Hijabu Yazua Kasheshe Uarabuni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hijabu Yazua Kasheshe Uarabuni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Feb 11, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  Thursday, February 11, 2010 2:32 AM

  Balozi mmoja wa nchi za kiarabu amempa talaka mkewe mpya muda mfupi baada ya kuoana naye baada ya kuiona sura yake kwa mara ya kwanza baada ya hijabu kufunuliwa na kugundua kuwa mkewe huyo mpya ana makengeza na ana vinyweleo usoni. Balozi mmoja katika nchi za kiarabu jina kapuni alizivunja sherehe za harusi baada ya kuiona sura ya mkewe kwa mara ya kwanza muda mfupi baada ya kufunga naye ndoa na kugundua ana makengeza na vinyweleo kwenye kidevu chake (ndevu za wanawake).

  Kwa mujibu wa gazeti la Gulf News balozi huyo alikuwa akikutana na mwanamke huyo mara chache sana kabla ya siku ya harusi na wakati wote mwanamke huyo alikuwa akiufunika uso wake kwa Niqab (Vazi linalofunika uso na kuacha macho pekee wazi).

  Baada ya ndoa kufungishwa balozi huyo alitaka kumbusu mkewe na ndipo alipofanikiwa kuiona sura yake kwa mara ya kwanza na kugundua ana vinyweleo kwenye kidevu na ana macho yenye makengeza.

  Balozi huyo alikata shauri la kuivunja ndoa hiyo kwenye mahakama ya sharia za kiislamu katika falme za kiarabu akisema kuwa aliingizwa mkenge wa ndoa na mama wa mwanamke huyo baada ya kuonyeshwa picha za dada yake badala ya zake.

  Balozi huyo alitaka ndoa hiyo ivunjwe na pia alimtaka mwanamke huyo amlipe fidia ya dirham 500,000 kwa mikufu, nguo na zawadi zingine alizomnunulia.

  Mahakama ilikubali kuivunja ndoa hiyo lakini ilitupilia mbali madai ya fidia ya balozi huyo.

  Taarifa iliyotolewa haikutaja jina la balozi huyo na wala haikutoa maelezo zaidi kuhusiana na sakata hilo.


  Chanzo: nifahamishe.com
   
 2. Katoma

  Katoma Senior Member

  #2
  Feb 11, 2010
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo jamaa hakuona macho yenye makengeza wakati huyo mchumba amevaa niqab?
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  KKKKKaaaz kweikwei
   
 4. B

  Bull JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Peleka kwenye udaku, mod pls
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Feb 12, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Madhara ya kuuziana mbuzi kwene gunia haya :D
   
 6. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  DuH!

  Nilikuwa cijui; hata wachumba hawaonani sura?
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Ooo wewe bana umechelewa sana aisee

  . Kuna kadhia moja ilitokea huko Persia miaka ya majukati hapa, baada ya mume mmoja kumvizia mkewe akiwa amelala na kutaka kumvua mtandio il aone kuona kunani chini ya paa, mambo kama kuna upaa au nywele kaa za jinn.. Mama akastuka bana ilikuwa kesi kubwa sana, na nadhani talaka ilidaiwa. :D

  Mind you hii couple ilikuwa ndoani ova 20 years, lakini mume hajui kichwa cha mkewe kikoje (??)!
   
 8. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #8
  Feb 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,210
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mbuzi kwenye kiroba? Kaazi kweli kweli!
   
 9. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #9
  Feb 12, 2010
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,161
  Likes Received: 923
  Trophy Points: 280
  Hizo ndizo faida ni NAQAB. Faida hizo ndizo zinazosabisha Wafaransa, Wamarekani na Waingereza wazipige marufuku ktk baadhi ya maeneo
   
 10. b

  bnhai JF-Expert Member

  #10
  Feb 12, 2010
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,234
  Likes Received: 1,385
  Trophy Points: 280
  Hii habari imekaa kiudaku zaidi. Hivi mtu anayevaa NIQABU haonekani macho? Km alikuwa anaonana naye hakugundua macho yako vipi? Naamini pia sheria inauhusu mtu kumuona mtarajiwa wake kabla ya ndoa, hapo ilikuwaje? Habari km hii haiwezi hata kutaja eneo husika zaidi ya kutaja nchi maana imejaa walakini.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...