Hili la bosi Emili wa TANAPA lataka uchunguzi wa kina!!

accused

JF-Expert Member
Aug 7, 2015
2,496
2,743
Wadau.
Kuna taarifa za jeshi la polisi Arusha la kumhusisha swalehe ambae ni mfanyakazi wa ndani wa Emil katika mauaji ya bosi wake, Swalehe according to police ana miaka 20 tu, na alikua houseboy. Wasi wasi wangu ni huu hapa, kama Swalehe alikua houseboy je ni kweli kutokana na maisha yake duni hadi kua houseboy na pia kwa umri wake ni kweli kua swalehe anaeza endesha gari ??

Na je, swalehe ni mgeni sana wa kuona pesa kiasi cha 5m ndan ya nyumba ya boss wake? Na je hata kwanini hatufikirii kua swalehe angeeza fanya means nyingne ya kubeba zile pesa bila kuua ukizingatia kua maamuzi ya kutoa uhai wa mtu si rahisi.

Sibishani wala sipingani na upelelezi wa awali wa police, ila kwa kuzingatia cheo alichokua nacho bwana Emil, na wakati tulionao wa utumbuaji majipu wa mh JPM, naliomba jeshi la police kufuatulia kwa kina zaidi ili kujua ukweli wa kifo cha Emil.

Ni mtizamo wangu tu!!!
 
Hiyo ya Househelp ni sababu cheap sana... Sipingi lakini siiamini hivi.

Na Story yenyewe ilikuwa straight sana. Towels wanazosema alitumia eti wala hakutupa alihifadhi.

Househelp ni Story tu. #JumbaBovu
 
Aisee ni Shida na mkewe anahojiwa,mtoto wa Miaka 20 kuwa na guts za Kuua askari??????? maswali mengi kuliko majibu.
 
Usalama wa Taifa wamefanya yao, baada ya kupewa maagizo kutoka kwa Wakuu, kuwa huyu Emil ni tatizo pia, anaihujumu nchi kwa kufanikisha ujangili nchini...! Ni kama ile ishu ya masamaki lakini yeye kauwawa lakini masamaki yupo mahakamani...!
 
Polisi arusha ni tatizo sana ! Hivi kwanini rpc wa arusha wanaakaa vituoni kwao muda mrefu kama Dsm Kanda maalum ?? Ukiacha ACP andengenye wengine walikaa zaidi ya miaka saba kituo kimoja na wanakua na intelegencia ya kutunga kama sele makengeza.................
Nasikia polisi wa arusha wana guatanamo yao unaingizwa spoku ya baiskeli kwenye uume eti wanakulazimisha ukiri makosa............
Hebu wafanye kazi kwa ueledi sio kuwa na makando kando na kutokuhaminika kwa wananchi.
Japo tunaona mabadiliko kidogo siku za hivi karibuni
 
Wadau.
Kuna taarifa za jeshi la polisi Arusha la kumhusisha swalehe ambae ni mfanyakazi wa ndani wa Emil katika mauaji ya bosi wake, Swalehe according to police ana miaka 20 tu, na alikua houseboy. Wasi wasi wangu ni huu hapa, kama Swalehe alikua houseboy je ni kweli kutokana na maisha yake duni hadi kua houseboy na pia kwa umri wake ni kweli kua swalehe anaeza endesha gari ??

Na je, swalehe ni mgeni sana wa kuona pesa kiasi cha 5m ndan ya nyumba ya boss wake? Na je hata kwanini hatufikirii kua swalehe angeeza fanya means nyingne ya kubeba zile pesa bila kuua ukizingatia kua maamuzi ya kutoa uhai wa mtu si rahisi.

Sibishani wala sipingani na upelelezi wa awali wa police, ila kwa kuzingatia cheo alichokua nacho bwana Emil, na wakati tulionao wa utumbuaji majipu wa mh JPM, naliomba jeshi la police kufuatulia kwa kina zaidi ili kujua ukweli wa kifo cha Emil.

Ni mtizamo wangu tu!!!

Uko Sahihi Kabisa Mkuu!! Hata Mi Nina Maswali Lukuki Juu Ya Kifo Au MAUAJI Ya "KACHERO " Huyo!!! MASHAKA Ni Mengi Mno, Je, Kama CHANZO Cha Mauaji Hayo Ni Muuaji Kutamani Kiasi Hicho Cha PESA!! Je, Kulikuwa Na ULAZIMA Wa KUFANYA MAUAJI Hayo!! Alishindwa Kuziiba Kwa Njia Nyingine!!!??? Na Je, Huyo KIJANA Alihitaji Hizo Mil 5 Tu,?? Kama SHIDA Yake Ilikuwa Ni KUPATA Pesa, Mbona Aliziacha Ndani Ya Boot Na Simu Nyingine Aliziacha Pia!!! Je, KWANINI Polisi Walilikokota Tu Gari Hilo Hadi Kituoni Na Kulipaki Bila Ya Kulifanyia Upekuzi Wa Kina!!! Hadi Pale Mke Wa MAREHEMU Alipoenda Kituoni KUTOA Taarifa Ya KUPOTEA Kwa Mumewe Kwa Kutoonekana Na Simu Zake Zoote Hazipatikani Kwa Kutwa NZIMA!!!?? Je, Mke Huyo Wa MAREHEMU Kwa Muda Huo MAUAJI Hayo Yakitokea!!??? Na Ni Kweli Aliyeendesha Hilo Gari Kutoka Nyumbani Hadi Lilipokutwa Ni Huyo KIJANA!!!?? Na Kama Ni Yeye Mbona Hizo FUNGUO Alizozitumia Hazijasemwa Kama Alikutwa Nazo Au Amezitupa!!!?? Maana Tumesikia Mke Wa MAREHEMU Ndiye Aliyepeleka Funguo Kituoni, Ambazo POLISI Wamesema Ni Za Akiba!! Je Zile Nyingine Ziko Wapi!!!?? Na KWANINI Huyo KIJANA Hakuweza Kutoroka Mara Baada Ya KUFANIKISHA Mpango Wake!!!? Hadi Aje Kukamatwa Na VITU HIVYO Amevihifadhi Ndani Ya Banda La KUKU!!!!?? Alijiamini Kwa Lipi Hasa!!!??? Je, Ni Kweli Ana UWEZO Wa Kuendesha Gari Kwa KIWANGO HICHO!!!!?? NADHANI Kuna Maswali Na Mashaka Mengi Mno!!!! JESHI La POLISI LIENDE Deep Zaidi!!! Mazingira Ya MAUAJI Hayo Yamegubikwa Na UTATA NA MASHAKA MNO!!!! KIJANA Huyo Ana "SIRI KUBWA MNO " Nadhani Kama MWISHO Wa Upelelezi Na Uchunguzi Wa Kina, UKWELI UTAJIDHARIRISHA!!!!!
 
Polisi Tanzania wajitahidi kwenda na dunia inavyozunguka.Kuna vitu haviendi sawa.Umuhimu wa wapelelezi binafsi uonekane sasa.
 
Polisi Tanzania wajitahidi kwenda na dunia inavyozunguka.Kuna vitu haviendi sawa.Umuhimu wa wapelelezi binafsi uonekane sasa.

na hilo likiruhusiwa hapa bongo basi itakuwa aibu tupu aisee.
hata wapelelezi wetu wa ndani wanaweza sana tatizo wanafanya kazi kwa maelekezo toka ngazi za juu.

hata usalama nao wanafanya kazi kwa maelezo kutoka juu
 
Upelelezi upo katika kiwango cha chini sana kwa hawa polisi wetu sijui shida ni nini..nakumbuka ulipolipuliwa ubalozi wa USA dar na Nairobi walikamatwa watu zaidi ya 200 mafundi wengi..walipokuja wapelelezi wa ukweli walisema toa hao hakuna hata mmoja hapo wao walimkamata mmoja Capetown yule dogo Mzanzibar na mwningine Pakistani..hapa kwetu wanajua matukio yakitokea muuaji hawezi toka mbali kama vile tuko katika enzi za Ujima..Fungukeni bwana nendeni na Dunia inavyobadilika mnaagiza magari meengi ya kusomba wanywa viroba mnashindwa kuwa hata na maabara ya kutunza Finger Prints kwa washukiwa mnaowatafuta kama wakifanya tukio mnachukua Prints alizoacha na kutunza tuu pindi mkimkamata ni kulinganisha tuu na si ivi mnavyofanya kazi..
 
Usalama wa Taifa wamefanya yao, baada ya kupewa maagizo kutoka kwa Wakuu, kuwa huyu Emil ni tatizo pia, anaihujumu nchi kwa kufanikisha ujangili nchini...! Ni kama ile ishu ya masamaki lakini yeye kauwawa lakini masamaki yupo mahakamani...!

Weka akuba ndugu
 
Wamedai Swalehe amekiri. Kama siyo yeye, bila shaka anajua aliyefanya mauaji hayo.

Amekiri au amekirishwa! Inawezekanaje mke wa marehemu akatoe taarifa ya kupotelew na mme wakati anajua ameenda kazini? Je ni mara ya kwanza kwa narehemu kwenda kazn na kuchelewa au nini hasa mkewe alichoshakia? Inawezekana yule msaidizi akafanya mauaji ndani na mke asione hata harakati za kudeki mle ndani na nguo zifichwe kwenye kibanda cha mifugo asione?

Kwanza tujue nini kilimfanya mke atoe taarifa ya kwamba mme amepotea tena kwa siku moja hali marehemu akiwa mtu wa intelijensia na shughuli zake kuondoka nyumba ghagla ni swala la kawaida!!! Huyo kijana ni chambo tu,Inawezekana mkewe anahusika 89% kwa kushawishiwa na nguvu kubwa na yeye akamtumia huyo kijana.

Yaani amuue akitafuta pesa halafu aiache pesa kwenye buti!
 
Huyu afisa alikuwa na informations zote kuhusu majangili papa ndio maana wamemuua.
Haiingii akilini hata kidogo eti houseboy wa miaka 20 kumuua askari kizembe alafu eti alizihitaji milioni tano za boss wake!
Kuna issue ipo behind the scenes na itabumbuluka tu.
 
Hivi Tanzania tuna Forensic detectives kama kwa wenzetu? Au tuazime kwa waliobobea naamini hofu ya mtoa mada itapata jibu..
 
Katika era hizi za utumbuaji majipu ambayo Tanapa nayo ni jipu tambazi linalosubiri kutumbuliwa juu ya Tembo na wanyama wetu, posho za juu za vikao,hati zisizoelezeka za mahesabu, Arusha ni mkoa wenye watu wa deal nyingi za porini. Marehemu anakuwa ni person of interests ikizingatiwa naye alikuwa ni Askari mkuu wa usalama Tanapa.
Technically, mke wa marehemu itabidi awe msaidizi mkubwa wa polisi. Houseboy naye ataisaidia sana jamhuri, Dna na other forensic tech zinahitajika hapo
 
Back
Top Bottom