Mr pianoman
JF-Expert Member
- May 22, 2019
- 2,552
- 6,114
Kwanza niwape pole sana ccm kwa spidi mnayo pelekwa na vyama vya upinzani hasa hasa chadema na mgombea wao Tundu Lissu. Tunajua hamku tarajia kama mambo yatakuwa hivi yanavyo onekana siku chache tangu kampeni zianze kwani kwa miaka mitano yote mlikuwa mkijimwambafai wenyewe tu kwenye majukwaa na kufikia hatua ya kusema upinzani nchi umekufa ila leo sizani kama mtatamka hili neno kwani mmejionea wenyewe.
Ushauri wangu kwa CCM nawaomba kuanzia leo muache zile kampeni zenu za kujisifia eti mmejenga sijui barabara, reli, madaraja, mmenunua ndege, na mambo mengine kama hayo ambayo hayagusi maisha ya watu moja kwa moja ila yanagusa vitu.
Kwa miaka mitano yote hizi ndizo zilikuwa kampeni zenu mpaka watu wamesha zichoka kabisa na hawawezi kuwaelewa kabisa kwani ni hoja ambazo hata mimi darasa la saba nikisimama jukwaani nazipangua ipasavyo.
CCM hoja mlizo takiwa kuja nazo hivi sasa ni hoja ambazo zinagusa maisha ya watu kwa asilimia mia moja. Na mambo yenyewe ambayo watu wanataka kuyasikia kutoka kwenu ni kama
Ajira
Uhuru na haki
Huduma za afya ikiwemo bima za afya
Punguzo la kodi
Ulinzi na usalama kwa raia
Ongezeko la bei za bidhaa
Masilahi kwa watumishi wa umma
Ushirikiano mzuri wa kimataifa.
Na mengineyo mengi kama hayo ndio wananchi wanataka kusikia kutoka kwenu CCM.
Jana kwa mara ya kwanza Magufuli akiwa jukwaani anazungumzia ajira za walimu na kutangaza zinatoka muda si mrefu hivi ndivyo vitu ambavyo watu wanataka kusikia sasa na hakika mtawavutia wengi kwani hapa mmewagusa wengi japo mmegusia sekta ya elimu peke yake ila kuna sekta nyingi bado vijana wanateseka mtaani wakisubiri ajira zake.
Sekta kama afya, watu wa kilimo, uhasibu, askari wapya ambao hapa ilikuwa kila mwaka ajira za majeshi zinatoka ila katika awamu hii ya tano imekuwa tofauti kidogo kwani tumeshuhudia vijana wengi wa jkt wakirudishwa nyumbani na kuna tetesi kwamba vijana zaidi ya elfu kumi wa jkt wanaandaliwa kurudi nyumbani muda sio mrefu kwani mpaka nauli ya kurudi nyumbani wamesha saini huko makambini kwao.
Je ni kweli kwamba ajira majeshini hakuna mpaka turudishe vijana hawa wa JKT nyumbani kwa wingi namna hiyo?
Vipi kuhusu wazazi ndugu na jamaa wa hawa vijana si ndio wapiga kura wa leo mnao waomba huko mtaani na Kuwaita wanyonge sasa mbona ndio mnazidi kuwanyonga zaidi vijana wao?
CCM huu ni ushauri wangu mdogo kwenu tu mimi darasa la saba B ufanyieni kazi kwani kilicho baki ni kumwaga ajira za serikali mtaani kidogo mtaeleweka kwa vijana na watu wengine. Acheni kutuimbia hizo ngonjera zenu za KUNUNUA NA KUJENGA tumezichoka.