Hii sio Siasa!

Nungunungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2007
311
13
Baada ya uchaguzi kumalizika na wakati watu wakitafakari ni muhimu kufahamu:
Kuwamwagia watu Tindikali sio Siasa. Ni Mauaji. Ni Ugaidi. Tunalaani kama tulivyolaani alipomwagiwa Kubenea.
Kuchoma nyumba za watu sio Siasa. Ni Mauaji. Ni Ugaidi.
Endapo haya tutayashabikia na kuyaona mambo ya kawaida, tuelewe Kenya haipo mbali nasi.
Hayo hatukupata kuyaona huko nyuma na tusingependa yaendelee.
Mwanademokrasia yeyote lazima apinge uhuni wa aina yoyote kwa nguvu zote!
Chama kitakachoshabikia matukio haya hakitastahili kuitwa chama cha siasa.
Mwenye macho haambiwi Tazama.
 

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,187
UCHAGGA NA UKRISTO NDANI YA CHADEMA NI ZAO LA NDOTO ZA MCHANA ZA WALE WAVIVU WA KUFIKIRI

Wanasaikolojia siku zote hutufahamisha ya kwamba NI HULKA YA BINADAMU KUONA TU KILE ANACHOKIFIKIRIA akilini mwake.

Kwa mfano wewe ndugu Mkalagale, kama uko na washikaji wako hapo hivi sasa basi jaribu kufanya zoezi hili hapa simpo na utapata jibu kwa nini unafikiri jinsi unavyofikiri juu ya CHADEMA na hiyo dhana ya miaka nenda rudi ya UCHAGA:

1. Jiweke kwamba wewe ni refarii hivyo hutoshiriki kama mchezaji katika zoezi hili,

2. Jitahidi walau ukawapate kama watu wanne hivi kushiriki zoezi hili,

3. kama mku labda ndani ya nyumba hivi; nyumbani, ofisini, au hata ndani tu ya gari vile - hebu kawaambie kila mmoja wao aangalie nje kila mmoja kwa nafasi yake.

4. Wakimaliza kufanya zoezi hilo la kuangalia nje, sasa waambie kila mmoja akupe jibu juu ya KITU KIMOJA TU alichokiona wakati ule ulipompa nafasi ya kuangalia nje,

5. Kanuni mojawapo ili zoezi hili lifanikiwe ni kwamba MAREJESHO YOTE YA KITU GANI MTU ALIONA KWA KUCHUNGULIA nje kupitia dirisha au mlangoni NI SHARTI UPEWE KWA KUNONG'ONEZEWA MASIKIONI ili mtu mmoja asije akaamua kukupa tu jubu la wasemaji watakaomtanguia kukupa marejesho ya zoezi lenyewewe,

NB: Mwisho wa zoezi hili, amini usiamini, utastajaabishwa sana kugundua kwamba JAPO DIRISHA NI MOJA PA KUCHUNGULIA NA KULETA MAELEZO KWAMBA MSHIRIKI KAONA NINI NJE LAKINI AJABU NI KWAMBA KILA MMOJA ATAKUPA JIBU TOFAUTI TOFAUTI kulingana na kile kitu ambacho ndicho kinachomgusa zaidi kwenye ubongo wake na hivyo kupendezewa nayo na kutani kulisikia wakati wowote ule.

Kwa mfano:

a. Haitoshangaza sana kumsikia mwana dada binti mrembo atakuambia alipochungulia nje yeye aliona maua mazuri sana.

b. Kama kulikua na mtoto wa Rostam Aziz kwenye hilo kundi lako la mazoezi sana sana huenda akakuambia ama amemuona mtoto wa Robert Mugabe anapita au kaona Mercedez Benze SE 200 Model ikipita.

c. Pengine Tambwe Hizza kama alikwepo naye kwenye timu yako akakunong'onezea kwamba kamuona kijana mchuuza mkaa akipita na mzigo mzito sana wa magunia mawili akikokota kwenye baiskeli.

d. Tuseme zoezi hili lilifanyika mijini basi hapo utamsikia alosto mwenzangu na mimi yeye akikuambia kwamba alipochungulia kupitia dirisha la hoteli ya yule Mganda orofa ya 3 pale kwenye jengo la Benjamin Mkapa - Posta, kati ya vitu vyote pale nje yeye atakuambia ameona dala dala ya kwenda Mbagala Rangi Tatu express bila kugeuzia pale kwa Aziz Ali.

Kwa matiki ya zoezi hili ambalo halihitaji usomi wa zaidi ya darasa la pili tu, basi mwenzangu utagundua kwa nini mtu akipiga darubini ndani ya CHADEMA basi yeye huona tu sura za wanyama fulani wanaoitwa WACHAGGA wakipiga kura Igunga ha kufikia mtu wa elfu 23.

Nasema tangu mara baada ya zoezi hili hutokaa uwapende tena Mwana-CCM yeyote anayeshindwa kuona UTANZANIA ndani ya wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro na badala yake UCHAGGA wao ndio hujitokeza mbele zaidi hasa kitu uchaguzi unapoitishwa popote pale.

Na kama sikosei, sasa sasa mtu kama huyo hutochelewa kumuona kama Nape Nnauye anayetangazia umma wa Tanzania fungu la matokeo ambayo masikio yake yangependa kusikia, hata kama kufanya hivyo huenda ukampokonya Kafumu Ubunge wake huo geresha baada ya siku 180.

Ndio, nasema tangu sasa huenda Magwanda Orijino nitakua nimefanikiwa kukuelimisha taratibu humu mpaka kujihisi kama vile ulikua sawa tu na Tambwe Hizza wa kwenye mfano tu hapo juu aliyeona kijana na gunia la mkaa kulingana na mahitaji ya kule kwake Mbagalla (na hasa zama hizi za Umeme Ngeleja), wakati ulipokua unauanzisha uzi huu hapa chini, hata ukashindwa kuwaona WATANZANIA badala yake ukawaona tu WACHAGGA wakitia timu ndani ya nyumba ya CHADEMA ...

... poorBaba wa Taifa Mwalimu Nyerere hebu kamsikie huyu mjukuu wako alivyo na mdomo mchafu uliojaa ukabila!!!!!!!!!!!!

Nadhani baada ya kuelimika hapa Jamvini unajisikia kama vile umetua mzigo vile au sio?? Hebu jitofautishe basi na lile Genge la akina Mkigoma, FF, Rejao, Mbopo, Nape na wengine wa aina yao ambao hawakuwahi kuandika kitu humu zaidi ya kudondosha kimstari kimoja ama lenye tusi, kejeni, mashairi, uzabizabina (Rweyemamu et al 2011) na wengine wengi kama hao.

Mpaka hapo naomba ukajipime wewe mwenyewe na ukajiamulie tu kwa moyo mkunjufu kabisa kama kweli leo hii uko kwenye mstari sahihi kuitwa JF GREAT THINKER au pengine utakua umeteleza kidogo kuungana na akina HAO kule katika ulimwengu wa JF GREAT STINCKERS.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom