Itzmusacmb
JF-Expert Member
- Jun 22, 2016
- 1,531
- 1,133
Wakuu
Nazani nilipaswa kuweka huu uzi kwenye Jami tech ila hata hapa nmeona panafaa
Okay Tuendelee....
Huwa najiuliza sana hili swali kwamba "Tunajua kwamba gari anayotumia Raisi wetu kutembelea ni Toyota Land Cruiser ambayo ina injini ya V8 na wote tunajua Umahili wa Injini ya V8 hasa kwa magari madogo ,mojawapo ya umahili wake ni Speed!!
Lakini kwenye msafara wa Rais huwa kunakuwa na msururu wa gari si chinj ya 6 na miongoni mwao ni gari ya Kikosi cha Kutuliza ghasia (FFU) na tangu mm "Nipate akili" hawa askari nawaona kwenye gari za Land Rover Defender (Siyo V8) na miaka ya karibuni wanatumia Toyota Land Cruiser (siyo V8)
Sasa hapa inakuwaje walinzi watumie magari ambayo siyo V8 na raisi atumia ambalo ni V8 ?
Je, kwenye safari haya magari hayawezi kuachwa? Pamoja na hilo kiutendaji zipo tofauti sana na wote tunalijua sasa hii imekaaje!?
Au zile za polisi ni v8 ?( kwamaana ni special vehicles)
Nawasilisha