Sio sawa sana, anachopaswa ni yeye kutathmini ugonjwa wako, matokeo ya maabara, hali yako kiafya, matatizo mengine uliyonayo na kadhalika halafu ajue ni dawa gani nzuri kwako. Baada ya hapo atakuambia nakuandikia dawa fulani, ndipo wewe useme kama unaafiki. Tusitumie dawa kwa mazoea jamani, bali ni kwa hali halisi ya ugonjwa na mgonjwa.
Mkuu, doc kudiscuss na mgonjwa aina ya tiba ni muhimu sana hasa kwa mgonjwa. Kwa mfano wako wagonjwa ambao hawawezi kunywa dawa muda mrefu, kwa kuogopa kukatisha dose Mara nyingi hushauriwa kunywa dose ya muda mfupi. Unachozungumza wewe ni suala la doc kuamua ampe dawa gani mgonjwa kulingana na madhara yaliyosababishwa na ugonjwa alionao. Doc kumuuliza mgonjwa anatumia dawa gani haimzuii doc kutoa dawa nyingine kulingana na severity ya ugonjwa. Aina ya tabibu unayozungumza wewe imepitwa na wakati. Bila kusahau kuwa, kitendo cha doc kudiscuss na mgonjwa kwa makini ni nusu tiba tayari kisaikolojia kwa mgonjwaMimi nasema si sawa kabisa ila dawa hutolewa kulingana na mgonjwa alivyokuja. Coz kama ni severe malaria mfano huwezi tumia dawa ya uncomplicated malaria. Mgonjwa kama anaallergy na dawa huulizwa kama na allergy na dawa yeyote kwenye history. Mimi niulizi nyinyi wadanganyika hivi ukiumwa typhoid au pneumonia huwa unafika kwa Dr kuwa mimi natumia ciprofloxacin au chlomphenicol si unatumia dawa yeyote anayojua Dr kuwa inatibu ugonjwa husika. Hapa ndo maana tunaendelea kusababisha resistance. Sasa mgonjwa nakuja kwangu Dr mimi huwa situmii Alu natumia SP. Wakati sp zilishasitishwa tangu 2007. Huyu hata simsikilizi coz ni lay man na hana information. Yaani hata leo nimetofautiana na mgonjwa hivi hivi. Huwezi nifundisha niandike dawa kulingana na matakwa yako. Watanzania tuache umuch know tutapoteza ndugu zetu na marafiki zetu pasipo sababu.
sasa kwa mtu ambaye ni layman hajui hata jina lolote la dawa si inakuwa ngumu kwake? na mtu ambaye hutumia say sp ila huwa kila baada ya mwezi anaumwa tena malaria, akiulizwa swali hilo na akisema huwa anatumia sp hapo dr akimpa tena sp itamsaidiaje? ni kusaidiana tu si-challenge madaktari!
Unakwenda hospitali unapimwa na baada ya kugundulika unaumwa malaria daktari anakuuliza, "unatumiaga dawa gani?" kisha anakuandikia hiyo hiyo uliyomuandikia kuwa huwa unatumia!!!
Naomba kuuliza hii ni sawa au?