Habari ya leo wanajamvi,
Naanza na pongezi kwa mh. Magufuli kwa hatua yake kuzuia vituo lukuki vya ukaguzi wa magari ya mizigo yaendayo nje ya Tanzania, vilivyotapakaa mabarabarani na kubakia vituo 3 tu. Yaani Vigwaza mizani, Singida mizani na Nyakahura mizani kwa magari yaendayo kigali RwandaBujumbura Burundi, Uganda, Goma Kongo na Bukavu Kongo.
Sijui kwa njia ya Mbeya, kwa magari yaendayo lumbumbashi Kongo na vitongoji vyake, Lusaka na miji mingine, lilongwe Malawi na miji mingine n.k. Ila kama mh. Magufuli amesahau njia hiyo, basi kwa mtazamo na maoni yangu, vituo 3 vya njia ya Mbeya, viwe vigwaza, makambako na mpemba mizani.
Sasa nije upande mwingine, kauli hii safari hii iwekewe mkazo vinaambatana vitendo, maana kauli kama mh. Magufuli alishawahi kuitoa akiwa waziri wa miundombinu na hakuna kilichoendelea.Hivyo tunaomba tamko hili liende sambamba na vitendo au utekelezaji wake, kwani maaskari wa usalama barabarani na wale wa kawaida wamejiwekea vituo vyao wenyewe, ambavyo vinaleta kero na usumbufu mkubwa kwa madereva wa hayo magari.
Pia mh. Itazame ile barabara ya Nyakanazi njia panda ya Kigoma, Lusahunga njia panda ya Bukoba, Nyakahura mizani hadi Rusumo border, kwani imekuwa kero kubwa mno na ni hatari kwa usalama wa madereva na magari wanayoyaendesha, ni mbovu mno mh. kama utakuwa hauna nafasi ya kupita njia hiyo na kuona hali halisi ilivyo, basi muulize mh. Majaliwa, maana yeye alipita huko, na kujioonea mwenyewe.