Hii ya chagua mtu badala ya chama imekaaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ya chagua mtu badala ya chama imekaaje?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by minda, Oct 18, 2010.

 1. minda

  minda JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  wakuu, hii ya chagua mtu badala ya chama umekaaje?
  mwanzoni ilianza kama jambo lisilo serious sana, lakini mpaka sasa tunaambiwa (mwananchi) hata viongozi wa dini wanasisitiza sana kwa mtu kuchaguliwa kwa kigezo cha ubora na si chama(malasusa).

  rioba alipata kusema kwamba ccm ikiweka hata ng'ombe atachaguliwa tu; lakini sasa inavyoonekana upepo umeanza kugeuza mwelekeo.

  hivi maana yake inaweza kuwa nini wakuu?
   
 2. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Simpo! Kwamba tuchague kiongozi ambaye tuna imani kuwa atatuletea maendeleo,, kwa kuzingatia utendaji wake/ sera zake.
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Watu wamechoka na ccm kuteuwa vilaza na wanachi wakawachagua! sasa tunachagua akili ya mtu na si chama chake!
  Tunataka maendeleo na chama hakiwezi kuleta maendeleo ila wanachama (WATU) VILAZA HATUTAKI!
   
 4. Joel

  Joel JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2010
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 908
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 80
  wanaposema chagua mtu na si chama maana yake ni kwamba chama kinaweza kuwa na katiba na sera nzuri sana na historia nzuri, lakini wle viongozi au wanachama wa hicho chama wasiwe na sifa za kuwa viongozi. Ila unapochagua mtu tayari unakuwa na uwezo wa kumbana yeye binafsi (individual) badala ya chama ambcho hata kikiboronga huwezi kukibana au kukiwajibisha hasa kwa mfumo wetu wa tanzania (chama ni taasisi sio mtu individual) mfano cccm tangu imeanzishwa mpaka leo imeboronga sana sasa kuiwajibisha ccm si rahisi kama kumuwajibisha mtu mmoja mmoja.
   
 5. B

  BabaEliza New Member

  #5
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chama ni kama SETI-Baadhi ya members ndani ya seti ndo wamekwama.Kwa sasa tuangalie nini mahitaji ya Taifa letu halafu tuchague mtu atakeyekuwa tayari kuyashughulikia.Tumeshaona nyufa kenye msingi wa nyumba yetu-tunahitahi fundi wa kweli kwa ajili ya kufanya ukarabati mkubwa! wanaojiita mafundi ni wengi sana -tunahitaji fundi mwenye sifa.
   
 6. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hatuchagui malaika ila tunachagua mtu ambaye atleast ana uwezo wa kututoa hapa tulipo kwenda mbele zaidi "kimaendeleo" na sio kutoka tulipo kwenda mbele zaidi "kiufisadi"
   
 7. m

  mapambano JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwenye siasa huwezi kutengenisha mtu na chama (itikadi, sera nk.) atleast for now...vinakwenda pamoja. Hawa viongozi wa kiroho wanalao jambo, tusikubali wajaribu kututenganisha. Mchanganyiko wa SIASA NA DINI ni sumu kali kwa mtazamo wangu..
   
 8. L

  Lorah JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2010
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Maana yake ni kubwa sana, watu wanatembea kwa kuhonga na kununua watu na wasanii wakuwashangilia tusipo pima uwezo wa mtu twaweza kujikuta tumechagua kelele na kina joti kutuongozea nchi, Tusijali amekuja na ndege ngapi na Bongo flava ngapi Kikwete tunamjua kwa 5 years pamoja na wabunge wengine, Tukubali kubadilika, sasa hivi tunashindwa kutenganisha serikali na chama cha kisiasa, kwani kuna mazoea flani, hata Mkuu wa Police anashindwa kujitofautisha na Chama, Tukianza kuchagua mtu tutajikuta hata viongozi mafisadi wanabadilika kuwa watu wazuei cause wanajua chama hata kitoe vitenge na wax ngapi hakiwezi kumsaidia kupita kama hatatumikia wananchi....

  Hata kama unapenda Chdema namna gani, Hata kama unapenda CCM au CAF kwa kiwango gani kama mtu ni mbovu mpotezee....
  Huu nimuda wa kuwatumia Viongozi wa kiroho watumie uteule wao kuongea na mtu na kuwafunulia watu ni nani atakae tufaa.. Nashangaa tunawaondoa kwenye uso wa siasa while ni watu muhimu kweli...

  Mwakembe kama alifanya vizuri na watu wa jimboni mwake wamerizika bali hwariziki na maamuzi ya Kikwete wampe TIKI Mwakembe na TIKI rais wanaeamini kuwa ataweza kushirikiana na Kikwete....

  Nashangaa kwanini tunalaumu Kikwete kumpigia kampeni Lowasa na Chenge ni kwasababu tumeacha kufuata maadili ya mtu tunaendekeza uanachama, CCM imeporomoka kima adili kwa sababu ya uanachama, kuna watu ndani ya CCM wanamchukia Kikwete vibaya Mno ila wako kwenye msafara wake kumpigia kampeni sio kwa sababu ya kupenda kwa sababu ya uchamaaa

  Bora kikwete anaenda Kifamilia zaidi, angalia ubora wa familia yake kama vipi chagua yeye
   
 9. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hii ni mwiba kwa CCM!
   
 10. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  kwa tafsiri yangu nimemuelewa mchungaji kuwa sasa tuchague watu na sio sera za chama! Hivyo sasa kama mgombea udiwani wa Chadema unamuamini mpe kura yako, kama mbunge unaemuani ni kutoka CUF basi mpe kura yako na kama rais unaemuamini ni kutoka CCM basi mpe kura yako na hii nadhani ni nadharia nzuri ya mtu kuwa neutral na huenda tukawa na bunge imara lenyesura tofauti za kichama!
   
 11. minda

  minda JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  lakini ikumbukwe kwamba mwalimu alipata kusisitiza ili tuendelee tunahitaji vitu vinne;

  sasa hii haimaanishi kwamba katika uchaguzi 2010 tuchague mtu na chama ili kukata mzizi wa fitina?
   
 12. K

  Kikwebo JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2010
  Joined: Aug 25, 2006
  Messages: 352
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hii mbona ni very sipmle.... Ililokusudiwa hapa ni moja tu. Chagua mtu wa DINI yako hata kama yuko chama gani! Mwaka huu natabiri kutokea yale ambayo watu wengi wamekuwa ni waoga kuyatamka.

  Hii lazima itatokea..ikiwa Slaa na Kikwete wakishika nafasi mbili za juu na bad enough mmoja wao asifipate 50% ya kura, katiba inasema kama uchaguzi urudiwe.

  Hali ikifika hapa, na naomba Mungu atuepushie... tutaona the unthinkable...Kampeni zitaanza kupigwa Kanisani na Miskitini kavu kavu.
  Huu ni mwisho mmbaya mno na nimatunda ya kubaguana. Nidhambi ambayo itatutafuna sote. Jamani jamani, choonde chonde na mustakbali wa taifa letu hili. Kwenye nyumba zenu za ibada tafakarini hali hii.

  Naamini watu wa Idara ya Usalama wa Taifa hili wanachangamoto kubwa hapa, of course for National Intrest hata kuridhia kupindisha sheria ruksa. Nchi haiwezi kufikia hatua ya kuchinjana raia kutokonana na ubinafsi wa watu wachache wanaojifunika kwenye joho la UDINI.

  I am very shocked na trend hii ya Kampeni ya baadhi ya wagombea..yaani maeneo mengine is like wameya abandon kabisa na wameconcentrate kule kwenye wafuasi na mwelekeo mkubwa wa wapigakura wa dini ya mgombea. Then statement kama chagua mtu na sio chama zinafuatia.
   
Loading...