Hili ndilo balaa la mapenzi

jamii01

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,974
1,401
Kuna dada mmoja nimetokea kumpenda sana ana miaka 29 sawa na umri wangu,katika kumfuatilia akaniambia ana jamaa yake yuko nje anasoma,ukweli mie sikuamini sababu tangu nimfahamu huyu dada kama miaka 3 iliyopita sijawahi kumuona na mwanaume yoyote wala kusikia kuwa anaboyfriend....nikaendelea kumfuatilia lakini maneno yake yakawa kama sitaki nataka..nikajipa moyo mwanaume na rafiki zangu wakanipa moyo sana kuendelea kufuatilia..baadaye yule dada akaniambia nimekwisha chumbiwa nikajua masiala..sababu nilipokuwa nampigia cim mda mwingine anapokea mara anapotezea na sms hivyo hiyo..

Wiki iliyopita sijui imekuwa vipi au sijuiyule dada alimwambia jamaa yake..mara nikaona simu number mpya hata sijui..jamaa kanisalimia akajitambulisha majina yake matatu akaongea kwa ustarabu tu kama vile tu nafahamiana story kama mbili tatu hivi baadaye akaniambia Tafadhari kaa mbali na mchumba wangu ambaye ni huyo dada.. akamtaja jina kisha akasema niache kumsumbua huyo dada wala kumfuata fuata sababu alikwisha mtolea mahari na tarehe ya arusi akanitajia.

Kwa kweli niliishiwa nguvu na sikuamini huyu dada angeweza kunifanyia hivi kwa nini asingesema mapema hakiwa serious na kwa nini aliamua kunisema kwa mchumba wake sababu inaonyesha alimpa full information zangu zote.nimepoteza zaidi ya miaka 2 namfuatilia huyu dada..

Naomba ushauri nifanyeje ili niweze kumsahau na kumtoa kwenye moyo wangu huyu dada..ukweli nampenda sana miaka 2 namfuatlia huyu dada lakini hakuna kitu.nimejaribu kumpa kila kitu nilichokuwa nacho ili aweze kusema ndiyo lakini alikataa kila kitu.siku ya tatu nalala naweweseka kwa ajili yake nampigia simu anasema hiyo ndiyo hari halisi.nikamuomba nitoke naye hata one night dinner kagoma.nifanyeje mimi......
 
pole sana..........

inaelekea ulizama haswa mapenzini, kumfuatilia mtu miaka 2 si mchezo, na inaonyesha ulipenda kwa dhati, lakini bahati haikuwa yako....

kama mdada alivyokwambia alikuwa kachumbia, uliyafumbia macho yote hayo kwa sababu ya mapenzi.... na usikute alipokwambia ana mtu kamtolea mahari, yupo masomoni ukadhani mdada hayupo serious kwa sababu tu hujawahi kumuona na mtu wala kupata habari zake, kumbe dada wa watu alikuwa anajitunza kwa ajili ya mchumba wake wewe ukadhani hayupo serious au analeta pozi za'kike?"

ila yote hayo ni maisha, huyo dada na mchumba wake wanapendana, mpaka mwanamke kajitunza miaka yote kumsubiria mtarajiwa yake........ na kwa mwanamke ajayejiheshimu hawezi kutoka na wewe ilhali anajua huo ni mtego.....

pia inawezekana alimpa mtarajiwa wake namba yako baada ya kuona upo serious zaidi, au kila akikuambia nae mtu wake bado wewe unamng'ang'ania, au kumfutilia kwako(kumbuka miaka 2 ni mingi) kumegeuka kero kwake, au ameona ndo njia muafaka ya kukufanya umuache awe na amani......

ofcourse maumivu ni makubwa, ukizingatia umewekeza hisia zako hapo...
lakini huo si mwisho wa dunia, kwenye maisha huwezi kupata kila ukitakacho .....
kwanza kubali hali halisi kuwa huyo dada tayari "keshawahiwa"
jitahidi umuone ni wa kawaida
punguza kumpigia simu
punguza kumuona
muepuke
go ut jichanganye na marafiki
in time utamsahau..... si rahisi kama unavyodhani lakini wanasema "time heals"
kwa wakati utajikuta unazoea
kwa wakati utajikuta unamsahau, hata ukimuona kiroho hakitashtuka.... na mwisho wa siku utamchangia sendoff take na kuhudhuria harusi

na mwisho wa siku utampata wako.... wako peke yako....

nakutakia christmass njema.....

time is the best healer....unaumia kwa sababu ni mwanzo wa kuwa dumped,ila with time utamsahau tu...jikeep busy fanya mazoezi mwili uchoke au find new hobby kama swimming itayooccupy muda wako na mind yako hivyo kutomfikiria....ila usimlaumu aisee alikwambia mapema,sema mapenzi yako kwake yakakutia upofu....au labda na yeye hakuwa sure amchague nani kati yenu ndio maana akakuweka mguu ndani mguu nje,sasa ameshafanya decision wewe cha kufanya ni kuaccept na kuheshimu mawazo yake.its hard but try....
 
Mkuu! Si kila siku kama maelezo ya picha hayasomeki vizuri basi tuangalie picha yenyewe. Sasa wewe vyote huvioni tatizo liko kwako. Na utakua na ziada ya tatizo ikiwa akili yako itasome baada ya huyo wanawake wamekwisha duniani.
 
Siumeshasema alikutaarifu kwamba ana mchumba wake?Watu jifunzeni kuchukulia HAPANA kama HAPANA na sio NDIO. Sio kila mwanamke ni nataka sitaki.

Alafu unachekesha kweli. . . . kwahiyo wewe mtu akipokea simu yako basi kakukubalia?Grow up na ujifunze kusikiliza na kuelewa. Sio unang'ang'ania hata visivyong'ang'aniwa.
Ningekua namfahamu huyo dada ningempa zawadi, au kama vipi mfikishie salam zangu.Mwambie "yeye ni mwanamke wa shoka, Lizzy anamkubali."
 
hakuniambia katika mazingira ya kuwa serious hadi kufikia hatua ya kuamini.nakama alikuwa hataki si angesema sitaki kwa kuonyesha moja kwa moja..na kwa nini alikuwa anakubari kushare naye idea zangu,future za maisha...
 
Unashangaza kweli. . . .
Huo usiriaz unaotaka labda sio asili yake.Siku nyingine chukua unachoambiwa bila kujidanganya vile unavyopenda wewe.
 
hakuniambia katika mazingira ya kuwa serious hadi kufikia hatua ya kuamini.nakama alikuwa hataki si angesema sitaki kwa kuonyesha moja kwa moja..na kwa nini alikuwa anakubari kushare naye idea zangu,future za maisha...

hee! Kumbe watu kama nyie mpaka tuwe tunawatukana ndio mjue tumemaanisha hapana!
 
Umejitakia mwenyewe mambo yote haya, wanawake wengine wakisema No wanamaanisha No, usidhani kila mtu ni SITAKI NATAKA, wenye heshima zao huwa wako straight! Pole sana jitahidi kumsahau na usikae karibu nae usije ujaanza kutongoza tena. Ila ata yeye alikosea kumwambia huyo jamaa akupigie, yeye mwenyewe alitakiwa kujiamini na kukujeleza black and white bila kulazimika kumwambia huyo mwanaume, Huyo mwanaume naye kwa upande mwingine pia alikosea, kwani siku mkewe akitongozwa na akamkubali mwanaume mwingine wa nje atamwambia mumewe??
 
hahahahahah....kijana pole ila umenifurahisha sana
let me tell u something kaka...no nation has benefited from prolonged warfare. unatakiwa wakatu unafuatilia unaangalia na mkao wa huyo demu wewe miaka miwili bado tuu hujaona kuwa hakuna kitu hapa. sasa kubali yaishe mwana wewe ndio kwishakula kwako...time itapita na u will find another
 
hivi unawezaje kumfuatlia mtu kwa miaka miwili???????
na unazungumza kama kitu cha 'kujivunia'
si ajabu huyo mchumba wake hakuchukua hata miezi sita 'kumaliza kazi'
 
sasa kaka angu, alishakwambia kuwa ana mtu wake na ametolewa na mahari, we bado tu unaganda, aiseeh, ni vizuri tukajaribu kuheshimu majibu ya wenzetu,pole lakini
 
Pole kwa kutoa kila kitu chako na kupoteza muda wako...inaelekea ulipenda haswaaaa bila kusoma alama za nyakati. Ukitaka kumsahau huyu binti,kubali matokeo..baaaaaasi!! Maana mpaka kakusemea kwa mtarajiwa wake ujue hataki masihara na wewe...sawa kaka?!
 
Mkuu hii thread yako na maelezo yako sidhani kama umefikisha miaka 29 au age zenu zipo hapo,coz maelezo yanaonyesha kwamba ndio kwanza mgeni wa mapenzi yaani ndio kwanza unaingia kwenye hizi anga,

Achana nae na mpotezee, wanawake wa siku hizi ndio walivyo mkuu tafuta mwanamke mwingine mbona wanawake ni wengi sana kuliko hata wanaume so why ujichanganye na huyo msichana,ingia facebook utakutana na kila aina ya wasichana.
 
Kuna dada mmoja nimetokea kumpenda sana ana miaka 29 sawa na umri wangu,katika kumfuatilia akaniambia ana jamaa yake yuko nje anasoma,ukweli mie sikuamini sababu tangu nimfahamu huyu dada kama miaka 3 iliyopita sijawahi kumuona na mwanaume yoyote wala kusikia kuwa anaboyfriend....nikaendelea kumfuatilia lakini maneno yake yakawa kama sitaki nataka..nikajipa moyo mwanaume na rafiki zangu wakanipa moyo sana kuendelea kufuatilia..baadaye yule dada akaniambia nimekwisha chumbiwa nikajua masiala..sababu nilipokuwa nampigia cim mda mwingine anapokea mara anapotezea na sms hivyo hiyo..

Wiki iliyopita sijui imekuwa vipi au sijuiyule dada alimwambia jamaa yake..mara nikaona simu number mpya hata sijui..jamaa kanisalimia akajitambulisha majina yake matatu akaongea kwa ustarabu tu kama vile tu nafahamiana story kama mbili tatu hivi baadaye akaniambia Tafadhari kaa mbali na mchumba wangu ambaye ni huyo dada.. akamtaja jina kisha akasema niache kumsumbua huyo dada wala kumfuata fuata sababu alikwisha mtolea mahari na tarehe ya arusi akanitajia.

Kwa kweli niliishiwa nguvu na sikuamini huyu dada angeweza kunifanyia hivi kwa nini asingesema mapema hakiwa serious na kwa nini aliamua kunisema kwa mchumba wake sababu inaonyesha alimpa full information zangu zote.nimepoteza zaidi ya miaka 2 namfuatilia huyu dada..

Naomba ushauri nifanyeje ili niweze kumsahau na kumtoa kwenye moyo wangu huyu dada..ukweli nampenda sana miaka 2 namfuatlia huyu dada lakini hakuna kitu.nimejaribu kumpa kila kitu nilichokuwa nacho ili aweze kusema ndiyo lakini alikataa kila kitu.siku ya tatu nalala naweweseka kwa ajili yake nampigia simu anasema hiyo ndiyo hari halisi.nikamuomba nitoke naye hata one night dinner kagoma.nifanyeje mimi......

Ushauri ameshakupa mwenye mali, unless kama unataka upotoshaji tu.... ACHA HIYO KITU
 
Demu alikuwa anaweka msisitizo kwa jamaa ili jamaa amuamini zaidi, sio mchezo aisee, ndio hivyo lakini ila demu kafanya makosa kumwambia jamaa ni mambo ya kishamba tu!
 
Demu alikuwa anaweka msisitizo kwa jamaa ili jamaa amuamini zaidi, sio mchezo aisee, ndio hivyo lakini ila demu kafanya makosa kumwambia jamaa ni mambo ya kishamba tu!
Ushamba wake uko wapi?
Mnafahamu mazingira yaliyosababisha amweleze?Kama msg za huyu mshkaji zilikua hazikomi?Kama alikua anapiga simu hovyo hata nyakati za usiku? Asimwambie mchumba wa ukweli kisa ni ushamba?

Kweli kazi tunayo, mtu akiwa mkweli (sikutaki,nna wangu, akimweleza mwenzake ukweli kuhusu wewe ukaonywa) TABU. Simsumbue wanaotaka huo usumbufu. . . . !
 
Yote 9,kwan we lizzy haunaga ma sleeping? Kunakucha ivyo.
 
Back
Top Bottom