACB) founded in 1919 to manage currency supply and exchange in the then British colonies of East Africa and neighbouring countries. Kuna maandishi yanasema kuwa baada ya kufa kwa EACB, pounds 950,000 as dividend of Zanzibar and 668,884 Pounds BOT capital from EACB were taken by Union Republic to establish the BOT.
Kwa mujibu wa swali la nyongeza la Hamad Ali Hamad (CUF), records zinaonyesha kuwa Zanzibar ilikuwa na asilimia 11.5 ya shares kwenye EACB. Wakati BOT inaanzishwa, shares hizo zilihamishiwa BOT. Katika swali lake, Hamad Ali Hamad (CUF), alitaka kujua zilipo hizi shares ambazo zilihamishiwa kutoka EACB kwenda BOT.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Fedha alikubali kuwa asilimia 11.5 ya shares za Zanzibar EACB zilihamishiwa BOT wakati wa kuanzishwa kwa benki hiyo. Kuhusu zilipo shares hizo, Naibu Waziri huyo alisema it is still unclear na kwamba ni moja ya controversial issues za muungano ambazo zinafanyiwa kazi kwa sasa na serikali za pande zote mbili.
Kuhusiana na kuwepo kwa People's Bank of Zanzibar ambayo ilikuwa ikifanya kazi kama "benki kuu" ya ZNZ kwa kipindi kirefu mpaka miaka ya 80 au 90, ni kweli kuna benki inaitwa the Peoples Bank of Zanzibar (
PEOPLE'S BANK OF ZANZIBAR ) ambayo ilianzishwa mwaka 1966 na serikali ya Zanzibar under Cap. 153 of the Zanzibar Companies Decree. Hii benki ilikuwa imejikita zaidi Zanzibar hadi mwaka 2011 ilipofungua tawi Dar Es Salaam na ilikuwa na mpango wa kufungua matawi Mwanza, Mtwara na Arusha.
Benki hii bado inamilikiwa na serikali ya Zanzibar kwa asilimia 100. Ni moja ya benki za zamani sana Tanzania. Ni kweli ilikuwa ina-function kama commercial bank na central bank ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hadi mwaka 2001 ambapo kazi zake ki-central bank zilihamishiwa BOT.
Whether Zanzibar imekuwa ikipata mgao kutokana na faida inayopata BOT kulingana na kiwango cha shares zake za mwaka 1966 au kutoa ruzuku wakati BOT ikipata hasara ni ngumu kujua. Lakini kwa mujibu wa majibu ya Naibu Waziri kwa wabunge hao, hisa zote za BOT zilimilikuwa na Serikali ya Muungano. Hata Bank of Tanzania Act 2006 bado inasema hivyo.
Kifungu cha 2 cha sheria hiyo ya mwaka 1965 kilisema kuwa the "Act shall extend to Zanzibar as well as to Tanganyika citation shall bind the United Republic." Section 14(1) of the 1965 Act provided that "the authorized capital of the Bank shall be twenty million shillings". Section 14 (2) provided that "the capital of the bank shall be subscribed and held only by the United Republic. Kama kweli start-up capital ya BOT i.e. twenty million shillings ilitokea Treasury ya Serikali ya Muungano na kuwa custodian wa shares za BOT alikuwa Treasury Registrar, interests and liabilities za Zanzibar to BOT as an individual zinatokea wapi tena?
Lakini kuna article moja inajaribu kuelezea kuanzishwa kwa BOT na kuhamishiwa rasilimali za Zanzibar kwa nguvu hasa zile zilizokuwa EACB kwenda BOT kinyume na makaubaliano ya Muungano ya mwaka 1964. Labda ndio maana katika majibu yake, Naibu Waziri alipoulizwa kuhusu zilipo asilimia 11.5 ya shares hizo alisema bado haieleweki na kwamba ni controversial issue ya muungano ambayo inayofanyiwa kazi na serikali za pande zote mbili. Nina hard copy ya hiyo article, nitajaribu kutafuta soft copy niiweke extract husika hapa.