Drjacka92
JF-Expert Member
- Jul 20, 2016
- 445
- 522
Salaam wakuu!!.
Wengi wetu naamini saahizi tumepumzika baada ya pilikapilika za kutwa nzima.
Kuna mambo huwa tunayaongea kwa makosa Mara kwa Mara bila ya kujua kuwa tunakosea au tunajua tunakosea lakini tunaamua kurahisisha tuu ilimradi tunaelewana baasi.
Tumezoea kuviita vituo vyote vya mafuta ya Petrol, Diesel na Mafuta ya taa kwa jina la 'Shell' kitu ambacho sio sahihi kabisa, kwasababu kila kitu cha mafuta kina jina lake, kuna Oil com, Lake oil, Bp, na mengine tuu ambapo mmiliki wa kituo husika ameamua kukiita kituo chake.
Kwahiyo ni vyema na sahihi kusema nimetoka Oil com kuongeza mafuta kwenye gari na sio nimetoka Shell, kwakuwa Shell ni jina binafsi la kituo cha mafuta ambacho kimejizolea umaarufu kwakutoa huduma hiyo kwa muda mrefu na sehemu nyingi Ulimwenguni hivyo imeathiri watu wengi kudhani kuwa kila kituo cha mafuta kinaitwa Shell.
Kwa sasa sidhani kama Tanzania kuna kituo cha Mafuta cha kampuni ya Shell japo huko awali kilikuwepo.
Nikushukuru kwakusoma nakama ulikuwa haufahamu umeweza kufahamu sasa, elekeza na wengine waelewe hii kitu.
Ahsante!.