MDANGANYIKAJI
Member
- Jan 27, 2011
- 77
- 59
Nakubaliana na wewe mkuuHao uliowapa lifti hawakuwa askari ni matapeli kama walivyo wengine, askari wanaoheshimu kazi zao wapo. Cha kufanya askari akikuomba lifti kariri '"orce number yake" utaujua ukweli.
Khaa, mboana mie natoaga sana lifti kwa askari na wanafunzi. Coz ndo nawaona kidogo ni ngumu kunitapeli. Juzi kati nilitoa lift kwa askari magereza kumbe mmoja wa wale askari nilisoma nae msingi enzi hizo za miaka ya tisini. Nilifurahi sana, nikamtembelea kwake akaja kwangu. Nawaaminia hawa watu. Sasa kama nao wanakua hivyo baasi tinted ndo suluhishi. Tena ile ambayo huoni nnje na wewe hakuoni.
Leo mapema asubuhi kuna mkaka nilimnyima lift kwa kuogopa mambo kama hayo. Ilikua saa tisa alfajiri. Jamaa kavalia tu poa. Lakini alfajiri ile nkasema chochote chaweza tokea. I felt guilty kumpita jamaa lakini hamna jisni
Na wewe 999 ulitoka wapi alfajiri yote hiyo?
Ndo nlikua naingia kazini mkuu. Now niko home nabofya tu!
Mimi yalinikuta, kuna watu wa mtaani kwetu ambao sikuwa nawafahamu sana zaidi ya ukazi wa mtaa mmoja tu waliniomba lift. Kwa kuwa huwa niko peke yangu au na wife tu nilizoea kuweka simu sehemu yoyote ndani ya gari hata siti ya nyuma. Siku nimewachukua nikajisahu kuiondoa,baada ya kushuka nilipotaka kupiga simu ndipo nilipogundua simu yangu haikuwepo sehemu yake.
Siku ya pili nilipowauliza waliapa kwa miungu yote kwamba hawajui chochote, nikamwachia Mungu.