hili linchi!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

hili linchi!!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by steveachi, Jul 27, 2012.

 1. steveachi

  steveachi JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 4,127
  Likes Received: 1,726
  Trophy Points: 280
  kwa kweli sijivunii kabisa kuwa raia wa nchi hii,cjui kwa nn nilizaliwa hapa,hata majirani zetu wanatudharau sana,wanatuona sie ndo mapimbi namba mja duniani,kwani tuna kila kitu kinachoweza kutufanya tuwe juu kwa kila kitu lakini waaapi,ndo maana nikisafiri kwenda nchi za nje mi najifanya ni msenegali tu kuepuka hii aibu
   
 2. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Ni wazi kwamba hukuchagua kuzaliwa nchini kwetu lakini unaweza kuchagua wapi ukaishi, kwa hiyo unaweza tu ukaamua kwenda huko kwa majirani zako kimya kimya! Mimi nafikiri labda hao majirani zako hukuwaelewa vizuri nafikiri walimaanisha wewe na familia yako ndio mapimbi na sio watanzania woote, sio kila mtu anaweza kuelewa mwingine anamaanisha nini hasa ukichukulia kama upande wa mpokeaji habari ana ubongo mdogo kama ulivyodhihirisha!

   
 3. Mapondela

  Mapondela JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Allah ana sababu zake za kukufanya uzaliwe huku
   
 4. Neiwa

  Neiwa JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 730
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  steveachi unadhani maisha ni rahisi rahisi? Be the change you want, kama kuna kitu kinafanya usiipende kuwa kati ya wale wachache na wenye udhubutu wa kuleta mabadiliko for the better instead ya ulalamishi... Na aliye zaliwa Somalia, Syria aseme nini? Hizi ni kufuru mkuu..
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. m

  mwaqsa Member

  #5
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 25, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hellow,kila nchi ina mapungufu yake,na katika nchi zingine kuna wananchi wengine wanataman wangezaliwa Tz,i'm proud to be Tanzanian.
   
 6. ndupa

  ndupa JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2012
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 4,448
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  najivunia sana kuwa mwafrica hasa wa tz..ila sasa kila nikichek hali ilivyo hapa nchini kwetu naishiwa nguvu!!! dah mungu bariki tz na uiponye pia.....
   
 7. f

  filonos JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 651
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  wewe kweli unasafili nnchi za nnje kweli???unawajua hao Wasenegar maisha yao yalivyoo??? wangekua na maisha wasingekua wana tembea na MAIRIZI...mwili mzima maana nao wameisha kata Tamaa ya Maishaa......
   
 8. m

  markj JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  dedication MISS TANZANIA- solo thang
   
 9. ndupa

  ndupa JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2012
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 4,448
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  soma nlichoandika na uelewe(kabla hujaropoka)..mimi sijaongelea maswala ya senegal!! mimi cjaongelea maswala ya kusafiri!! USIKURUPUKE KIJANA ELEWA MADA KABLA YA KUJIBU..nawakilisha
   
 10. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2012
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Mwanzisha mada kamalizia hivi ".......................... ndo maana nikisafiri kwenda nchi za nje mi najifanya ni msenegali tu kuepuka hii aibu". Swali aliloulizwa ni je, anawaelewa vizuri Wasenegali? Ni swali muhimu maana kwa kujifanya Msenegali badala ya MTZ maana yake anaona Senegali na Wasenegali ni bora kuliko Tanzania na Watanzania. Hiyo ni sawa na kuwakana wazazi wako kwa sababu hawakusoma au ni masikini. Halikufanyi uwe mzalendo bali zuzu tu.
   
 11. ndupa

  ndupa JF-Expert Member

  #11
  Jul 30, 2012
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 4,448
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  uko sawa kabisa!! Lakin kumbuka mimi sio mwanzisha mada,sasa inakuaje unanichukulia mimi kama mwanzasha mada? Hayo majib ilibid umpe yeye coz ndo aliyesema maneno hayo,kwamba anasingizia yeye ni mtu wa senegal na mengine meng!! Nadhan hap ulidandia treni kwa mbele..pole sana!!
   
 12. R

  Rebel volcano JF-Expert Member

  #12
  Jul 30, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa kuwa marekani kwenyewe ambapo wengi wenu munapaabudu kimaisha,wanchi wa huko waliandamana haswa maeneo ya wall street kutokana na ugumu wa maisha na kupigwa virungu na kuvunjiwa mahema mpaka wakarudi majumbani kwao,na kwa kuwa huko huko marekani wanajeshi waliolitumikia jeshi la huko wakipata ulemavu na kurudi kwao wanavyodhalilika kimaisha,nina kila sababu ya kujivunia kuwa mtanzania!
  mwanaume kama hukuajiriwa si mwisho wa maisha!
  mashirika mengi tajiri ya ulaya yanapunguza idadi ya wafanyakazi wake kutokana na hali ngumu ya kibiashara!
  kazeni kamba musije kuolewa watoto wa kiume!
   
 13. C

  Choi Member

  #13
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 27, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ninajivunia kuwa Mtanzania, ila mwelekeo wa nchi hii unaniumiza sana! natamani kama muujiza ungetokea ukabadilisha mitazamo na fikra zetu, kama jirani zetu Rwanda wameanza kidogo kidogo lakini wanchukua kasi wanaondoka! watatuacha hapahapa! EE MUNGU uingilie kati utusaidie!
   
 14. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #14
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 925
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Najivunia kuwa Mtanzania Halish!
   
Loading...