Hii sheria ilikuwa poa sana kwa Guest za Dar ila Meya ameikanusha!

Mr Hero

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
5,540
7,452
Guesthouse-for-Rent-in-Sihanoukville3.jpg



Ijumaa ya May 6 2016 kama ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii hususani Whatsappnajua utakuwa ulipokea ujumbe ambao ulikuwa unaripotiwa kuwa umetoka kwa meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita, ujumbe uliokuwa umeenea ulikuwa unahusisha kuwa meya wa Dar es Salaam Isaya Mwita ametangaza sheria mpya.

Meya Isaya Mwita ameongea na millardayo.com na kueleza kuwa ujumbe unaoenea kuwa ametangaza sheria mpya Dar es Salaam sio wa kweli na umetungwa na watu ambao wanapanga kumchafulia jina lake.

ADAS.jpg

Ujumbe wa uongo ambao ulisambazwa leo May 6 2016 na kudaiwa umetoka kwa meya wa Dar es Salaam

“Sio kweli kuwa kuna sehemu nimetoa statement ya namna hiyo ila huyo atakayekuwa ameandika atakuwa na lengo tofauti, kwa hiyo naomba wananchi wapuuze hiyo statement ambayo imekuwa ikisambaa, bahati mbaya sikuwahi kupata mtu akiuliza maoni yoyote kuhusiana na tukio hilo la Kimara ila kwa upande wangu sijatoa tamko lolote”

Kama utakuwa unakumbuka vizuri usiku wa May 1 2016 millardayo.com iliripoti habari za mwanamke kuuwawa na mtu anayeaminika kuwa ni mpenzi wake kwa kudaiwa kuwekewa sumu kwenye chakula na mwanaume kuondoka kwa kumuaga mlinzi kuwa anaenda kununua vocha.
 
Mkishapigwa picha mkiondoka mnapewa au inabandikwa guest kwa kumbukumbu?? Wachepukaji mpooo. Kweli hii sheria inatakiwa ianzishwe
 
Wenzetu nchi za wenzetu wanalazimishwa kufunga CCTV camera kila sehemu ya huduma za jamii hata kama Duka au Saloon kwa usalama na matukio kama hayo, nawaza tu sheria hiyo ingekuwa hapa kwetu mpaka mama lishe waweke CCTV duh sijui ingekuwaje
 
Back
Top Bottom