Hili ni tusi kwangu, 'watu weusi hamuwajali na kuwathamini wazee'

Mgodo visa

JF-Expert Member
Nov 1, 2016
3,590
3,626
Ni baada ya masiku mengi kupita...nikiwa na shauku kubwa ya kumtembelea RAFIKI yangu ambaye ana Asili ya Asia kwa jina SHAFIQ...

Ilikuwa ni baada ya yeye kufanya juhudi.. kupitia watu walio nifahamu hivyo kufanikiwa kupata namba yangu ya Simu..

Baada ya mawasiliano na kuweza kuelekezana namna ya mmoja, ni vipi akutane na mwenzake...nilifanikiwa kumpa ramani ya nivipi anifikie na kuja eneo ilipo kuwa ofisi yangu...

Ni kweli baada ya mawasiliano (akiwa njiani) aliweza kujikuta akiwa LANGONI katika eneo langu la kazi....

Tulipeana Mikono kwa furaha na kukumbatiana kwa bashasha tele...huku kila mmoja akionesha upendo na kutaka kujua ni vipi...wapi...kilicho kupoteza na kadha wa kadha....

Alikaribia ofisini na tulipiga story...maongezi ya muda wa zaidi ya saa moja....

Nilimueleza ni wapi nilikwenda (baada ya kupoteana tukiwa SHULE) wapi nashi sasa na familia yangu...huku nae akanieleza alipo kwa sasa pamoja na wazazi na familia yake kwa ujumla..

Hiki kinacho fuata hapa ndio sababu ya mimi kuandika UZI huu....

Baada ya siku kupita Rafiki yangu huyu aliamua kunitembelea nyumbani...
Alishangaa sana kunikuta tayari nina mke na familia kubwa ya watoto....

Tulifurahi kwa kula na kunywa kadiri ya jinsi tulivyo kuwa tume muandalia mgeni wangu... huku tukikumbushana na kucheka kwa yale mambo tuliyo kutana nayo tukiwa shuleni....

Hatimaye ilifika siku ya mimi.... nikiwa na familia yangu (kama alivyo omba) kwenda nasi kumtembelea....

Tulifika kwake na tulipokelewa kwa furaha tele.....akinitambulisha kwa wazazi wake (baba na mama) akamuita mkewe na familia ya watoto wawili...CHA AJABU ALINIPELEKA PIA KATIKA CHUMBA BIBI YAKE (mzaa Baba) kweli nilishangaa kidogo...!!

Nilimuuliza ni vipi BIBI yake aliweza kusogeza umri wake na wakati ni miaka 25 (ishirini na tano) imepita BIBI huyu alikuwa anasumbuliwa na magonjwa ya KANSA....ugonjwa wa MOYO pamoja na KISUKARI.....!!? nakumbuka pia alikuwa na ugonjwa wa KUSAHAU...!!

SHAFIQI alicheka kidogo na kuniambia..."TATIZO LENU WATU WEUSI HAMUAJALI NA KUWATHAMINI WAZEE"

Hili ndilo tusi lenyewe la mwaka..!!

Aliniambia Ndugu na jamaa zake bado wanaendelea kumpigania BIBI yake katika tiba aweze kuongeza tena japo miaka mingine kumi(10) na wakati sasa ana umri wa miaka 94 (tisini na nne)...

Aliniponda akasema ni kwa nini (sisi ngozi nyeusi) TUNAWATELEKEZA BIBI ZETU VIJIJINI wakiwa wanataabika kwa MAGONJWA na NJAA wakati sisi tukifurahia MAISHA MIJINI....!!?

Aliniambia anashangaa kuona Bibi zetu wakigeuka OMBAOMBA kana kwamba WAZEE hao hawana watoto wa kuwawezesha kupata mahitaji yao...!!

Alinieleza mambo mengi....Ni kwa nini wao huwatunza na kuwaenzi MAAJUZA (Bibi zao)...
Cha kale ni dhahabu...!!

Sisi (WABONGO) atujali wazee wetu..sana sana tunapambana kuwaua..kwa kisingizio cha eti ni WACHAWI....!!

Tizama idadi ya Vikongwe idadi waliyoko Mjini na Wale waliyo baki VIJIJINI wakitaabika na shida ya Kuni na Maji...

Watanzania tubadirike....
Tuwajali...tuwathamini na kuwaenzi MAAJUZA (VIKONGWE)...

Nunua Mchele ama Mkate..
Nunua Sabuni ama Sukari...
Nunua dawa ya Mswaki ama Mafuta ya kupaka...
Serikali pelekeni dawa vijijini...

Mkumbuke BIBI jirani yako ama yule wa MTAA wa pili...au yule uliye msahau kwa Muda mrefu na unahisi anahitaji.....

Kwa pamoja tuamke na kuziunganisha nguvu zetu kwa pamoja na tuseme hi ni kwa ajili ya BIBI wa Tanzania.....

[HASHTAG]#Happy[/HASHTAG] "GRANDMA" DAY....
 
Attachments

  • 1483620660192.jpg
    1483620660192.jpg
    96.7 KB · Views: 27

ndugu jiamini usiwe mwoga kila ukiona ngozi nyeupe.siyo kila mzungu ni mwekezaji.sijaona cha hasa kumsifia kifo kipo hata kama una pesa kiasi gani.yaani wahindi watu wa hovyo
bora angekuwa mwingine
 
Generalization hiyo
wazee wengi wa vijijini ukiwaleta mjini ndo wanakufa haraka
sababu wanakuwa hawako active tena....kilimo ni afya na mazoezi ya mwili
 
alisahau kukwambia kuwa baadhi yetu tukiambiwa ukweli tunalalamika....kosa lake ni kusema watu weusi alitakiwa tu kusema "baadhi ya" ,acha kulalamika ukipewa ukwel!
 
download.jpg
images (3).jpg
images.jpg

Usitumie hawa waasia wa huku Bongo kama reference, fanya uchunguzi zaidi. Internet ipo watu wameandika machapisho mengi sana kuhusu mambo mbali mbali.
 
Generalization hiyo
wazee wengi wa vijijini ukiwaleta mjini ndo wanakufa haraka
sababu wanakuwa hawako active tena....kilimo ni afya na mazoezi ya mwili
Siyo kulima ni afya kwa vizee bw.
Sema wakiletwa mjini "wanavuta" mapema kwa sababu ya upweke na kuwabadilishia mazingira.
Wengine hupenda fahari ya shamba kuangalia nyani ngabhu wakicheza milimani, kufukuza kwale mashambani nk.
Ss leo umlete mjini kwenye makelele ya magari, pia kumtenganisha na mabest wake wa kuazimana ugoro, unategemea nini? Wallah, utakuwa unamchimbia kaburi.
Kama mleta mada alivyoshauri, pata sukari,pata mafuta, pata sabuni, pata makoti na mablanketi ya baridi na chochote utachoona kinafaa, pia usiwasahau matibabu ukisikia wanaumwa wasogezee hukohuko walikozoea watakushukuru mara elfu na wataishi idadi ya siku alizowapangia M /Mungu.
 
Back
Top Bottom