Hili muhimu sana kuingizwa ktk KATIBA mpya

Hili muhimu sana kuingizwa ktk KATIBA mpya

Erastojhn

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
244
Reaction score
229
Hbr wana jf,napenda kuwakumbusha hasa wale wenzetu ambao hawajatembelewa na tume ya kukusanya maoni au watakaoiandikia tume kwa barua au e-mail kuwa napendekeza baada ya kufuatilia utaratibu wa marekani katika kumpata mgombea urais katika chama kwa awamu tatu sasa yaani miaka 12,nimebaini na kuufurahia utaratibu wao ambao kama tutautumia hapa tanzania tutapata rais ambae atakuwa amechaguliwa na wananchi wa kawaida na ambae atakuwa powerful na asibanwa na marafiki ambao hupitisha jina lake kwenye kikao cha chama,mfumo wao uko hivi:kila chama-tawala na upinzani wanawakilisha majina ya wagombea na si viongozi wa chama wanaoteuwa mgombea kwani kunakuwa na utaratibu ambapo kila chama mf km ni hapa kwetu tz wagombea urais kupitia ccm wanapangiwa ratiba ya kufanya kampeni kila mmoja na sera zake na mipango yake akiwa rais wanaenda mikoani na tarehe ya kupiga kura kwa wanachama wao inakuwa inajulikana na mgombea aliyeshinda na jumla ya kura alizopata sambamba na wagombea wengine mwisho wa sk aliyekusanya kura nyingi zaidi nchi nzima ndo anakuwa mgombea wa urais kupitia chama husika chamani anaenda kupata baraka za chama,mfumo wetu wa sasa unasababisha rushwa kwa rais mtarajiwa ambae pia hutengeneza mtandao wa watu ambao ni wachache wanakuwa kwenye halmashauri kuu mf ya ccm ambapo mtu wao anapokuwa rais haohao ndo huwateua kushika nyadhifa mbalimbali na hata wakiharibu au kufisidi mali na fedha za umma hawez kuwashitaki mfano ulio hai ni viongozi wa sasa,rais is now powerless though is basically powerful,huu ndo mfumo wa wamarekani na unasaidia sana kuondoa migogoro vyamani kwan wananchi wa chini kabisa ndo wanamteua mgombea urais wamtakao na si wajumbe wa nec wa ccm au chadema ambao ni wachache sana hivyo kuhonga wajumbe wakuchague inakuwa rahisi na ndipo pia viongozi wengine huahidiwa vyeo endapo wanamchagua mtu wao atakaeshinda urais,watanzania tafakarini mfumu huu na mtoe maoni yenu,nawasilisha
 
Back
Top Bottom