Hili la Sitti, RITA wasikwepe kwa kutumia Polisi

Hili la Sitti, RITA wasikwepe kwa kutumia Polisi

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Posts
16,520
Reaction score
34,505
Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, mamlaka ya RITA imekamilisha uchunguzi kuhusu nyaraka za ''miss Tanzania'' na vielelezo vyote na kuvikisha Polisi kwa Uchunguzi. RITA wamedai hawajamhukumu Sitti kwa namna yaoyote,hadi Polisi watakapomaliza uchunguzi.

Katika uchunguzi wao, RITA wamemtumia mwanasheria wao ili kujiridhisha kuwa kila kitu kilifanyika kwa mujibu wa sheria.RITA hawakueleza ni nini jukumu lao kuhusiana na upatikanaji wa cheti cha kuzaliwa kutoka katika ofisi zao.

Kuna mambo yanayojitokeza hapa. Huko nyuma Rais Mkapa aliwahi kulalamika kufanya ziara ambayo aliambiwa kuna Watanzania wengi. Mwisho wa siku alikutana na Watanzania wachache, kumbe wengi wao walikuwa na passport za kughushi.

Passport hutolewa kwa kuangalia nyaraka mbali mbali ikiwemo uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa vinavyotoka RITA. Hii maana yake ni kuwa uzembe wa RITA si kwamba unaathiri sehemu moja, bali sehemu kubwa ya shughuli za kijamii hasa ulinzi na usalama wa taifa.

Tulitegemea uchunguzi kuhusu nyaraka za Sitti uambatane na jinsi aluivyoweza kuzipata kutoka RITA. Tunaelewa hakuna madai ya kuvunjwa kwa ofisi za RITA hata siku moja. Na wala hakujawahi kudaiwa uwepo wa mfumo wowote wa elekroniki ulioningiliwa na taarifa kutolewa kwa umma

Hatuna sababu za kumhukumu Sitti kwasababu nasi hatuna vithibitisho kama walivyo navyo RITA

Hata hivyo, kitendo cha kupeleka nyaraka Polisi kinaonyesha RITA wameona kitu kinachohitaji uchunguzi wa kidola

Ni kwa mantiki hiyo, tunajiuliza, iweje RITA washindwe kuwa katika nafasi ya kusema hii ni ''fojari'' au la. Hilo tu linaonyesha tatizo lililopo RITA, kwamba hawawezi kubaini kama cheti wanachotoa wao kina uhalali au hapana.

Katika hili, RITA ilipaswa kuueleza umma kuhusu uchunguzi wao kwa kina. Kwamba wamejiridhisha hakuna mtumishi aliyehusika au wapo waliohusika.

Kama wapo (kwa dhana kuwa jambo lipo Polisi) ni vipi basi wasitueleze wao walishindwaje kuzuia jambo hilo kutokea, au kama limetokea watumishi wangapi wamehusika na hatua gani zimechukuliwa dhidi yao?

Kitendo cha kupeleka hili jambo Polisi, ni njia ya kukwepa uwajibikaji.

Hapa kuna neno, kuna jambo na ndipo pa kuongelea. Hatuwezi kuhangaika na matokeo kila siku bila kujua chanzo chake ni nini.

Ahsanteni
 
Moto wa Mbunge ----- Zuberi Mtemvu tapeli la wananchi wa temeke. Like faza like dota.
 
RITA ni tatizo, naamini kuna watu wengi wasio Watanzania watapata vitambulisho vya Taifa kwa utendaji huu wa RITA. Kughushi cheti cha kuzaliwa ni suala la hatari na lina madhara makubwa kwa Taifa letu ingawa naona linafantiwa mzaha,
 
RITA ni tatizo, naamini kuna watu wengi wasio Watanzania watapata vitambulisho vya Taifa kwa utendaji huu wa RITA. Kughushi cheti cha kuzaliwa ni suala la hatari na lina madhara makubwa kwa Taifa letu ingawa naona linafantiwa mzaha,
Nakubaliana nawe, kwa nchi za wenzetu, cheti cha kuzaliwa kina determine mambo mengi sana ya mtu husika, na taifa kwa ujumla.

Sasa RITA kama hawajui cheti walichotoa ni halali au la hadi watumie Polisi, hapa kuna tatizo kubwa sana.
Kinachowasukuma ni kujibu tu tuhuma za Sitti zilizo na hisia kwa sehemu ya jamii na si tatizo zima.

Kwa hili, na jinsi wanavyokwepa kuna tatizo kubwa RITA
 
RITA wamezama zaidi kwenye ukusanyaji wa ada za vyeti wanavyotoa kuliko kuangalia uhalali wa mtu wanayempa cheti kama anastahili na hata hawaangalii usahihi wa taarifa zilizomo kwenye vyeti wanavyotoa wanategemea taarifa ya muomba cheti hata kama kadanganya RITA wanatoa tu vyeti kwa kutegemea taarifa za muomba cheti wapo watu wengi tu wana vyeti vya kuzaliwa vinavyosomeka wao ni watanzania lakini ukweli si watanzania
 
RITA wamezama zaidi kwenye ukusanyaji wa ada za vyeti wanavyotoa kuliko kuangalia uhalali wa mtu wanayempa cheti kama anastahili na hata hawaangalii usahihi wa taarifa zilizomo kwenye vyeti wanavyotoa wanategemea taarifa ya muomba cheti hata kama kadanganya RITA wanatoa tu vyeti kwa kutegemea taarifa za muomba cheti wapo watu wengi tu wana vyeti vya kuzaliwa vinavyosomeka wao ni watanzania lakini ukweli si watanzania
Ni jambo la hatari sana kwa usalama wa taifa. Ndio maana tumewahi kuwa na kanali asiye raia, mwisho wa siku akarudi kwao.

Rita ina vyombo vyote vya uhakiki, hivi inawezekanaje wasijue document iliyopelekwa kwao ni halali au la.

Hapa watu wanamuongelea Sitti kwavile ni ''celebrate'' na suala lake lina shika jamii fulani hasa wburudani.

Tujiulize kwa mwendo huu ambao RITA wameonyesha, kuna watu wangapi wana vyeti feki, passport na document nyingine za taifa hili ambao si halali. Please, watu wafikirie ukubwa wa tatizo na si kumwangalia Sitti tu.

Bila kuangalia mambo kama haya tutaishia pale pa radar, pesa zimerudi hatujui zilitokaje.
Hili la Sitti ni dalili ya hali mbaya sana iliyopo RITA

Ingawa wanaficha lakini ni taasisi yenye rushwa. Hili linaeleza bila shaka.
 
Polisi wachunguze nini tena?
Nilitegemea polisi wafanyie kazi Taarifa za RITA..wao ndio wenye jukumu la kutambua uhalali wa cheti cha kuzaliwa.

Kwa hiyo RITA wanategemea uchunguzi wa polisi kujua uhalali wa Cheti cha Sitti...
 
Polisi wachunguze nini tena?
Nilitegemea polisi wafanyie kazi Taarifa za RITA..wao ndio wenye jukumu la kutambua uhalali wa cheti cha kuzaliwa.

Kwa hiyo RITA wanategemea uchunguzi wa polisi kujua uhalali wa Cheti cha Sitti...
Ndugu yangu hapo ndipo mazingaombwe yalipo. Kwamba, Polisi wana uwezo wa kuhakiki cheti na vielelezo kuliko RITA ambao wamekiri kutoa cheti hicho.

Hivi nchi hii turaendelea kuwa na wababishaji kama RITA hadi lini?

Hili RITA wanalifanya kama shamra shamra za Sitti, hawalioni kama tatizo lao.

Ukweli ni kuwa RITA wanakwepa kwa kutambua kuwa suala la rushwa litawekwa wazi.
Hili si tatizo la Sitti, ni tatizo la RITA kuongozwa kwa rushwa.

Katika nchi za wenzetu, hao viongozi wangeshapoteza kazi. Hawajui wanachunguza nini, sasa wanafanya kazi gani?
Hawajui kuhakiki nyaraka zao, sasa wanafanya kazi gani?
 
Na wao wameingia katika ushabiki badala ya utendaji. Kuna tatizo kubwa nchi hii, si Dodoma, si magogoni wala Rita. Ubabishaji tu.
Wanataka kuifanya Tanzania iwe nchi ya viwanda, watu wanafoji nyaraka nyeti, tutarajie wimbi kubwa na raia wa nchi jirani kujazana Tanzania na kuajiriwa kama watanzania. Shamba la bibi.
 
Back
Top Bottom