Hili bunge ni aibu tupu

Hili bunge ni aibu tupu

Naamini Job Ndugai ni mdau hapa JF au ana mtu wake wa karibu anasoma michango hapa na kumpa notes! Mara nyingi anaonekana kufanya maamuzi huko bungeni baada ya mijadala hapa. Ni jambo zuri.

Hata hivyo bunge sasa linatakiwa kipitie tena kanuni zake na kuamua ni wakati gani msiba unagusa bunge au la? Ni pia bunge litoa mwongozo kuhusu ushiriki wa serikali kwenye misiba. Inakuwaje waziri na naibu wake wapige kambi kwenye msiba mmoja huku wizara haina mtu? Ni vigezo gani vinatumiwa na serikali kutoa rambirambi kupitia kodi ya wananchi?

Lakini la muhimu, bunge lijadili kuhusu eneo la kuzika watu mashuhuri. Lazima kuwepo na eneo maalum kwa watu ambao ni wa kitaifa.

Mkuu wakati nakubalina na wewe kuhusu mengine, nadhani hatustahili kuendelea kuzika kwenye makaburi. Tunatakiwa kuanza kuchoma miili na kuhifadhi majivu tu!
 
Walisimama kifo cha michael jackson,wiki iliofuata akafa NASMA Hamisi Kidogo(muimba taarabu)Hawakusimama kumkumbuka,lakini kaikuza taarab Bongo
 
Kuna maandamano makubwa tulishayaratibu zamani kwa ajili ya kutetea maaskari polisi na JWTZ. Ingawa awali halikuwapo, hili nalo sasa litaingizwa kwenye mabango: haiwezekani IGP wa Polisi na Jenerali wa JWTZ waonekane hawana mchango kwa taifa. Tunahitaji uungwaji mkono kutoka majeshi yote nchini, kwani ajenda za awali zilikuwa ni maslahi ya askari wetu

Ninakubaliana nawe kwa mengi uliyoyaeleza hapa isipokuwa katika hill: si kila IGP au General wa jeshi anakuwa na mchango kwa taifa -japo Mahundi na Kyaro wanastahili heshima. Watu kama Mahita na Shimbo (aliejipa majukumu ya kuwapigia magamba debe) wanastahili adhabu na si heshima!
 
Back
Top Bottom