Hii ni sawa kwa daktari

Hii ni sawa kwa daktari

Aine

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
1,603
Reaction score
489
Unakwenda hospitali unapimwa na baada ya kugundulika unaumwa malaria daktari anakuuliza, "unatumiaga dawa gani?" kisha anakuandikia hiyo hiyo uliyomuandikia kuwa huwa unatumia!!!

Naomba kuuliza hii ni sawa au?
 
unakwenda hospitali unapimwa na baada ya kugundulika unaumwa malaria daktari anakuuliza, "unatumiaga dawa gani?" kisha anakuandikia hiyo hiyo uliyomuandikia kuwa huwa unatumia!!!

naomba kuuliza hii ni sawa au?
Ni sahihi kabisa mkuu, doc kukuuliza hivyo maana yake anakuepusha na madhara mengi likiwemo la allergy na baadhi ya dawa. Kwani mkuu ujasikia kuna watu wana allergy na dawa aina ya SP - zenye sulphur. Hata ukienda kwa wenzetu walioendelea lazima watakuuliza kama una allergy na dawa yoyote. Ni kwa usalama wako mkuu
 
asate kwa kumsaidia ana wabog hawakawii o huyu DR sio
 
haswaaaa, kama unavoulizwa wapenda kinywaji gani! maana kama uliwai tumia dawa fulani ikakuletea matatizo inabadilishwa.
 
Unakwenda hospitali unapimwa na baada ya kugundulika unaumwa malaria daktari anakuuliza, "unatumiaga dawa gani?" kisha anakuandikia hiyo hiyo uliyomuandikia kuwa huwa unatumia!!!

Naomba kuuliza hii ni sawa au?

sasa kama unajua na aina ya dawa na unaulizwa unahoji kwa nini niulizwe nyie ndio mnafanya kazi ya udocta iwe ngumu kwa kutoelewa
acha jeuri,kuingilia office za watu
 
Ni sawa kabisa! Hata ukija duka la dawa, achilia mbali huko hosptali, kununua dawa za kutuliza maumivu tutakuuliza, je unatumia dawa gani?
 
Jaman hata nyumbani kwako unaulizwa na mkeo utapenda ule nn leo??yaaani roho inapennda ?na dr Ana haki ya kumuuuliza mgonjwa wake anatumia dawa gani ndo Ina msaidia
 
sasa kama unajua na aina ya dawa na unaulizwa unahoji kwa nini niulizwe nyie ndio mnafanya kazi ya udocta iwe ngumu kwa kutoelewa
acha jeuri,kuingilia office za watu
mwili wako sio wa majaribio.... Anapokuuliza inamrahisishia akupe nini...
 
Unakwenda hospitali unapimwa na baada ya kugundulika unaumwa malaria daktari anakuuliza, "unatumiaga dawa gani?" kisha anakuandikia hiyo hiyo uliyomuandikia kuwa huwa unatumia!!!

Naomba kuuliza hii ni sawa au?
Samahani kama ninakosea!
Bilashaka muuliza swali ni mwanasiasa au mfuasi/shabiki wa chama fulani.
Maswali yake yanafanana sana na baadhi ya wanasiasa ninaokutana nao ninapokuwa kazini kwangu hususani pale OPD.
Mara nyingi mwanasiasa anaamini kwamba kila kitu wewe daktari ndiye final say, na hata ukimuuliza huwa unatumia dawa gani ya ugonjwa huu, yeye atakwambia WEWE NI DAKTARI HUTAKIWI KUNIULIZA MIMI MGONJWA DAWA YA KUTUMIA. HILO NI JUKUMU LAKO DAKTARI.
Hii ni kama vile baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani vinaamini kwamba kila kitu lazima kifanywe na Serikali hata kama kiko ndani ya uwezo wake.
Ajabu iliyoje, waweza kukuta mwanasiasa huyuhuyu anamnyanyasa mkewe then ndo anakuwa wa kwanza kublame kwamba Wanawake wananyanyasika na Serikali imekaa kimya.
TUSIINGIZE POLITICS KWENYE FANI ZA WATU!
 
Dawa za Malaria zipo nyingi,nyingine zina reaction,nlisikia watu wenye sukari huwa hawatumii kwinini ulishasikia?
 
NI SAWA NA NI SAHIHI KABISA KUKUULIZA SWALI HILO.
Mbali na madhara yatokanayo na dawa, pia tunazingatia zaidi ADHERENCE ya hiyo dawa. Inawezekana wewe umezowea kumeza Single dose kama SP, METAKELFINE etc lakini daktari kama hatokuuliza na akakuandikia ALU ambazo ni 24 tablets kwa six doses, au QUININE 42 tablets kwa 21 doses hapo lazima ufuatiliaji wa dawa utakuwa hafifu na matokeo yake yanakuwa mabaya na pengine kupelekea hata DRUG RESISTANCE.
 
Mimi nasema si sawa kabisa ila dawa hutolewa kulingana na mgonjwa alivyokuja. Coz kama ni severe malaria mfano huwezi tumia dawa ya uncomplicated malaria. Mgonjwa kama anaallergy na dawa huulizwa kama na allergy na dawa yeyote kwenye history. Mimi niulizi nyinyi wadanganyika hivi ukiumwa typhoid au pneumonia huwa unafika kwa Dr kuwa mimi natumia ciprofloxacin au chlomphenicol si unatumia dawa yeyote anayojua Dr kuwa inatibu ugonjwa husika. Hapa ndo maana tunaendelea kusababisha resistance. Sasa mgonjwa nakuja kwangu Dr mimi huwa situmii Alu natumia SP. Wakati sp zilishasitishwa tangu 2007. Huyu hata simsikilizi coz ni lay man na hana information. Yaani hata leo nimetofautiana na mgonjwa hivi hivi. Huwezi nifundisha niandike dawa kulingana na matakwa yako. Watanzania tuache umuch know tutapoteza ndugu zetu na marafiki zetu pasipo sababu.
 
Unakwenda hospitali unapimwa na baada ya kugundulika unaumwa malaria daktari anakuuliza, "unatumiaga dawa gani?" kisha anakuandikia hiyo hiyo uliyomuandikia kuwa huwa unatumia!!!

Naomba kuuliza hii ni sawa au?

Ni sawa. Au wewe unasemaje?
 
Samahani kama ninakosea!
Bilashaka muuliza swali ni mwanasiasa au mfuasi/shabiki wa chama fulani.
Maswali yake yanafanana sana na baadhi ya wanasiasa ninaokutana nao ninapokuwa kazini kwangu hususani pale OPD.
Mara nyingi mwanasiasa anaamini kwamba kila kitu wewe daktari ndiye final say, na hata ukimuuliza huwa unatumia dawa gani ya ugonjwa huu, yeye atakwambia WEWE NI DAKTARI HUTAKIWI KUNIULIZA MIMI MGONJWA DAWA YA KUTUMIA. HILO NI JUKUMU LAKO DAKTARI.
Hii ni kama vile baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani vinaamini kwamba kila kitu lazima kifanywe na Serikali hata kama kiko ndani ya uwezo wake.
Ajabu iliyoje, waweza kukuta mwanasiasa huyuhuyu anamnyanyasa mkewe then ndo anakuwa wa kwanza kublame kwamba Wanawake wananyanyasika na Serikali imekaa kimya.
TUSIINGIZE POLITICS KWENYE FANI ZA WATU!

Hii sentensi yako ya mwisho inakusuta mwenyewe. Sioni ulazima wa wewe kuingiza siasa kwenye hii thread.
 
Ni sawa kukuuliza kwa sababu
Moja kujua unauelewa kiasi gani kuhusu dawa
Pili itamsaidia kujua historia yako ya ugonjwa na matibabu yake
Pia teknolojia ni kubwa dawa ni nying so ni kushauriana sio km zamani malaria dawa = kloroquin
Vile vile ni kurithishana ujuz na kubapata feedback ya dawa zinazotumika na zinavyoweza kuponya
 
Back
Top Bottom