Hii tabia ya kuwatenga Watoto wa nje ya ndoa ni mbaya sana, ni kutengeneza sumu kwa watoto

Mimi ni muhanga wa jambo hili. Asikwambie mtu hili suala la kutengwa lipo tu hata mkiunganishwa. Haiwezekani ikatokea mkaishi kama vile watoto wa mama na baba mmoja.

Yeah at least watambue uwepo wako
 
Nakumbuka nilipopelekwa nyumbani kwa baba mzazi (nilizaliwa nje ya ndoa) mama yangu mlezi niliyemkuta alikuwa na watoto 11, wanane kati yao ni wakubwa kwangu nilifika nikiwa darasa la pili kiukweli mama yangu alinichukia sana tena kwa uwazi na mara nyingi baba alikuwa masafa.

Hivyo niligundua pale sina changu nikaamua kukaza msuli skuli, but b4 i go on with this story nataka niwajulishe nilifikaje kwa baba?
Ilikuwa hivi, nilipomaliza kidato cha 6 kuna mwl wangu wa la pili aliyekuwa akinipenda sana alikuwa zaidi ya mwl aliniita nyumbani kwake akanambia aliwahi muuliza baba kama alikuwa na mtoto nje ya ndoa (mwl alikuwa mchepuko wa mshua nilikuja jua baadae), baba akasema ndiyo tena unamfundisha darasani.

Ndipo mwl akamwambia baba lazima anihalalishe, anichukue, anitunze na kunilea nyumbani kwake bila hivyo asikanyage kwa mwl ndo baba akaja kunichukuwa ili ku secure hicho alichokuwa akikipata kutoka kwa mwl. Ukweli ni kwamba kwa mama nilikokuwa nikiishi hali ilikuwa mbaya sana kiuchumi hata viatu vya kwenda shuleilikuwa taabu sana kuvipata na kuna kila dalili kwamba nilikuwa si haba darasani.

Kilichomfanya mwl amuulize baba kama ana mtoto nje ni ufanano uliyopo kati ya mshua na mimi kwamba kila alipokuwa akiniona class alikuwa anamuona dingi na ni ukweli usiopingika. Maisha nyumbani yakaendelea hivyo hivyo kibabe hadi university hadi kupata ajira serikalini ingawa niliipiga chini baadae ili kupata nafasi ya kufanya mambo mengine.

Pamoja na yote hakuna hata mmoja aliyetoboa hata kwa kidogo ktk wale watoto 11 wa mama mlezi hakuna hata mwenye certificate ya welding na hata mishe zingine ziliwagomea na hivi ninavyoongea mama yangu alishatangulia mbele ya haki (RIP) lakini yule mama yangu mlezi anaishi kwangu namlea na kashindwa kukaa kwa wanawe, ukweli ni kwamba alinitesa sana ila sijawahi lala njaa wala sijawahi lala nje hivyo pamoja na mangufu yake naamini kuna sehemu ya mema aliyafanya kwangu kama mtoto wa mmewe na kama mwanawe hivyo yeye ni mama nitamlea ktk maisha yake yote hapa duniani kama sintotangulia kabla yake.

Tuwalee vizur watoto wa wenza wetu kwani kesho ndiyo yenye hofu nyingi kuliko leo.
 
Nakumbuka nilipopelekwa nyumbani kwa baba mzazi (nilizaliwa nje ya ndoa) mama yangu mlezi niliyemkuta alikuwa na watoto 11, wanane kati yao ni wakubwa kwangu nilifika nikiwa darasa la pili kiukweli mama yangu alinichukia sana tena kwa uwazi na mara nyingi baba alikuwa masafa.
Hongera sana Kaka kwa kutomfanyia roho mbaya mama mlezi.

Ila hawa akina mama jamani jamani mnh mnh mnh.

Watoto wote Mungu awajaalie wepesi waliopo kwenye such situations. Sio rahisi kabisa.
 
Mme wangu alikuwa na watoto wa nje ya ndoa wanne, wote nimewatambua, shida ikaja mtoto wa nje ya ndoa mmoja ni mkorofi anataka arithi kila kitu cha baba yake mwenyewe.

Imenitesa imenifikisha mahakamani. Sometimes hawa watoto wa nje ya ndoa wengine ni wasumbufu mno.
Wakiume ndio wasumbufu, ila wakike hawana shida
 
Ukitaka uvunje ndoa yako mapema na kuleta migogoro ndani isiyokuwa ya lazima, jaribu kutambulisha watoto wa nje. Cha kufanya, watoto wa nje wasaidie kule kule kwa mama yao bila nyumba kubwa kufahamu, ikiwezekana muwekee mradi wa kumkuza huko huko kwa mama yake.
 
Siku hizi wanaume kuzaa hovyo hovyo na kila sehemu ishakuwa kama fashion vile Ila hii kitu inaaribu psychology ya Watoto wa Nje ya ndoa Yani wanatengwa kwenye kila sehemu hawathaminiki kabisa wanaonekana kama watoto wa bahati mbaya as if waliomba wazaliwe nje ya ndoa
Kirahisi rahisi tu
 
Cha pili ni kuwaharibia wanawake kuolewa, mwanaume ana mke wa ndoa anaenda kuzaa nje na mwanamke mwingine halafu hamuoi, vijana wanaanza kumuogopa huyo binti anakaa kwao muda mrefu bila kuolewa kwa kuwa tayari ana mtoto
Hamna wanaume wanaowindwa na wanawake kama walioa, wana ujinga wao mmoja wanaamini "mume wa mtu anajua kucare......".Asilimia kubwa huwaga wanajitongozesha na wengine huenda mbali zaidi kutumia ndumba.
 
Cha pili ni kuwaharibia wanawake kuolewa, mwanaume ana mke wa ndoa anaenda kuzaa nje na mwanamke mwingine halafu hamuoi, vijana wanaanza kumuogopa huyo binti anakaa kwao muda mrefu bila kuolewa kwa kuwa tayari ana mtoto
Vijana wenzake hakuwaona sio. C wanasema mapenzi pesa, haya mume wa mtu ndio mwenye pesa jiachie vizuri mishalizwa huko ndio mnatafuta vijana wakuoa. Mambo ya kuanza mechi eti nishafungwa goli Moja bila hayo Mambo siyawezi kwakweli. Mabinti lazma wajue maisha ni hatua sio kutaka makubwa alafu hata akili ya kuzuia mimba hajui
 
Nakumbuka nilipopelekwa nyumbani kwa baba mzazi (nilizaliwa nje ya ndoa) mama yangu mlezi niliyemkuta alikuwa na watoto 11, wanane kati yao ni wakubwa kwangu nilifika nikiwa darasa la pili kiukweli mama yangu alinichukia sana tena kwa uwazi na mara nyingi baba alikuwa masafa.

Tuwalee vizur watoto wa wenza wetu kwani kesho ndiyo yenye hofu nyingi kuliko leo.

Vizuri boss
 
Siku hizi wanaume kuzaa hovyo hovyo na kila sehemu ishakuwa kama fashion vile Ila hii kitu inaaribu psychology ya Watoto wa Nje ya ndoa Yani wanatengwa kwenye kila sehemu hawathaminiki kabisa wanaonekana kama watoto wa bahati mbaya as if waliomba wazaliwe nje ya ndoa

Wanaume ndo wanaotengeneza hii sumu ya kuwatenga watoto wa nje ya ndoa
Ni Jambo Zuri sana kama mwanaume atasimama na kuwaunganisha watoto wote na Watoto Wote Kujuana na kuwa Kimoja sio kutengwa kama vile hawastahili au hawana thamani kama hao watoto wengine

Ila Watoto wa nje ya ndoa mambo yao yanawanyookeaga sana kuliko wa ndani ya ndoa

Kuzaa zaa hovyo kunafanya kuaribu psychology ya Watoto

Mimi nilipompata binti yangu nje ya ndoa nilifanya mambo kadhaa. Kwanza nilimtambulisha kwa dada yake mkubwa, nikamtambulisha kwa mke wangu mkubwa, alafu mwisho nikamtambulisha kwenye familia na ukoo.

Mama yake alivyoona ule ujasiri wa kumtambulisha mwanangu kwa ndugu zake bila shida, si akakubali kuunga tela kawa mke wa pili. Mpaka sasa nachakata ngozi vizuri tu. Yeye nimemkuta na mtoto wake wa kiume, huyo mtoto namchukulia kama mwanangu pia kwasababu baba yake alishatwaliwa hivyo naziba pengo.

Rai yangu kwa wanaume wenzangu: Kabla ya kuingia kwenye mahusiano na wanawake ambao tunajua hatuna malengo nao, tuwe wawazi. Ikiwezekana tukatae ishu ya kuwa na mtoto kwasababu hii kitu siyo sifa nzuri na jamii inateseka kwa makosa yetu wanaume.

Tusiongeze idadi ya watoto bila kuwa na utaratibu wa kuwalea kwa maana ya kuwa katika maisha yao ili na wao wajihisi sehemu ya familia na jamii kwa ujumla.
 
Mme wangu alikuwa na watoto wa nje ya ndoa wanne, wote nimewatambua, shida ikaja mtoto wa nje ya ndoa mmoja ni mkorofi anataka arithi kila kitu cha baba yake mwenyewe.

Imenitesa imenifikisha mahakamani. Sometimes hawa watoto wa nje ya ndoa wengine ni wasumbufu mno.
Sasa simbaka awemo kwe urithi
 
Back
Top Bottom