Hili nalo linatatiza katika siasa za bongo....

Simcaesor

Senior Member
Jul 15, 2011
111
8
WanaJF wanasiasa kushikana mashati na viongozi wa sirekali inaashilia kitu gani au inaonesha indicator ipi katika ukuaji wa demokrasia nchini. mfano wale ngugu zangu watatu na mkuu wa wilaya, mi sielewielewi mpaka sasa hivi tunaenda wapi tunakua au tunaporomoka kisiasa?
 
Bishop Hiluka

JF-Expert Member
Aug 12, 2011
6,960
13,564
Inaashiria kuwa magwanda wanataka kuingia madarakani kwa nguvu

Nguvu ni matumizi ya mwisho kabisa ya akili; inamaanisha kuwa mahali ambapo akili
inatumika kufanya kazi, nguvu huwa haihitajiki au inahitajika kwa kiwango kidogo sana.
Ukiona mtu anatumia nguvu kufanya jambo fulani, ujue kuwa uwezo wa akili yake
katika ufanya jambo hilo umefikia ukomo na kwa wakati huo mtu huyo huwa hana
akili ya ziada ya kufanyia jambo husika, isipokuwa kutumia nguvu.
Kwa tafsiri rahisi
ni kwamba ukiona mtu anatumia nguvu katika jambo fulani kwa wakati huo huwa ni
‘mjinga’ kwa sababu huwa hana akili mbadala ya kuepuka nguvu kufanya jambo hilo.
 
ndetichia

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
27,772
6,528
WanaJF wanasiasa kushikana mashati na viongozi wa sirekali inaashilia kitu gani au inaonesha indicator ipi katika ukuaji wa demokrasia nchini. mfano wale ngugu zangu watatu na mkuu wa wilaya, mi sielewielewi mpaka sasa hivi tunaenda wapi tunakua au tunaporomoka kisiasa?

na wao watu wa serikalini kuingilia mambo ya siasa ndio kigezo kikubwa cha watu kurushiana makonde..
 
THINKINGBEING

JF-Expert Member
Aug 9, 2010
2,778
1,303
WanaJF wanasiasa kushikana mashati na viongozi wa sirekali inaashilia kitu gani au inaonesha indicator ipi katika ukuaji wa demokrasia nchini. mfano wale ngugu zangu watatu na mkuu wa wilaya, mi sielewielewi mpaka sasa hivi tunaenda wapi tunakua au tunaporomoka kisiasa?
Kawaulize polisi maana ya kumtia nguvuni mhalifu.
 
only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,524
WanaJF wanasiasa kushikana mashati na viongozi wa sirekali inaashilia kitu gani au inaonesha indicator ipi katika ukuaji wa demokrasia nchini. mfano wale ngugu zangu watatu na mkuu wa wilaya, mi sielewielewi mpaka sasa hivi tunaenda wapi tunakua au tunaporomoka kisiasa?

Sikuelewi unataka tuchangie nini hasa....Ni bora kujiandaa kabla ya kuleta thread hapa JF,Jamani tunakazi kwa hiyo tukiamua kusoma thread yako tumeipa heshima sana,sasa tukikuta ni majitaka inauzi....
 
zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
1,448
2,640
Lakini mleta mada anayo point. Kwamba kwa mwanasiasa kumkaba koo mtendaji wa serikali je ni ukuaji wa demokrasia au ni kuporomoka? Jibu langu ni ukuaji wa demokrasia. Hasa ukizingatia mazingira ya jinsi shughuli za kidemokrasia Tanzania zilivyohatamiwa na chama tawala chenye kiburi cha kutumia watendaji wa serikali na nguvu za dola kwa manufaa ya maslahi yake kinyume na katiba ya nchi. Sasa watu wa kawaida wameisoma katiba ya nchi na wameielewa na inapotokea mtendaji wa serikali anafanya isivyo na watu hao wanapomgundua, kumkaba koo ni ishara kwamba hawajafurahishwa na hicho kitendo anachofanya; ni alama ya kukua kwa demokrasia kunakodhihirisha kwamba vitendo hivyo havitavumiliwa na nguvu ya umma katika serikali inayokuja.
 
Simcaesor

Senior Member
Jul 15, 2011
111
8
na mashaka na upeo wako kwenye kufikili afu wewe ni mshabiki siyo mtafakali, kuelewa muelekeo mzuri ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa
 
NEW NOEL

JF-Expert Member
May 21, 2011
862
405
Kwanza yakupasa ujiulize,nini maana ya Demokrasia? Kwa uelewa wangu Demokrasia maana yake ni uhuru wa mtu au kikundi cha watu kushiriki jambo lolote ambalo ni lenye manufaa kwao pasipo na kuvunja sheria. Sasa unapozungumzia suala la kushikana mashati kati ya vyama vya siasa unashindwa kueleweka. Yakupaswa kuwa muwazi.
 
Bakeza

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
348
191
Sio lazima kupost thread waweza acha au ukawa mchangiaji ama msomaji tu. Sheria zinaruhusu. Kwa taharifa yako kama umetumwa kawaambie walokutuma hatudanganyiki wanafiki wakubwa nyie.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom