Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,860
- 50,646
Mimi sina hata chembe ya ujuzi wa masuala ya kiuchumi, siyajui kabisa,lakini najua kuna sera ambazo huendesha mambo ya mabenki kwenye nchi zote duniani. Na sera hizo hutungwa au hupitishwa na wanasiasa.
Swali langu ni hili: Hapa Tanzania mtu akienda kukopa mkopo binafsi kwenye taasisi za kifedha hukatwa kiasi fulani cha fedha kama gharama za mkopo. Kwa mfano mtu anakopa milioni Ishirini (20,000,000) basi hukatwa hadi shilingi laki sita(600,000) kama gharama za Mkopo. Hivi hii ni sahihi kweli? Benki inaandika imemkopesha Ml. 20 wakati kiuhalisia mkopoji kaondoka na Ml. 19,400,000. Ni haki kutoza Riba kwa kusema unatoza riba kwenye Ml.20 ya mkopo wakati Mkopaji mwenyewe umempa Ml. 19,400,000?. Nataka kujua kama huu ni utaalam wa kibenki au ni sera za kibenki au ni mfumo uliopo kwa kufuata sera za BOT?
Hiyo ni bima ya mkopo ikiwa utakufa kabla ya kumaliza marejesho
hiyo 600,000tzs iliyokatwa hapo ni down payment ya mwanzo kabisa,kwa makubaliano kila mwezi lazma urudishe kiasi fulani kwa muda waliokupangia kama ni miaka 2 au vinginevyo.kwa hiyo kwente hiyo mil.20 downpayment ya kila mwezi ni 600,000tzs kwa miezi/miaka mliokubaliana.
Ndugu yangu kuna tofauti kati ya "Loan Down Payment" na "Loan Processing fee" Deni linabakia pale pale na laki sita umekatwa! Unafanyaje hiyo unayoisema "Loan Down Payment" kabla kuutumia mkopo kwa lengo ulilolikusudia?hiyo 600,000tzs iliyokatwa hapo ni insurance/bima ya mkopo. na baada ya hapo utaanza kulipa down payment ya mwanzo kabisa,kwa makubaliano kila mwezi lazma urudishe kiasi fulani kwa muda waliokupangia kama ni miaka 2 au vinginevyo.
KABAYAPAITA hapa kuna hii kitu inatwa "Loan Processing fee" wala haina uhusiano na "Interest" kwani bado riba utakatwa na hiyo uliyokatwa haitaingia kwenye hesabu za mkopo unaolipa!
Ha! Ha! Ha! Eddy nashukuru kwa kuwa pamoja katika hili. Kukopesha si ndiyo biashara yenyewe ya mabenki, na wafanyakazi mishahara yao si inatokana na riba inayotozwa kwenye mikopo na kwenye uwekezaji mwingine unaofanywa na Benki, kama kwenye ununuzi wa hati fungani za serikali? Sasa hii "Loan Processing fee" kazi yake ni nini hasa na faida yake kwa mkopaji ni nini?Allen kwa hili leo tuko pamoja, halafu wakati unaomba mkopo hawakwambii haya makandokando utakutana nayo kwenye mkataba tu, kwa kifupi hili ni jipu na gavana asipolitolea ufafanuzi lazima limlipukie tu.
hata mie hili linanichanganya sana, hizo gharama za mkopo ndo inakuwaje hasa? bado hapo afisa mikopo anataka hongo ya milioni moja. jamaa yangu alikopa benki mil 5 akawa anarejesha laki sita ina maana hadi mkopo kukamilika atakuwa amerejesha 7.2 sasa hiyo riba ni 45% sasa bora nikakope saccos au nikachukue mali kauli dukani kwa mangi.
Hapa tunahitaji riba na tozo elekezi kutoka benki kuu.