TandaleOne
JF-Expert Member
- Sep 4, 2010
- 1,644
- 709
Alitaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi hicho kuwa ni ujenzi wa shule za sekondari za kata, zilizoondoa tatizo la watoto wanaofaulu na kushindwa kuendelea sekondari kwa kukosa nafasi.
Mama Salma alisema, ujenzi wa shule za sekondari umeongezeka kutoka 1,745 hadi 4,102 katika kipindi cha miaka mitano, jambo ambalo ni mafanikio makubwa, lakini kuna watu wanaojifanya kutoyaona.
Katiba inamtambua huyu mama kama mwanasiasa au mke wa rais anaeomba ridhaa ya wananchi tena?
Hivi huyu Mama alishawahi kutembelea zile shule za msingi alizokuwa anafundisha? Natumaini HAPANA - vinginevyo asingethubutu kutamka hayo maneno!
BTW: Haya majengo (mengine hayana hata madirisha) yanayopewa jina "shule za kata" ni SHULE kweli?
Wakati mwingine ni busara kumuongelea mtu aliyetoa ujumbe kabla ya kuzama katika ujumbe wenyewe.Unamjua Michelle Obama????Na yule aliyepandishwa jukwaani na magwanda??Hii forum sijui inakuwaje.Mnaongelea watu badala ya ujumbe.Kweli waafrika.
Wakati mwingine ni busara kumuongelea mtu aliyetoa ujumbe kabla ya kuzama katika ujumbe wenyewe.
Fuatilia utajua kama kweli unataka kujua aliwahi kutembelea au la.Wanafunzi wangapi wameenda form 5 na 6 kutoka shule za kata???Jiulize hilo swali.Acha ubinafsi.Kama si hizo shule wangekuwa wapi???Hakuna msomi makini asiyejua mapigano ya nchi masikini kutoka katika umasikini wake hupitia nyakati zipi.Nyakati za maopportunists na manabii wa uongo wa kisiasa ambao wanatupa mema yote na kusimama kusema mabaya kwa nguvu zao zote.Ila umma makini huwatambua.
Kutokana na kuongezeka kwa shule hizo, alisema idadi ya wanafunzi nayo imeongezeka ambapo uandikishaji wa kidato cha kwanza hadi cha nne ulitoka kuwa wanafunzi 401,598, mwaka 2005, hadi 1,401,559 mwaka 2009.
Jumla ya watahiniwa 55,764, ambao ni asilimia 88.86 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani huo mwaka huu
Fuatilia utajua kama kweli unataka kujua aliwahi kutembelea au la.Wanafunzi wangapi wameenda form 5 na 6 kutoka shule za kata???Jiulize hilo swali.Acha ubinafsi.Kama si hizo shule wangekuwa wapi???Hakuna msomi makini asiyejua mapigano ya nchi masikini kutoka katika umasikini wake hupitia nyakati zipi.Nyakati za maopportunists na manabii wa uongo wa kisiasa ambao wanatupa mema yote na kusimama kusema mabaya kwa nguvu zao zote.Ila umma makini huwatambua.
Matokeo yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) mwishoni mwa wiki, yanaonesha kuwa kati ya shule hizo, 26 zilizoko katika Wilaya za Kinondoni na Temeke, zimefanya vibaya baada ya jumla ya wanafunzi wake 2,321 kufeli,
huku 2,963 wakifaulu kwa kiwango cha daraja la nne.Kwa mujibu wa matokeo hayo, kati ya shule zilizofanya vibaya, baadhi zimefikisha wanafunzi 119, nyingine 129 na nyingine 176 waliofeli, huku waliofaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza wakiwa ni 45.
Jumla ya waliofaulu kwa kiwango cha daraja la pili katika shule hizo,
ni 120 wakati waliofaulu kwa kiwango cha daraja la tatu wakiwa 533.
Huyu mama anaugonjwa wa mumewe! Nadhani naye akili zinaanza athirika nasubiri aanze kula mieleka!
Huyu mama anaugonjwa wa mumewe! Nadhani naye akili zinaanza athirika nasubiri aanze kula mieleka!
Mbona alishaanza!! Siku mme wake ameanguka jangwani na yeye alianguka pia.
Ila ananikera kweli kwa kitendo cha kujivunia ujenzi wa shule ambazo watu tuliuza hadi vijiko ili tutoe michango ya ujenzi wa hizo shule! Sijui kwanini hao anaowahutubia hawamuulizi haya? Mwenzake Mkapa alitekeleza MMEM bila kututoza hata shilingi moja. Sasa huyu Kikwete katuchangisha hadi senti ya mwisho bado anajisifia.
By the way, shule ni majengo au wanafunzi, walimu, vifaa vya kufundishia na samani? Huyu jamaa inaonekana hakutaka kabisa kujifunza kutoka kwa Mkapa wakati anatekeleza MMEM, kwa sababu mwenzake pamoja na kuongeza udahili wa wanafunzi almost kwa asilimia 100, bado hakukuwa na shida kubwa ya walimu na vifaa vya kufundishia kama ambavyo imekuwa kwake. Nina wasiwasi na aina ya watu anaowahutubia. Manake katika hali ya kawaida, hotuba kama hii inapaswa kuwa na maswali kibao.
[
Takwimu ya waliofanya mtiahani Form SIX 2010 kutoka NECTA hii hapa:
Kama kujiandikisha Form I-IV umefikia 1.5mil sasa inakuwaje wanaomaliza Form VI hawafiki hata 100,000?
Unajua vijana wangapi wako pale UDSM kutoka hizo shule unazozizarau???Leo wangekuwa wapi kama si hizo shule??Acheni ubinafsi.Watanzania wanasoma comments zenu na wanaona upungufu wa akili zenu.
uwezo wako wakufikiri wewe unayeisifia ccm ambayo imezeeka haina jipya haina mtazamo mpya kazi kuturudisha na kututesa na umaskini cha uhanga wa ujinga wewe huoni umaskini uliotopea huwenda wewe pia nifisadiunajua vijana wangapi wako pale udsm kutoka hizo shule unazozizarau???leo wangekuwa wapi kama si hizo shule??acheni ubinafsi.watanzania wanasoma comments zenu na wanaona upungufu wa akili zenu.
Anayependa maendeleo atatambua mafanikio ya serikali-Mama Salma
NA JACQUELINE LIANA, BAGAMOYO
MWENYEKITI wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete, amesema mtu anayependa maendeleo nchini, atatambua mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa serikali ya awamu ya nne.
Akizungumza kwa nyakati tofauti na wanawake wa wilaya za Kibaha, Chalinze na Bagamoyo, mkoani Pwani jana {24.8.2010}, alisema mengi yaliyoahidiwa na Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu wa 2005, yametekelezwa.
Mama Salma Kikwete alisema, katika suala la maendeleo na mustakabali wa nchi, ni lazima wanawake waangalie ni chama gani chenye sera na ilani makini, katika kuwaletea maendeleo yao, na jamii yote ya Watanzania.
Alitaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi hicho kuwa ni ujenzi wa shule za sekondari za kata, zilizoondoa tatizo la watoto wanaofaulu na kushindwa kuendelea sekondari kwa kukosa nafasi.
Mama Salma alisema, ujenzi wa shule za sekondari umeongezeka kutoka 1,745 hadi 4,102 katika kipindi cha miaka mitano, jambo ambalo ni mafanikio makubwa, lakini kuna watu wanaojifanya kutoyaona.
Kutokana na kuongezeka kwa shule hizo, alisema idadi ya wanafunzi nayo imeongezeka ambapo uandikishaji wa kidato cha kwanza hadi cha nne ulitoka kuwa wanafunzi 401,598, mwaka 2005, hadi 1,401,559 mwaka 2009.
Kuhusu miundombinu, alisema ujenzi wa barabara zinazounganisha mikoa na wilaya nchini umewezesha wananchi kusafiri kwa haraka kutoka sehemu moja ya nchi kwenda nyingine, ikilinganishwa na hali ilivyokuwa huko nyuma.
"Zamani ilikuwa kutoka hapa (Kibaha), hadi Lindi tulilazimika kulala njiani, lakini sasa mambo ni mazuri," alisema na kupigiwa kofi.
Alisema, Chama Cha Mapinduzi kimetekeleza ilani yake kwa mafanikio makubwa, na asiye na macho haambiwi tazama, kwani wengine wanaona mafanikio hayo lakini wanajifanya hawaoni," alisema.
Mama Salma aliwaomba kina mama hao kuwachagua wagombea wa Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 31, mwaka huu katika mtindo maarufu wa CCM wa mafiga matatu.
"Siku ya tarehe 31 mwezi wa kumi, ukifika kituoni piga kura kwa mgombea urais wa CCM, mgombea ubunge wa CCM na mgombea udiwani wa CCM hayo ndiyo mafiga matatu," Alisema.
Akizungumzia kura za maoni za CCM kuwapata wagombea ubunge na udiwani, Mwenyekiti wa WAMA alisema, zilisababisha makundi tofauti kwa sababu wagombea walikuwa ni wengi.
Kwa vile mchakato huo umemalizika na wagombea kupatikana, aliwasihi wanachama wa CCM kuvunja makundi hayo na kuwa na kundi moja la CCM kwa ajili ya kukipatia Chama Cha Mapinduzi ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao.
Kesho, (Agosti 25, 2010) Mama Salma Kikwete ataendelea na ziara ya kuzungumza na wanawake katika wilaya za Kisarawe, Mkuranga na Rufiji, na Agosti 26, 2010 anatarajiwa kuwa Mafia.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
'Zingatieni masharti mikopo isaidie wengi'
*Ni kauli ya Mama Salma kwa kinamama
God Bless Our Country and protect it from liars,disorganized and crazy people