Ujasirinimtaji
Member
- May 3, 2016
- 18
- 10
Katika watu ambao wanatakiwa kushukuru na wanaomba sakata la sukari liendelee,basi ni wale wenye tuhuma za matumizi mabaya ya mali za umma pamoja na rushwa.
Leo sakata la Sukari limefuta kabisa sakata la kashfa ya Lugumi,na ripoti ya CAG,leo hata waliokuwa vinara wa kutaka hatua kali za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya wote waliotuhumiwa katika ripoti ya CAG,hawazungumzi tena,leo wale wote waliokuwa vinara kwenye sakata la Lugumi hawazungumzi tena.
Hata media ambazo zilikuwa kinara kutangaza na kuandika sana masakata haya,sasa zimeyaweka pembeni,ni sukari tu,nadhani kuna watu wanaomba sukari iendelee kuwa story,matamko yatoke kila siku ili media zisahau sakata la Lugumi na ripoti ya CAG.
Leo naona hata shinikizo la bunge live limezikwa na sakata ya sukari,nakumbuka mwaka 2011 jinsi sakata la Dowans lilivyozimwa na ujio wa babu wa Loliondo,akaja jamaa mmoja kutoka Oman akasema yeye ndiye mmiliki wa Dowans,hakupata shinikizo lolote kwani media zilikuwa zimehamia Loliondo kwa Babu.
Nakumbuka wakati nchi ikiwa kwenye sakata la pesa za Escrow,ukaja ugonjwa wa Dengue,watuhumiwa wa sakata la Escrow wakapona,naona hata hawa wa Lugumi,ripoti ya CAG na WALIOKULA PESA ZA WATUMISHI HEWA,wanakwenda okolewa na sakata la uhaba wa sukari nchini Tanzania.
Angalizo,sakata la uhaba wa sukari,lisiwe ndiyo nafuu kwa wahusika wa sakata la Lugumi na waliotajwa na ripotI ya CAG.