Hili Pengo la Walimu tutalizibaje????

Hili Pengo la Walimu tutalizibaje????

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
61,208
Reaction score
99,957
Miezi michache Mwigulu Nchemba alijitokeza hapa jukwaani kueleze kile alichokiita ukweli wa jina lake, hongera zake maana inataka ujasiri, katika mjadala ule aliulizwa swali juu ya maoni/mtazamo wake kuhusu zoezi la ukaguzi na yeye alikiri kuwa kwa kweli maadamu watu walisoma na wengine wameshafanya kazi kwa muda mrefu sasa, ni heri ikatafutwa namna ya kuwaacha tu, nakumbuka vyema hili maana nilim-quote kumpogeza na kumchokoza kuwa anatofautiana na Boss wake.

Sasa kwa taarifa za awali nilizonazo ni kwamba kuna Mkoa mmoja ambao uhakiki wa vyeti feki umeshakamata Walimu takribani mia tano na hamsini (550) kwenye Wilaya mbili tu, nikashtuka sana, na kwamba watu hao wako makazini wengine kwa zaidi ya miaka ishirini, sio kwamba hawajaenda vyuo, Lah, wameenda vyuoni wakafundishwa, wakafaulu, wakaja wakafundisha, Wakaguzi Wa Elimu kila mwaka wanakagua maandalio ya na scheme of work na wanafaulisha. Leo hii kuja kuwaondoa hawa wote ni nani ataziba pengo lao?

Kumbuka kila siku kuna Walimu wanaokufa kwa ajali na magonjwa mbali mbali zikiwemo shida lakini pia kuna kundi kubwa tu la walimu wanaostaafu kila uchao sasa hao wote bado haitoshi kuna hili kundo ambalo linaondoshwa kazini, Watoto wetu nani atawafundisha??? Kumbe hili ongezeko la UFAULU wa Wanafuzi limechangiwa na kufundishwa na Walimu wenye vyeti feki??

Ushauri, wakati tunang'oa magugu tuwe tumeandaa mbegu za kupanda!! Vinginevyo tutakua na shamba safi lisilo na magugu wala Mbegu!!! Majanga
 
Litazibika tuu kwa sirikali hii ya mwendokasi isiyoangalia ubora bali makaratasi na utendaji kazi uliotukuka.
 
Acha tu wawapunguze hii itakua ni faida kwa walimu, kuwafanya wawe watu wenye msimamo baada ya miaka kadhaa hatutaki walimu wenye tabia za kimbwa mbwa kama polisi wao wakiambiwa shika wanashika bila kujali watashika nn nani na kwa namna gani, tunataka walimu wasomi ambao wanajitambua na kutambua haki zao, kwa kuwaondoa hao walimu waoga watakwisha ukisikia mgomo utakua ni mgomo wa walimu wasomi wenye vyeti vyao ambao hawatotikiswa na woga
 
hali za binadamu wanameno kias gan na wanasaut gan ktk mambo haya
 
Mkuu kama taarifa uko ni kweli weka bayana unachotuaminisha kwa kutaja wilaya na mkoa
 
Acha tu wawapunguze hii itakua ni faida kwa walimu, kuwafanya wawe watu wenye msimamo baada ya miaka kadhaa hatutaki walimu wenye tabia za kimbwa mbwa kama polisi wao wakiambiwa shika wanashika bila kujali watashika nn nani na kwa namna gani, tunataka walimu wasomi ambao wanajitambua na kutambua haki zao, kwa kuwaondoa hao walimu waoga watakwisha ukisikia mgomo utakua ni mgomo wa walimu wasomi wenye vyeti vyao ambao hawatotikiswa na woga
Dada leo umenena ukweli.
 
Hafukuzwi kazi MTU, hii ni janja-janja tu ya hapa na pale siku ziende.
 
Mkuu kama taarifa uko ni kweli weka bayana unachotuaminisha kwa kutaja wilaya na mkoa
Hahahahahahahaaaaa bahati mbaya Mpwa huwa siandiki ili kuwaaminisha watu Bali kushea information na pengine kusaidiana kutatua tatizo. Sina uwezo wa kuwaaminisha watu
 
Back
Top Bottom