Hii tabia ya kufundisha watoto kuita wakubwa 'uncle' au 'aunt' ni sahihi?

Watoto wetu wakitoka huko kwenye shule za INGILISHI MIDIAMU ndio wanakuja na hayo, maana hata dreva wa gari la shule anaitwa anko, wale wanaowahudumia pale shuleni nao wanaitwa anko/anti
Inafika pahala hata kuwafahamisha kwa ndugu zako inachanganya, nimeamua ndugu zangu waitwe Kiswahili baba mdogo, mjomba, ma unle wanakuwa hao ma dereva wa shule
 
Amina Chifupa (RIP) na Masoud, enzi hizo kipindi cha watoto pale Kitegauchumi, Amina alijiita "Mam Mdogo" na Masoud akajiita "Ba Mdogo" baadae nadhani walielewa athari za ile style, wakabadili na kuanza kujiita "aunt Amina" na "Uncle Masoud"
Tulifahamushwa mdogo wake baba ni baba mdogo na mdogo wake mama ni mama mdogo. Rafiki wa mama ni mama Asha, mama Clara sasa siku hizi mdogo wako anaitwa uncle na mlinzi wa kwenye gate anaitwa uncle kwakweli ni mchanganyiko
 
Kiingereza cha baba mkubwa/mdogo na mama mkubwa/mdogo ni kipi ili watoto wetu waendeleze uafrica ndani English tafadhali!!! Manaake kutafsiri vitu vingine moja kwa moja inagoma
 
Sasa ulitaka mwanangu akikutana na watu huko mtaani nimwambieje? Maana kuna watu wazima ambao ni marafiki zangu siwezi kumwambia awaite dada hiyo kitu haipo kabisa, hao ni mashangazi na wajomba wa hiari ni kawaida tu, sema mnaitumia hiyo heshima vibaya
 
Kiingereza cha baba mkubwa/mdogo na mama mkubwa/mdogo ni kipi ili watoto wetu waendeleze uafrica ndani English tafadhali!!! Manaake kutafsiri vitu vingine moja kwa moja inagoma
Baba mkubwa ni big father baba mdogo ni small father na kwa mama ni ivoivo big and small mother
 
Back
Top Bottom