Hisa za Mwanza Community Bank PLC: Speculators Mnasemaje??

Kivumah

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
2,428
1,050
Nimesikia matangazo ununuzi wa hisa za Mwanza Community Bank PLC umeongezwa muda, Biashara hii ya Hisa kwangu mimi imekaa ki-speculation zaidi kwa maana unawekeza/unatupa pesa zako huko lakini tegemea kupata au kukosa(Rejea hisa za TOL, Precision Air n.k).

Niliwahi kununua Hisa za NMB walipokuwa wanauza hisa zao lakini baadae nilivoona hazifanyi vizuri sokoni nikaziuza, Leo hii najutia uamuzi ule niliufanya haraka sana kwasababu NMB wanafanya vizuri sana sokoni sasa hivi, na kama ningeamua kusubiri hadi sasa ningekula bingo nzuri sana.

Sasa swali langu kwa Mabingwa wa Speculation(Speculators) hizi hisa za Mwanza Community Bank PLC mnadhani zitakuja fanya vizuri sokoni?, na Je kwa vigezo vipi mnavoviona?

Poster-A2.jpg

Cc: DseTanzania Pasco SanctusMtsimbe

Last edited by a moderator:
Zitafanya vizuri tena saana.......kumbuka hii ni bank ya kanda (Japo niu mwanza), ila itategemea na uongozi wake utakuwaje.......hii bank wanaanza kama Dar es Salaam Community Bank PLC walivyoanza japo kimfumo kuna kautofauti kidogo....Hisa za DCB zinafanya vizuri,,,,,kama unataka kuwekeza ni vema ukazinunua ila ukumbuke hii bank ndo inaanza kwa hiyo itachukua muda kidogo kupata faida,,,,kama unataka faida ya muda mrefu .....you can go for it ila kama ni faida ya muda mfupi......sikushauri
 
nio maaana mimi nikaacha baada ya kuona kuna matatizo ya hapa na pale poa tuwaache kwanza wanunue ili tuone kwanza
 
Zitafanya vizuri tena saana.......kumbuka hii ni bank ya kanda (Japo niu mwanza), ila itategemea na uongozi wake utakuwaje.......hii bank wanaanza kama Dar es Salaam Community Bank PLC walivyoanza japo kimfumo kuna kautofauti kidogo....Hisa za DCB zinafanya vizuri,,,,,kama unataka kuwekeza ni vema ukazinunua ila ukumbuke hii bank ndo inaanza kwa hiyo itachukua muda kidogo kupata faida,,,,kama unataka faida ya muda mrefu .....you can go for it ila kama ni faida ya muda mfupi......sikushauri
Asante nimekusoma kiongozi, umezungumzia kuhusu uongozi,hilo ni la muhimu kiukweli. hata precision air na Nicol kilichoziangusha ni management
 
Isije ikawa yale yale ya NICOL! Watu wanasikilizia maumivu mpaka kesho!
Nicol watu walizichangamkia kwa kuwa waanzilishi walikuwa wazawa wenzetu waliofanikiwa kibiashara watu wakajenga imani nao, lkn kilichotokea kilikatisha tamaa kiukweli
 
Kisingizio et manangement ilikuwa mbovu! Kila kitu kinawezekana TZ!
 
Nimesikia matangazo ununuzi wa hisa za Mwanza Community Bank PLC umeongezwa muda, Biashara hii ya Hisa kwangu mimi imekaa ki-speculation zaidi kwa maana unawekeza/unatupa pesa zako huko lakini tegemea kupata au kukosa(Rejea hisa za TOL, Precision Air n.k).

Niliwahi kununua Hisa za NMB walipokuwa wanauza hisa zao lakini baadae nilivoona hazifanyi vizuri sokoni nikaziuza, Leo hii najutia uamuzi ule niliufanya haraka sana kwasababu NMB wanafanya vizuri sana sokoni sasa hivi, na kama ningeamua kusubiri hadi sasa ningekula bingo nzuri sana.

Sasa swali langu kwa Mabingwa wa Speculation(Speculators) hizi hisa za Mwanza Community Bank PLC mnadhani zitakuja fanya vizuri sokoni?, na Je kwa vigezo vipi mnavoviona?

Poster-A2.jpg

Cc: DseTanzania Pasco SanctusMtsimbe

Mimi nakushauri nunua hizo Hisa hiyo bank itafanya vizuri nakuhakishia na ni bora ununue sasa hivi kwenye IPO - primary market zikishakwenda kwenye secondary market una cash in kwakuziuza kunauwezekano zikapanda kwa asilimia 15 mpaka 20 kipindi tu watakapo kuwa wameziweka kwenye secondary market kwahiyo unauza hapo hapo zikapanda usisubiri dividend kwa sababu kampuni bado ni ndogo unachukua muda kwa management kuanza kutoa dividend na kumbuka kuwa ordinary shares hazina obligation ya kulipwa dividend ni preference shares ndio zina right ya dividend. Na makampuni mengi madogo ni mazuri kwa capital growth na sio income ambayo ni mengi makampuni makubwa na ambayo tayari yako stable kwenye market.
Pesayako - Money Speculator
 
Last edited by a moderator:
Kwa kuongezea angali jinsi Maendeleo Bank baada ya kuwa listed kwenye secondary market shares value zake zimeongezeka kwa asilimia 20 yaani market value. Changamkieni fursa msingoje kesho maana opportunity come once. We call it arbitrage opportunity in finance. If you leave it someone will take it. Changamkia fursa
 
Mimi nakushauri nunua hizo Hisa hiyo bank itafanya vizuri nakuhakishia na ni bora ununue sasa hivi kwenye IPO - primary market zikishakwenda kwenye secondary market una cash in kwakuziuza kunauwezekano zikapanda kwa asilimia 15 mpaka 20 kipindi tu watakapo kuwa wameziweka kwenye secondary market kwahiyo unauza hapo hapo zikapanda usisubiri dividend kwa sababu kampuni bado ni ndogo unachukua muda kwa management kuanza kutoa dividend na kumbuka kuwa ordinary shares hazina obligation ya kulipwa dividend ni preference shares ndio zina right ya dividend. Na makampuni mengi madogo ni mazuri kwa capital growth na sio income ambayo ni mengi makampuni makubwa na ambayo tayari yako stable kwenye market.
Pesayako - Money Speculator

Mkuu Tambua hii bank haijaanza........kwa kuhisi tu inaweza fanya vizuri.........hapo hatuna uhakika hata kidogo......Ili kampuni ifanye vizuri......yapo mambo mengi saana.....mfano mazingira inayofanyia biashara.......UONGOZI....mfumo utakatumika........bila kusahau connection na wafanyabiashara wakubwa.......makampuni nk........hivi vyote bado HATUJAVIONA so kwa wataalamu wanakuambia.......kwamuda mrefu itafanya vizuri..ila kwa muda mfupi hapo ningumu saana kuhisi

Swala la Maendeleo Bank ni vigumu saana kuanza kulizungumzia hapa kwani bank hina hata miezi tangu ianze kufanya biashara.........haya mambo hayatabiriki ndugu yangu....kumbuka FACEBOOK ilikuwaje...na kikubwa bado kwa TZ hii kitu bado ni kinaugeni fulani hivi

Mie nashauri kama mtu anazitaka hizi HISA asitegeme faida ya MUDA MFUPI.......faida itaanza patikana bada ya muda mrefu kidogo............miaka 2 au mitatu hivi......Jaribu fuatilia DCB walivyoanza ndo utaelewa vizuri
 
Mkuu wewe haujaelewa suala ni jinsi ambavyo strategy zako ni muda mrefu kwa ajili ya income au wewe ni pure speculator huko kwa ajili ya gain ya muda mfupi. Naona mkuu umeandika mambo mengi ambayo yanadharia tupu ya darasani . Mimi ninawapa vitu ambavyo ni practical sio mambo ya theory hapa.
Mkuu mimi naudhoefu na hivi vitu siongei theory za darasani jaribu kuelewa tofauti ya primary market na secondary market ndio utaweza kuelewa namaamisha nini . Kuhusu Facebook maspeculator tulisha iona iko over price kabla hajaenda kwenye secondary market.
Watanzania mnatabia ya kukatishana tamaa mko negative sana msipobadili mind set zenu mtaendelea kuwa maskini. Tofauti Kati ya maskini na Tajiri iko kwenye mind set na Wala sio kitu kingine.
Na wasomi wengi wako pia very risk averse sio na risk taker ndio maana wanaishia kuajiliwa na kuwa maskini.
 
Nicol watu walizichangamkia kwa kuwa waanzilishi walikuwa wazawa wenzetu waliofanikiwa kibiashara watu wakajenga imani nao, lkn kilichotokea kilikatisha tamaa kiukweli

Hivi hatma ya hii kitu ikoje wakuu?
 
nnahitaji elimu kuhusu mambo ya hisa, ntapata wap hii elimu?
Kuna thread humu zinatoa hio Elimu, unaweza zitafuta. Au kwa kifupi sana soma hapo Chini:
FAHAMU HISA NI NINI
HISA NI NINI? Hisa ni mgao (share) ya umiliki wa kampuni au biashara yoyote kubwa. Unaponunua hisa maana yake umetoa fedha kwa ajili ya uendeshaji wa kampuni au biashara husika kwa hiyo na wewe ni miongoni mwa wamiliki na nguvu au umuhimu wako unatokana na mgao ulionao. Kama kampuni ina mtaji wa shilingi laki moja na wewe umenunua hisa za shilingi elfu hamsini, maana yake utakuwa na nguvu ya kushiriki hata kwenye maamuzi nyeti yahusuyo kampuni au biashara husika, tofauti na mtu mwenye hisa za kwa mfano shilini elfu kumi. Soko la hisa (stock exchange) ni mfumo wa kibiashara ambapo wajasiriamali na wafanyabiashara, hununua vipande (stock) za kampuni au biashara na kuwekeza fedha zao kwenye mtaji kwa lengo la kuisaidia biashara husika kuendelea kukua. Soko kubwa zaidi duniani lipo jijini New York, Marekani likiwa na jina la New York Stock Exchange (NYSE). Kwa mujibu wa shirika la fedha duniani, soko la hisa ndiyo linaloongoza kwa kuingiza fedha nyingi kwenye mzunguko kuliko biashara nyingine zozote, takwimu zinaonesha kuwa mwaka 2008, mtaji katika soko la hisa dunia nzima ulikuwa ni dola za Kimarekani, trilioni 36.6 na mpaka mwezi Juni mwaka huu, mtaji ulikuwa umepaa na kufikia dola za Kimarekani trilioni 791, ikiwa ni mara kumi na moja zaidi ya uchumi wa dunia. Huu ni uthibitisho kuwa soko la hisa linakua kwa kasi kubwa na ndiyo lililoushikilia uchumi wa dunia. Kwa msingi huo, ni lazima kila mjasiriamali ajifunze juu ya soko la hisa ili kuyafikia mafanikio ya kweli.
 
Mkuu wewe haujaelewa suala ni jinsi ambavyo strategy zako ni muda mrefu kwa ajili ya income au wewe ni pure speculator huko kwa ajili ya gain ya muda mfupi. Naona mkuu umeandika mambo mengi ambayo yanadharia tupu ya darasani . Mimi ninawapa vitu ambavyo ni practical sio mambo ya theory hapa.
Mkuu mimi naudhoefu na hivi vitu siongei theory za darasani jaribu kuelewa tofauti ya primary market na secondary market ndio utaweza kuelewa namaamisha nini . Kuhusu Facebook maspeculator tulisha iona iko over price kabla hajaenda kwenye secondary market.
Watanzania mnatabia ya kukatishana tamaa mko negative sana msipobadili mind set zenu mtaendelea kuwa maskini. Tofauti Kati ya maskini na Tajiri iko kwenye mind set na Wala sio kitu kingine.
Na wasomi wengi wako pia very risk averse sio na risk taker ndio maana wanaishia kuajiliwa na kuwa maskini.

Mkuu

Kumbuka hii ni TZ...... Usifikiri nakurupuka....nakijua nachokiandika......najua nachokiandika.....najua vema siasa za soko la hisa la DSM......tangu TCC, TBL, TOL waanze kuuza hisa zao

Kwa hiki Kibank ambacho hakijaanza kufanya BIASHARA.....hatujui itakuwa na uongozi gani? inaungwa vipi mkono na Serekali.........Makampuni watakaofanya nao biashara.......board yake itaundwa na wakina nani....na wana influence gani.....kibongo bongo HUWEZI KUTUSHAWISHI HISA/BANK ITAFANYA VIZURI.....Pia unatakiwa utambue.....watu bado wanamachungu ya NICOL,TOL...tambua uelewa wa hisa kwa watanzania ni mdogo saana........nachelea kukuambia atakaye nunua hisa asitegemee faida ya muda mfupi....faida ni baada ya miaka si chini ya miwili na hata mitatu....refer back to DCB.....na kama wewe ni mbunifu waulize watu walionunua hisa za MKOMBOZI japo bado haijasajiliwa.

NAHESHIMU UZOEFU WAKO LAKINI KWA TANZANIA UNAWEZA USIWE Applicable
 
Mkuu usinichukulie vibaya . Mimi nilichosema wewe bado ujanielewa suala ni kuuza mapema zikishakwenda kwenye secondary market siyo kusubiri dividend atakayetaka kusubiri ni uhamuzi wake . Kununua ni wakati ziko kwenye primary market baada ya hapo unauza mapema zikipanda tu pindi zinapokuwa kwenye secondary market. Na huu ni ushauri wa bure simlazimishi mtu ahamini ni uamuzi wake mwenyewe kama unavyo jua biashara ya Hisa unaweza kupata zaidi au kupoteza hata kile ulichowekeza hilo kila mwanahisa uelezwa pindi unapo nunua kinachotakiwa ni wewe mwenyewe kuelewa risk iliyopo.
Ambacho sikipendi mimi ni mtu kuwakatisha tamaa Watanzania wasichangamkie fursa kwa kuzungumza kama mwakilishi wao. Biashara yoyote ina risk zake hakuna ambayo ni risk free. Na ikishakuwa risk free ni kwamba haina deal.
Naendelea kuwahimiza Watanzania wenzangu changamkieni hii nafasi kikubwa mjaribu kuweka mayai yenu kwenye vikapu tofauti. Maana yake kama unahela unataka nunua Hisa jaribu kuzigawanya labda tuseme una million mmoja. Nunua Hisa za Maendeleo bank za 300000 , mwanza community bank za 250000, KCB za 250000 na TBL za 200000. Baada ya hapo utakuwa umepunguza uwezekano wa kupoteza hela yako yote yaani 1000000(million mmoja). Kama una wasiwasi jaribu kupata ushauri kutoka kwa broker ambaye utakwenda nunua Hisa.
Hapa hatuko kukatishana tamaa tupo kwa ajili ya kusaidiana kwenda mbele siyo kulalamika tu bila kuangalia tatizo ni nini na jinsi ya kutatua tatizo na siyo kukimbia matatizo na hiyo hatakuwa ni suluhisho.
Kwenye matatizo kuna fursa na hii ndio maana yapo hili kuweza kutatuliwa na watu kupata hizo fursa.
Nawatakia Watanzania wenzangu uwezekaji mzuri wa kwenye soko la mitaji . Ni fursa nzuri na pesa yako itakuwa. Mwenye swali aniulize nitamsaidia sikimbii matatizo kwani ni fursa. Mnakaribishwa ni mimi pesa yako- Money speculator
 
Walifanya vizuri sana kwenye Victoria Saccos, uongozi una credibility. Yes, kuna tofauti kubwa ya kuendesha Saccos na bank lakini bank iko more regulated than Saccos. So huu ni uongozi ulijaribiwa na kufuzu. Kuhusu opportunities za growth kwa banks particularly regional banks, ni kubwa. Hawa jamaa wanaanza na customer base kubwa. My advice, buy the shares. NB: just like any business follow your instincts ie risk appetite.
 
Mkuu usinichukulie vibaya . Mimi nilichosema wewe bado ujanielewa suala ni kuuza mapema zikishakwenda kwenye secondary market siyo kusubiri dividend atakayetaka kusubiri ni uhamuzi wake . Kununua ni wakati ziko kwenye primary market baada ya hapo unauza mapema zikipanda tu pindi zinapokuwa kwenye secondary market. Na huu ni ushauri wa bure simlazimishi mtu ahamini ni uamuzi wake mwenyewe kama unavyo jua biashara ya Hisa unaweza kupata zaidi au kupoteza hata kile ulichowekeza hilo kila mwanahisa uelezwa pindi unapo nunua kinachotakiwa ni wewe mwenyewe kuelewa risk iliyopo.
Ambacho sikipendi mimi ni mtu kuwakatisha tamaa Watanzania wasichangamkie fursa kwa kuzungumza kama mwakilishi wao. Biashara yoyote ina risk zake hakuna ambayo ni risk free. Na ikishakuwa risk free ni kwamba haina deal.
Naendelea kuwahimiza Watanzania wenzangu changamkieni hii nafasi kikubwa mjaribu kuweka mayai yenu kwenye vikapu tofauti. Maana yake kama unahela unataka nunua Hisa jaribu kuzigawanya labda tuseme una million mmoja.
Nunua Hisa za Maendeleo bank za 300000 , mwanza community bank za 250000, KCB za 250000 na TBL za 200000. Baada ya hapo utakuwa umepunguza uwezekano wa kupoteza hela yako yote yaani 1000000(million mmoja). Kama una wasiwasi jaribu kupata ushauri kutoka kwa broker ambaye utakwenda nunua Hisa.
Hapa hatuko kukatishana tamaa tupo kwa ajili ya kusaidiana kwenda mbele siyo kulalamika tu bila kuangalia tatizo ni nini na jinsi ya kutatua tatizo na siyo kukimbia matatizo na hiyo hatakuwa ni suluhisho.
Kwenye matatizo kuna fursa na hii ndio maana yapo hili kuweza kutatuliwa na watu kupata hizo fursa.
Nawatakia Watanzania wenzangu uwezekaji mzuri wa kwenye soko la mitaji . Ni fursa nzuri na pesa yako itakuwa. Mwenye swali aniulize nitamsaidia sikimbii matatizo kwani ni fursa. Mnakaribishwa ni mimi pesa yako- Money speculator

Mkuu Sidhani kama kuna mtu namkatisha tamaa hapa
najaribu kuwa mkweli.........na kuzungumzia hali halisi..........sijasema watu msinunua hisa za Mwanza community au Maendeleo commercial bank...naomba unielewe........tambua mbinu zinazotumiwa na hizi bank hazijawahi tumiwa na bank yoyote hapa Tanzania......wakati wanafanya hivyo kuna mambo amabayo yalitutia hofu na refer kwa NICOL na TOL.............haya kwanini yasitufanye watu waogope???????? kumbuka hakuna mwekezaji anayeweka bila kutegemea faida....Ungejaribu ku adress concern zangu ningekuelewa.....
 
Mie naomba kuuliza hisa zinauzwa shillingi ngapi kwa hisa moja?? Na utalatibu ukoje kwa wale tulio nje ya nchi??
 
Back
Top Bottom