Rumishaeli
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 227
- 72
Nimejaribu kukaa na kufikiri na kila ninapomsikiliza Raisi John Pombe Magufuli akiongea huwa lazima aseme mniombee ili aweze kufanikisha azma yake ya kuiona Tanzania mpya, nikaona pamoja na hayo ni vyema basi Raisi akaweka walau siku moja katika kila mwaka kama NATIONAl PRAYER DAY (SIKU YA KULIOMBEA TAIFA)
Ni ukweli usiopingika kwamba mtu akiwa na hofu ya Mungu awe mkristo, muislamu au mpagani mambo huenda vizuri. Na siku zote ukimuweka Mungu kuwa wa kwanza mambo yote hunyooka, ni kama vile umeandika 1 halafu mengine yakafuata ambayo ni kama unaandika sifuri mbele ya moja. Mwisho wa siku unakuta umeandika namba moja ambayo ni kubwa sana.
Mfano amemuomba Mungu amtangulie kwa yote hiyo ni 1 umeandika, then akaanza kupambana na rushwa hiyo ni 0 umeandika mbele ya moja, then akaendelea na kupambana na watumishi hewa hiyo ni 0 ya pili ameandika mbele ya 1.
Sasa hivi kuna vikundi vidogo vidogo vinavyofanya hivyo yaani kukusanyana na kuliombea Taifa ila hili swala linapaswa kuchukuliwa kwa uzito kitaifa hapa ndipo tutakapoona mafanikio. Lakini vita bila kumtanguliza Mungu (Allah) ni vigumu kupata mafanikio.
Ni hayo machache tu. Mimi si mtaalamu wa kuandika sana. ila nafikiri michango yenu itakuwa productive na wenye mamlaka watafanya hivyo wakiona inawapendeza.
Thanks