Hili la michango ya mwenge ni nchi nzima au?

Feeling Haillee

JF-Expert Member
Sep 27, 2016
205
97
Jamani huku kwetu kati Halmashauri yetu watumishi tumekua tukilazimishwa kuchangia michango kwa ajili ya MWENGE. Ninachouliza huu utaratibu ni wa nchi nzima au ni ubunifu tuu wa great thinkers wa Halmashauri yetu.

Nauliza tuu kwa nia njema.
 
Kuna sehemu zingine hawachangi Bali wanakesha tu na kunywa,kula na kucheza ,rhumba tu Hayo ni huko kwenu tu
 
Jamani huku kwetu kat Halmashauri yetu Watumishi tumekua tukilazimishwa kuchangia Michango kwa ajili ya MWENGE. Ninachouliza huu utaratibu ni wa nchi nzima au ni ubunifu tuu wa Great Thinkers wa Halmashauri yetu. Nauliza tuu kwa nia njema. Msinitafute.
Niliwahi kutoa UZI humu kumtaka Magufuli atoe tamko kuhusu michango hiyo.
Ukweli ni kwamba, jambo hilo LINAKERA sana hasa katika kipindi hiki cha vyama vingi.
Ni makosa KISHERIA KUMLAZIMISHA mtumishi yeyote KUCHANGIA Mwenge wakati CCM ina bajeti yake yenyewe Hili ni lazima liangaliwe upya katika siasa ZILIZOBADILIKA.
Maana tunaenda na wakati.
 
Yaan ni heri atoe tamko ili tuwe na Amani. Watu tunatoa huku tukiwa tunanung'unika. Haipendezi.
 
Wanaochanga ni kutoka serikali za mitaa chini ya mkurugenzi ila wa serikal kuu hawachangi
 
Mwaka jana walinilia 5000 yangu kizembe sana.Tunajitoa kuchangia wakati maslahi yetu kazini yanakanyagwa. Vitisho tu! Ooh usipotoa sahau kupanda daraja.Tumetoa hatupandishwi madaraja.Huu ni utapeli tu wa fedha zetu.
 
Back
Top Bottom