Ukiongea kingereza na Mtanzania mwenzako kiukweli ni tabu sana maana anataka kuonyesha anajua na kukukosoa kila unapokosea na kukucheka. Nimefanya kazi na Wazungu hasa Waingereza hawana muda wa kukukosoa lakini utajifunza tu kutoka kwao kama unaakili ya kufikiria kwasababu ulichokosea baadae yeye anaweza kuongea na ukajua kumbe mimi nilikosea. Jamani watanzania tunajifunza kiingereza kama lugha ya kigeni na siyo lugha ya kuzaliwa nayo. Kazi kubwa ya Lugha ni ili wazungumzaji waweze kuelewana na suala la ufasaha wa lugha ni lingine.