Dj Kool Herc
Ambaye ni mmoja kati ya waasisi wa Hip Hop anasema “sehemu nilipoanza kupiga muziki ilikuwa ni 1520 Sedgwick Avenue, katika recreation room, chumba kilichokuwepo katika jengo lilipokuwa pango langu, watu walikuja kucheza muziki kutoka maeneo jirani”
Krs One
Anasema “.mwaka 1973, nilikuwa Bronx, katika hii sehemu iliyoitwa 1520 sedgwick Ave, hii ndiyo sehemu ambayo hip hop ilipozaliwa. Mtu anayeitwa Cool Dj Herc alikuwa akifanya maenesho..”
Tarehe ya kuzaliwa
August 11, 1973, ndiyo tarehe ambayo hip hop ilizaliwa kwa mujibu wa Cindy Campbell ambaye ni dada yake na Dj Kool Herc. Onesho la kwanza la hip hop lilifanyika siku hiyo. Onesho hilo liliandaliwa na Dj Kool Herc kwa lengo la kuchangisha pesa ili dada yake (Cindy Campbell) aweze kurudi shule (back to school party). Herc alikodisha recreation room kwa dola ishirini na tano za kimarekani na kiingilio ilikuwa ni thumni (cent) 25 kwa wanawake na thumni 50 kwa wanaume. Herc alikuwa kwenye mashine na msema chochote (mc) wa siku hiyo alikuwa ni dada yake (cindy), tukio hili ndilo linalomfanya cindy Campbell kuwa mwanamke wa kwanza katika hip hop (first lady of hip hop).