Hii ni sawa?.


kwanza kabisa unajua kuwa huyo binti anaishi kwenye nyumba ya dada yake?

Pia unajua kuwa anachungwa na kubanwa ili awe katika mstari ulioonyooka?

Unadhani atatokaje hovyo hovyo kama gesti?

Badala ya kumlaumu kwa nini msitafute solution ya pamoja?
.....

Huyu Jamaa Kahaso Sana Kwa Hii K,Na Ndio Maana Anataka Waonane Ili Wazungumze!
Ina Maana Hakuna Siku Ambayo Anapata Mda Wa Kuonana Na Jamaa?
 
Mi Najua Machungu Aliyo Nayo Ndugu Yangu!..Hizi Sketi Sijui Zina Lengo Gani Na Nafsi Zetu!?
Pole Sana,Mi Naomba Legeza Upendo Na Usumbufu Kwake Kama Ndugu Yangu MASALAPA livyokushauri!
 
Tena Ashukuru We Jamaa Una Uvumilivu Sana(Sijui Upole?)
Aisee Nami X Wangu Nilizama Kwake,Kila Wiki Nilihitaji Kumuona Ila Akaletaga Kama Hizo Za Wako,Mi Sikuchelewa Kumpa Makavu Na Kukata Mawasiliano,Baada Ya Mda Akawa Makini Ila Ndo Tulishindwana...Mpaka Sasa tumeachana Wakati Bado Nampenda Saaaana!!
 
Kama kweli unampenda, jaribu kufanya utafiti kama hana mtu mwingine maana hali kama hizo zinaashilia kutopedwa au kuwa na mtu mwingine.
 
pengine inawezekana anaogopa kutoka naww kwa kilikinachodaiwa ni tabia za mabinti walokole na vp www umeshatambulishwa hapo kwao nakama ni tayar kwann asiage anakuja kukusalimia na kama hujatambulishwa basi inawezekana ana waswasi
 
Wewe huyo siyo mchumba. Nijuavyo mchumba ni mtu ambaye umeshaenda mpaka kwao kujitambulisha. na saa yoyote akiaga anakuja kwako njia ni nyeupe. Hapo sasa hivi unacholilia ni uzinzi tu. Mtoto wa watu anajiuliza mara mia hivi huyu jamaa akinitoboa atakubali kuendelea kuwa na mimi? ndo maana haji. na ataendelea kufanya hivyo hivyo mpaka ukajitambulishe kwao, ukionyesha nia mzigo utapata. Kajitambulishe.
 
Habari wana JF,nina kerwa sana na jambo hili kwa muda mrefu nimelileta kwenu ili nipate mawazo yenu,Mimi ni kijana nina mchumba ila tabia za mchumba wangu zinanitia mashaka mpaka nimeanza kuhisi kushindwa kuwa katika huu uchumba.
Habari iko hivi,
Mchumba wangu anakaa kwa dada yake ambae ameolewa maeneo ya jirani na ninapokaa pia ni wacha mungu sana kila jumapili ni lazima waende kanisani.Mazingira anayoishi mchumba wangu kidogo yanabana hivyo swala la kuonana mimi na yeye hata kwa mazungumzo ni shida kidogo hivyo kuonana inakuwa ni kwa muda mfupi anapopata nafasi.Kutoka na hali ya kubanwa mimi nikamshauri kuwa awe anatafuta siku ambayo anaona yuko free anijuze alafu tutoke mbali na maeneo ya kwao na yeye akasema sawa,kuna siku aliniambia kesho atakua poa ivyo tutatoka nami nikamwambia sawa ilipofika iyo siku ya kutoka nikamtafuta kwenye simu alichonijibu ni kuwa ametoka amepata simu kutoka kwa dada yake mkubwa hivyo yupo huko mimi nikasema sawa ila nikamuuliza kwanini hukunipa taarifa kuwa umepatwa na dharula akasema amejisahau ila nimsamehe nikamsamehe,siku nyingine tena akasema siku flani ntakuwa free hivyo tutatoka, ilipofika siku yenyewe mambo yakawa yaleyale ameeenda tena kwa dada yake mkubwa tena bila kunijulisha mimi nikamsamehe tena mara nyingine.
Baada ya muda kidogo mimi nikaitwa kwenye usaili na tume ya Ajira Morogoro nilipokua huko akaniambia ukirudi tutatoka mana shemeji anaondoka hivyo itakuwa rahisi yeye kutoka,nilipo rudi akaniambia shemeji hajaondoka hivyo hawezi kutoka, ni kweli shemeji yake hakuondoka ilo likawa limeeleweka, sasa juzi akaniambia kesho ntakuwa na muda mimi nikamwambia sawa ilipofika jioni akaanza kusema kuwa simu yake haina charg hivyo ana wasiwasi kuwa itazima na hana chaja kwa ajili ya kuichagi hivyo atashindwa wasiliana na mimi atakapo kuwa anatoka kwao mimi nikamwambia wewe ukiwa unatoka kwenu nijulishe hata kwa kutumia simu ya mtu mwingine mimi ntakuelelkeza nilipo na utanikuta hapo sasa ajabu ni kwamba simu yake ilipozima kama mwenyewe alivyodao ni chagi haina mpaka nanivyoandika huu uzi simu yake haipatikani na hakuna ujumbe wowote wa kunijulisha kuwa hatokuja.
Jamani labda mimi sijui, kweli hii ni sawa? watu mnapeana miadi halafu mwenzako hatokei na wala hatoi taarifa kuwa hatokuja,mimi napatwa na kichefuchefu na hii tabia yake mana anaukologa ubongo wangu nashindwa kuelewa ana mawazo gani kichwani kwake.
Nimefikia hatua ya kufikiria kuachana na huyu mtu mana sidhani kama ntaishi kwa raha siku tutakapo kuwa mke/mme mana sasa hivi tu ananipasua kichwa huko mbele je itakuwaje,nimejaribu kumweleza umuhimu wa ahadi lakini naona anielewi sasa najiuliza hii ni tabia ya mtu au ni kweli anabanwa na kama anabanwa kwanini hatoi taarifa kuwa hatuweza kuja.
Ndugu naombeni mawazo yenu nifanyeje kwenye hili mana nilipanga awe mke wangu,nampenda sana huyu msichana ila tatizo ndo ilo sijui nifanyeje wakuu.

pole sana kaka. Fanya hivi
kama kweli ana mtu mwingine anamzingua utajua tu. Fanya kupuuzia kama unataka kumwacha. Yaani kama ulizoea kupigia simu mara 5 kwa siku punguza au acha, asipoulizia mabadiliko yeyote anayoyaona kwa ko..baba lala mbele. Shukuru mungu kaanza kuoonesha kucha mapema kabla ya mikataba ya kudumu..utoe moyo kwenye mafuta ya transifoma kaka pliz
 
Hiyo K ni ya kupiga chini tu wewe,


pole sana kaka. Fanya hivi
kama kweli ana mtu mwingine anamzingua utajua tu. Fanya kupuuzia kama unataka kumwacha. Yaani kama ulizoea kupigia simu mara 5 kwa siku punguza au acha, asipoulizia mabadiliko yeyote anayoyaona kwa ko..baba lala mbele. Shukuru mungu kaanza kuoonesha kucha mapema kabla ya mikataba ya kudumu..utoe moyo kwenye mafuta ya transifoma kaka pliz
 
Huyo bnt ana visabsabina but madem wengi ndo tabia zao hasa wale wanaojiona wazuri sasa we mchunie mazima tuone atafanyaje........
 
Kama vip vip tu binua meza pasilike kabisa kuliko kuchanganywa na situation isiyo na majibu yasiyoeleweka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom