Hii ya Raila Odinga nimeipenda, ina ukweli humu JF!

Gagurito

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
5,600
803
Juzi nikiwa nimetulia nyumban sebureni huku nikitaza tv kwa lengo la kujiburudisha, dogo akaweka Citizen tv ya kenya, kwa wale wapenz wa project fame kwenu si tatizo kuitambua, pindi nashangaa mara ikaonyesha kipante cha mh. Waziri mkuu wa nchi hiyo ktk moja ya Hotuba zake za hivi karibuni alizofanya kwao na Mh.Kilonzo msyoka huko ukambani akinena kwamba "KUNA WAZEE WENYE AKILI ZA KITOTO PIA KUNA VIJANA WENYE AKILI NA FIKRA ZA KIZEE PIA"

Ilinichukua muda nikitafakari kwa kina maneno hayo, lakini kwa kupitia comments nyingi humu Jf nimepata lithibisha hilo, KUNA WATU HUMU TENA VIJANA WENZETU WANAMAWAZO YA KIZEE, hii inanipelekea kuamini kuwa hayo wameyarithi toka kwa WAZEE WAO WENYE AKILI ZA KITOTO" Kumeibuka kundi la watu humu pindi wengine tukijadili mwenendo wa kisiasa nchini, tukipeana modalities juu ya nini kifanyike kwa kuinusuru Tanzania yetu toka mikononi mwa mafisadi na kupe wanyonyezi wa watanzania wao ndio kwanza wanashabikia matendo ya kifisadi, wanaleta story na hoja za kipumbavu, wanacoments kijinga na kutoa matusi instead of points.

Kwa mwenendo wao nadhan ni stahili kuwaita hawa kwa jina la VIFISADI VITOTO, ambayo mpaka muda huu vinakaa na kujadili ni jinsi gan maandamano yao ya trh 16 march yatafana. Hawa ni watu wa ajabu sana inapaswa kuwakwepa sana, inapobidi kuwakosa kwa matendo yao, realy Raila Odinga alikuwa sawa kusema kuwa kuna watu wa ajabu, haswa pale vijana wanapokua na akili za kizee zitokanazo na wazee wao kuwa na Akili za kitoto.

Ndugu wanaJF nawasilisha hoja!
 
Raila kichwa ila naye ana kazi sana maana mafisadi wa kenya hamtaki wanaaamini akichukua madaraka watakiona cha moto, uwa napata tabu sana wakumringanisha naye hapa kwetu! maan UWT wanavuruga sana siasa za Tanzania
 
Leading the list are the following:
.....
kupenge
jeikei
muhogomchungu
mjepu
thinktwice
mkmap
mwera
mahesabu
zemarcopolo
kashaga

nk. nk nk !!
 
bwana GAGURITO, kwanza nikupongeze kwa thread nzuri ila iliyotiwa kasoro kidogo na makosa ya kimaandishi badala ya sebule ukasema sebure na badala ya kipande ukasema kipante ila overall mada ni nzuri. Nainze kwa kusema ya kwamba kumbuka unapaswa kuheshimu maamuzi na fikra za mtu mmoja mmoja, ktk dunia ya leo kila mmoja anacho anachokiamini na kukipenda ambacho kila mmoja hujiona yuko sahihi kuliko mwingine. Wakati we unaamini kile kinachofanywa na hao unaowaita mafisadi ni makosa kuna mwingine ana muono tofauti kuhusu hilo, kinachopaswa ni kumfundisha kwa hoja madhubuti ili na yeye aamini katika hayo mabadiliko unayoyahubiri. Sio lazima ufanye mabadiliko ukiwa chama fulani cha siasa bali ni kwa kuwa na msimamo thabiti, fikra moyoni na ujasiri wa kufanya hayo mabadiliko.MABADILIKO YA KWELI HAYALETWI NA CHAMA bali wananchi walio tayari kufanya mabadiliko.
 
Naheshimu sana mawazo yao bt the way wanavyowakilisha yatia mashaka, abt typing error think next tym nitakuwa makini, that tym nilikuwa fasta!
 
Umenena vyema kabisa ila kwa humu jf unawezaje kuwatambua vitoto na vijitu vizima?
Inawezekana hivyo tunavyoviona vitoto ni vizee vyenye akili za kitoto.
 
watoto wa mafisadi hebu comment na nyie kidogo! Mawazo yenu ni mhm!
 
Raila kichwa ila naye ana kazi sana maana mafisadi wa kenya hamtaki wanaaamini akichukua madaraka watakiona cha moto, uwa napata tabu sana wakumringanisha naye hapa kwetu! maan UWT wanavuruga sana siasa za Tanzania
<br />

Lakini Raila sio mwenzetu,ni mtu mwenye na pesa mingi na tajiri pia,sasa ni ngumu kujua zipi za urithi na zipi ni mali yake na uhalali wa ndururu/chapaa hizo.Pengine anaweza kuwa fuswadi huyu shemeji yake Najib Balala.
 
bwana GAGURITO, kwanza nikupongeze kwa thread nzuri ila iliyotiwa kasoro kidogo na makosa ya kimaandishi badala ya sebule ukasema sebure na badala ya kipande ukasema kipante ila overall mada ni nzuri. Nainze kwa kusema ya kwamba kumbuka unapaswa kuheshimu maamuzi na fikra za mtu mmoja mmoja, ktk dunia ya leo kila mmoja anacho anachokiamini na kukipenda ambacho kila mmoja hujiona yuko sahihi kuliko mwingine. Wakati we unaamini kile kinachofanywa na hao unaowaita mafisadi ni makosa kuna mwingine ana muono tofauti kuhusu hilo, kinachopaswa ni kumfundisha kwa hoja madhubuti ili na yeye aamini katika hayo mabadiliko unayoyahubiri. Sio lazima ufanye mabadiliko ukiwa chama fulani cha siasa bali ni kwa kuwa na msimamo thabiti, fikra moyoni na ujasiri wa kufanya hayo mabadiliko.MABADILIKO YA KWELI HAYALETWI NA CHAMA bali
wananchi walio tayari kufanya mabadiliko.
Hawa hawafundishiki, kwani wanajua fika ukweli umelalia wapi, ila kama Railla alivyosema ni vijana wenye akili za kizee na wazee wenye akili za kitoto, Labda dawa ni kuwapuuza tu, mtu ukishagundua ana matope kichwani ni upuuzi kumfundisha!
 
Kuheshimu fikra za watu ni jambo zuri,lakini kuna fikra zinakuwa potofu moja kwa moja kwa kipimo chochote kile ama kwa kukosa mantiki au uwongo au upotoshaji wa dhahiri
eg mmiliki wa dowans simjui,sijawahi kukutana naye........,baada ya siku kadhaa unayemkana anafika nyumbani kwako
 
<br />

Lakini Raila sio mwenzetu,ni mtu mwenye na pesa mingi na tajiri pia,sasa ni ngumu kujua zipi za urithi na zipi ni mali yake na uhalali wa ndururu/chapaa hizo.Pengine anaweza kuwa fuswadi huyu shemeji yake Najib Balala.

Hivi balala ni shemeji yake?!
 
wanaboa sana hawa watu ndugu zangu, imagine kijana mwenzako stil anang'ang'ania hoja ya amani, utulivu wkt maendeleo kwa nananchi ni duni. Aaah! Wanaboa sana!
 
Back
Top Bottom