Hili litasaidia Timu yetu ya Taifa

Hili litasaidia Timu yetu ya Taifa

MO11

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2014
Posts
19,698
Reaction score
42,008
Kwa miaka zaidi ya ishirini timu yetu ya taifa haifanyi vizuri kimataifa hii naitafsiri kama mkosi sio vinginevyo.

Daahh.....!! Katika kuuliza uliza nikasikia kipindi cha nyuma utawala wa Alhaj Ally Hassan Mwinyi alisema eti "MPIRA WA TANZANIA NI KICHWA CHA MWENFAWAZIMU" duhhh....!! nilisikitika yaani hii ni laana kutoka kwa mzazi kwenda kwa mtoto. Hivyo haina budi iondolewe tupate baraka badala ya laana.

Mh. Jamal Malinzi hii laana inatuandama sio siri na haitoisha mpaka iomdolewe. Itaondolewaje ??

Andaa (tayarisha) mechi ya kirafiki kwa timu yeyote hapa afrika kisha siku hiyo muombe mh rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi ajumuike na wachezaji kuanzia chakula cha mchana hadi uwanjani awepo. Kabla ya mechi kuanza apewe kipaza sauti na umwombe aondoe ayafute yale maneno yake ya "MPIRA WA TANZANIA KICHWA CHA MWENDAWAZIMU" hapo laana iliuodumu kwa zaidi ya miaka 20 iondoke. Hiyo mechi tutashinda mpaka tutakapo kwenda kombe la dunia Uarabuni.

kwako Jamal Malinzi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom