Hii ya Act wazalendo na Cuf Zanzibar inanikumbusha muungano wa Tanu na ASP mwaka 1977 uliozaa chama imara CCM!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,963
141,963
Kiukweli kama vyama vya ACT wazalendo na ile Cuf ya Zanzibar vitaamua kuunganisha nguvu ni dhahiri kitakachozaliwa kitakuwa chama chenye nguvu.

Na hii haitakuwa habari nzuri kwa CCM bali pia itakuwa ni habari mbaya kwa Chadema.
Ikumbukwe ifikapo 2020 sehemu pekee itayoweza kutoa wabunge wa upinzani ni Pemba na ndio maana Chadema walikuwa wanamuwinda maalimu Seif kwa udi na uvumba.

Kwa historia za Kigoma na Pemba zenye ufanano fulani wa kutokubali kuonewa ni wazi kabisa Yajayo yanafurahisha.

Maendeleo hayana vyama!
 
Ha ha ha! Mlishindwa mkiwa na nguvu ya vyama vyote "UKAWA" leo unasema midoli ya vyama eti itikise Chama Cha Mungu/Mapinduzi?

Utoto hautawaisha!
 
Back
Top Bottom