Taarifa kutoka katika soko la hisa la Dar es salaam zinasema thamani ya hisa za nafasi za uongozi na uanasiasa zinazidi kuporomoka siku hadi siku tangu serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani.
Taarifa zisizo rasmi zinasema kuporomoka huku kutokana na mkakati unaoonekana kutenganisha uongozi na biashara au uongozi na ufisafi. yasemekana huko nyuma watanzania wengi waliwekeza mitaji mikubwa kutafuta nafasi za kisiasa na uongozi wa kitaifa si kwa kuwa na machungu na shida za wananchi ili wawasaidie bali ilikuwa ni biashara inayolipa kuliko biashara nyingine zozote kwa wakati huo.
mwekezaji mmoja katika nyanja hizo wakati akihojiwa alidokeza kuwa kiongozi ilifanya mtu apate biashara zenye tija, au kama hana biashara basi ilikuwa rahisi kupata kamisheni kutoka kwa wafanya biashara ilimradi tu kulinda biashara zao au kuwapatia shughuli.
kazidi kusema mwanzoni ilikuwa inakuwa ngumu maana kupita kwa wananchi ilihitaji kuwajua, kama ungejidai kusema ukweli basi hawakupi kura hivyo ilibidi kuvika biashara zako ngozi ya matatizo yao na kwenda kuwalilia kuwa unakwenda kuwasaidia. akazidi kusema kimsingi kula na vipofu ilibidi usiwaguse mikono hivyo mara kwa mara ilibidi ukumbuke kuwapelekea misaada lakini akasema kwa tija iliyokuwepo katika biashara hiyo wala hilo halikuwa tatizo.
akasema unajua kinachoisumbua nchi hii zaidi ni ujinga wa wananchi maana wao mtu anayewapa lifti kwenye magari yake, kuwapa chakula yaani vitu vya kutoa mfukoni ukiwa mkarimu wao wanaona wewe ndiye kiongozi bora.
akasema sasa upepo umebadirika, akasema sio kwamba wananchi ujinga umeisha bali usinajua katika kucheza bahati nasibu kuna siku unabahatisha unakula? akasema wananchi sasa wamebahatisha jamaa yaani alivyokuja uongo sasa kwenye majukwaa haufanyi kazi! mianya ya biashara kwenye siasa na uongozi anaziba. akasema sijui kwetu sisi ambao hatuna shughuli nyingine ya kufanya tutaishije?
akasema kwa sasa sote kuanzia tuliokuwa na majina makubwa kwenye siasa mpaka wenye vipaji waliokuwa wanaibuka kila siku tumetulia tuli maana siasa zimebadilika kabisa.
akasema mimi nikiangalia madesa yangu ya siasa yote hayafanyi kazi mpaka najiuliza nitaanzia wapi? akasema siasa hii inakoelekea wala haina maana ni bora kuiacha lakini akasema atafanya nini zaidi ya siasa.
akasema hakuna ilikuwa na faida kubwa kama siasa lakini najiuliza sijui nianzie wapi sijui kukusanya mahindi vijini na kuuza kazi zenyewe usumbufu mwingi lakini faida kidogo.
mwisho akasema lakini wananchi wakidanganyika na sisi tulikuwa tunakula jasho zao na wale tuliokuwa tunawapelekea kwa makelele tunayopiga kuwa hali mbaya mara uchumi unarudi nyuma bila kutafakari watajijua. akasema mimi nayasema haya kwa kuwa nimekwisha ona kuwa hata siasa zikibadilika huko mbele mimi siwezi kurudi sasa nikatafakari tulikuwa tunatumia ujanja tunarithishana nafasi hizo, sasa mimi sipo watoto wangu na wajukuu si ndio nao watakaa pembeni na maana mimi sipo tena kuwaingiza!
ni bora mifumo hiyo ife kabisa sasa watoto wetu na wajukuu wetu tuwarithishe kutafuta kwa kutumia jasho lao.
akasema na hili huyu jamaa kama alivyotengeneza mazingira siasa zikaacha kulipa inabidi atengeneze mazingira watu wavune kwa jasho lao.
lakini akasema kwa sasa si utani siasa na uongozi vitu ambavyo vilikuwa njia za panya kuelekea kwenye kula jasho la watanzania kwa sasa zinageuka kuwa nafasi za kusema ukweli na kufanya kazi. wengi tuliokuwa huku haya haya hatukuyazoea maana wanasema hayana tija kwa kizungu wanasema efficincy.