Hili la Passport nalo ni jipu?

bnhai

JF-Expert Member
Jul 12, 2009
2,829
2,387
Tulikuwa tumesonga mbele sana katika utoaji wa passport. Ukikamilisha taratibu, unapewa passport. Kuna tatizo gani uhamiaji sasa hivi? Mbona tarehe za ahadi zinapita? Hayo mabadiliko ndiyo yamevuruga? Hivi tumefika mahali kila kitu lazima tupige kelele. Hivi Waziri wa Idara hii nyeti ni nani vile!!!
 
Imekuwaje Mkuu,
Mbona hawa jamaa mie naona sasa hivi wameimprove sana?? Mie nilikuwa na renew passport yangu ilinichukuwa wiki moja tu baada ya kuwa nimekamilisha vigezo vyao. Nililinganisha huduma zao Mwaka 1996 ndo mara ya kwanza kuomba passport, ilinichukuwa miezi sita kuipata. Enzi hizo vishoka kibao, mtu usipokuwa makini pesa inaliwa na Kishoka, na passport hupati au unapata passport fake., 2006 nilipoenda ku-renew ilinichukuwa mwezi mmoja. 2016 imenichukuwa week moja. Kwa mtiririko huu mie naona kama wameimprove sana. Na Customer care angalau inaridhisha kidogo japo kuna mapungufu wanayopaswa kuyarekebisha.
 
Imekuwaje Mkuu,
Mbona hawa jamaa mie naona sasa hivi wameimprove sana?? Mie nilikuwa na renew passport yangu ilinichukuwa wiki moja tu baada ya kuwa nimekamilisha vigezo vyao.
Mkuu, utaratibu wa ku-renew upoje? Passport yangu inaisha muda wake. Nahitajika kuzingatia nini zaidi?
 
Nenda Office za Uhamiaji sehemu yoyote ukachukuwe form( Kama uko Dar ningeshauri uende Makao makuu Kurasini).
Jaza form hiyo (inajieleza yenyewe). Kurudisha form wanahitaji viambatanisho vifuatavyo.
1) Kopi ya passport inayoisha (ukurasa ulio na picha yako).
2) Kopi ya kitambulisho ( Kazi, Mpiga kura au Taifa).
3) Picha passport size ( 6)
4) Barua ya Mwajiri (if any)
5) Kopi ya cheti cha kuzaliwa
6) Pesa Tshs 50,000.
Nadhani ndivyo vitu vinavyohitajika mkuu
 
Na kwa anayehitaji passport mpya inakiwaje! Kuna dogo kaenda kuulizia leo, ameambiwa mpaka apate barua ya mualiko kutoka nje ya nchi
Alternative ya hiyo barua n nn?
 
Yap hapo umemaliza kila kitu..na tena siku hizi hakuna longo longo..fasta tu unapatiwa gamba lako.
 
Nenda Office za Uhamiaji sehemu yoyote ukachukuwe form( Kama uko Dar ningeshauri uende Makao makuu Kurasini).
Jaza form hiyo (inajieleza yenyewe). Kurudisha form wanahitaji viambatanisho vifuatavyo.
1) Kopi ya passport inayoisha (ukurasa ulio na picha yako).
2) Kopi ya kitambulisho ( Kazi, Mpiga kura au Taifa).
3) Picha passport size ( 6)
4) Barua ya Mwajiri (if any)
5) Kopi ya cheti cha kuzaliwa
6) Pesa Tshs 50,000.
Nadhani ndivyo vitu vinavyohitajika mkuu
Asante sana mkuu
 
Na kwa anayehitaji passport mpya inakiwaje! Kuna dogo kaenda kuulizia leo, ameambiwa mpaka apate barua ya mualiko kutoka nje ya nchi
Alternative ya hiyo barua n nn?
Wasimubabaishe bwana.
Passport ni haki ya raia yoyote siyo mpaka awe anasafiri.
Mwambie kama kaunta wanambabaisha anone na Mkubwa wao.
Awaeleze kuwa haitaji kusafiri kwa leo wala kesho ila ana omba apate haki ya kuwa na passport kama raia yoyote.
Atakacho takiwa kuthibitisha kama muombaji mpya ni Barua kutoka Kwa mwenyekiti wa serikali za mtaa + nilivyoorodhesha kwenye post ya SMU. Yawezekana kakutana na wrong person
 
Mkuu mimi niliacha mchakato wa kutafuta passport hivi hivi baada ya kurudishwa mara kadhaa eti lazima niwe na barua ya nje ya mwaliko ndio nitapata passport.
 
Siyo sahihi kabisa. Shida iliyopo kwenye taasisi zetu ni kwamba kuna watu wanafanya kazi tu hawajuhi malengo na madhumuni ya taasisi husika. Huyo aliyekwambia hivyo ungemuuliza swali moja tu mkuu. Kuwa ina maana kama mtu hawezi kusafiri kwenda nje ya nchi haruhusiwi kumilki passport? Passport ni document ya serikali kama kitambulisho cha Urahia ndiyo maana document hiyo hutumika si tu kwa kusafiria bali hata mambo mengine kama kitambulisho. Mfano Ukitaka kukopa pesa benki kama si mfanyakazi moja ya vitu utakavyoambiwa kutoa ili kukutambulisha ni passport. Rudi tena, kuchukuwa form, na ukirudisha pale counter wakikubabaisha omba kuonana na mkubwa wao. Atakuelewa mkuu. Wakubwa wanajua. Jieleze tu vizuri bila jazba. Naamini atakuelewa
 
Mkuu nasikia wameishiwa vitabu hawana fungu la kuprint.... Mgao haujaemda kule bado... hizo ni nyepesi nyepesi za pale....

Tangu mwezi wa 8 mwaka jana wamekuwa na uhaba wa "vitabu" hivyo naona taratibu wanataka kurejesha mambo ya rushwa ambayo kwa kweli yalikuwa yamepungua sana hasa kama mtu anarenew na safari yake haina makandokando. Ila kwa sasa na mpaka juma lililopita kumeanza kuwa na shida...
 
Ni kweli uhamiaji wameishiwa vitabu. Sasa hivi passport ni za kusubiri mpk hapo vitabu vitakapofika.
 
Siyo sahihi kabisa. Shida iliyopo kwenye taasisi zetu ni kwamba kuna watu wanafanya kazi tu hawajuhi malengo na madhumuni ya taasisi husika. Huyo aliyekwambia hivyo ungemuuliza swali moja tu mkuu. Kuwa ina maana kama mtu hawezi kusafiri kwenda nje ya nchi haruhusiwi kumilki passport? Passport ni document ya serikali kama kitambulisho cha Urahia ndiyo maana document hiyo hutumika si tu kwa kusafiria bali hata mambo mengine kama kitambulisho. Mfano Ukitaka kukopa pesa benki kama si mfanyakazi moja ya vitu utakavyoambiwa kutoa ili kukutambulisha ni passport. Rudi tena, kuchukuwa form, na ukirudisha pale counter wakikubabaisha omba kuonana na mkubwa wao. Atakuelewa mkuu. Wakubwa wanajua. Jieleze tu vizuri bila jazba. Naamini atakuelewa

Mkuu ni kweli kabisa uhamiaji wamebadili utaratibu, ss hv kupata passport mpaka uwe na kithibitisho cha kuonyesha kwann unataka kuitumia hiyo passpor mfano: barua ya mwajiri kuonyesha kama una safari ya nje eidha kimasomo au kikazi, admission letter ya chuo unachoenda kusoma nje kama unaend ww binafsi na co kwa mgongo wa mwajiri, barua toka nje etc.
Yan wanasema hawez kutoa passport tu kwa kila mtu kama hawaoni wapi ataenda kuitumia wakati anaomba hiyo passport.
So anayosema mkuu MarianaTrench ni sahihi kabisa. Hii imentokea nikapeleka barua ya mwajiri kuwaambia kuwa nna safari ya nje.
 
Siyo sahihi kabisa. Shida iliyopo kwenye taasisi zetu ni kwamba kuna watu wanafanya kazi tu hawajuhi malengo na madhumuni ya taasisi husika. Huyo aliyekwambia hivyo ungemuuliza swali moja tu mkuu. Kuwa ina maana kama mtu hawezi kusafiri kwenda nje ya nchi haruhusiwi kumilki passport? Passport ni document ya serikali kama kitambulisho cha Urahia ndiyo maana document hiyo hutumika si tu kwa kusafiria bali hata mambo mengine kama kitambulisho. Mfano Ukitaka kukopa pesa benki kama si mfanyakazi moja ya vitu utakavyoambiwa kutoa ili kukutambulisha ni passport. Rudi tena, kuchukuwa form, na ukirudisha pale counter wakikubabaisha omba kuonana na mkubwa wao. Atakuelewa mkuu. Wakubwa wanajua. Jieleze tu vizuri bila jazba. Naamini atakuelewa
Passport ni hati ya kusafiria mkuu
 
Mchakato Wa kupata passport kwa sasa imekuwa rahisi sana hawana complications kama ulivyo kuwa miaka iliyopita
Kilichotokea kwa sasa wana uhaba Wa hivyo vitabu vya passport
Nasema hivyo kwani nipo kwenye foleni ya kusubiri passport za wanangu na tarehe niliyopangiwa ilipita na nilpoenda tena wamenieleza tatizo ni vitabu nisubiri
 
Duh,hapo kwnye passport acheni tu,nilipigwa ela mpaka basi,wakati ni sh 50000 tu cna hamu na passport tena
 
Back
Top Bottom