Hili ni bomu la hatari sana ingawa tunalichekea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili ni bomu la hatari sana ingawa tunalichekea

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dark City, Jan 12, 2009.

 1. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Nimekuwa nikifuatilia hii hali ya wananchi kufurahia kupewa misaada. Kwanza kuna misaada au michango inayotolewa na viongozi kama vile wabunge, mawaziri na hata Rais mwenyewe. Pili kuna misaada inayotolewa na makampuni au wafanyabiashara binafsi. Kwa maoni yangu hili ni bomu la hatari sana kwa vile ni chanzo na pia chaka la ufisadi na matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi pale inapohusisha viongozi wakubwa.
  Nimekuwa nikijiuliza, mbunge anapata wapi pesa za kujenga shule au zahanati? Na kwa nini atoe hizo pesa katika mazingira ya kushawishi wananchi wamkubali? Huu ni ufisadi wa kutisha na ndio chanzo cha EPA zisizoisha.
  Je Mawaziri na Rais mwenyewe wanapata wapi pesa za kutoa misaada au eti kuchangia miradi ya maendeleo? Zinatoka kwenye bajeti ya serikali au mifuko yao na kwa nini?
  Makampuni au wafanyabiashara wanapotoa misaada au kuchangia miradi ya maendeleao wanatumia sheria gani kufanya hivyo? Na je watafaidi nini kutokana na michango yao?
  Huko nyuma sikuwahi kusikia Rais (mfano Mwalimu) akichangia mradi wa maendeleo au kutoa misaada ya kizushi. Nadhani ni vizuri pesa zote zitoke kwenye bajeti. Na wafadhili watoe misaada yao kwa serikali za mitaa (au Mashirika ya hisani kama hawana imani na Local governments) ili zitekeleze majukumu yake kutegemea ni mipango waliyojiwekea. Na mwisho makampuni au wafanyabiashara wakitoa misaada basi iwe katika viwango vinavyofuata sheria (kama ipo). Vinginevyo tunzidi kulea hali ambayo kila mtu akifika kijijini (ili mradi katoka mjini au ni mfanyakazi) basi kwa wananchi walio wengi huyo mtu wa kutoa misaada au michango isiyo na mpangilio.
   
Loading...