Hirizi ya simba

adden

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
7,033
15,616
Mabibi na mabwana natanguliza salam,Kwa wale waliofunga swaumu makbul walio wagonjwa Mungu awajazie afya tele.

Leo naomba tupeane habari kuhusu hirizi ya simba, hili jambo toka nikiwa mdogo hadi sasa huwa nasikia kuhusu hii hirizi ya simba ni kwamba simba akikaribia kufa huwa kuna kitu kama hirizi anakitema ambacho binadamu akikichukua na kukitumia kitu ambacho humfanya aogopwe na kila mtu hadi wanyama.

Kuna namna na njia ya kuitumia kuna wengine nasikia humeza jambo ambalo mwisho siku we kufa itakuwa shida unaweza kufa na kufufuka hata mara 60 hadi kuna maswala ufanyiwe ndo unakufa kimojaa!Mimi ndo hayo machache nayajua nasikia pia mahakamani zinafikiwagwa hapo ndio mana kama una kesi unabaki kutetemeka tu!

Mwenye ujuzi zaidi atuelimishe na jinsi ya kuipata hirizi kirahisi
 
kwahiyo wewe unataka uwe nayo?. mtoto unataka balaa, hebu endelea na utafiti wako ukifanikiwa utupe mrejesho,
 
Back
Top Bottom