Hii ni pesa zaidi ya Benzi

Sim Card

JF-Expert Member
Dec 30, 2019
882
1,594
Wakuu poleni kwa taharuki ya leo ya mechi ya watani wa jadi YANGA NA SIMBA kuahirishwa na TFF bila kufuatwa kwa kanuni na pengine mbaya zaidi bila hata sababu kwa wadau wote wa soka na wananchi kwa ujumla wake. Niende tu moja kwa moja kwenye lengo.

1. Kwa nijuavyo mimi timu zetu Simba na Yanga ni timu kubwa na kongwe kihistoria hapa Tanzania na nje ya Tanzania. Kwa kitendo cha leo bila shaka ni fedha nyingi imepotea kwenye maandalizi ya mechi ya leo kwa ujumla.

2. Naomba kusaidiwa, sheria inasema vipi juu ya fidia endapo vilabu vitaamua kudai fidia kwenye mamlaka husika?

3. Naona sheria za soka sasa zinasiginwa tu bila hata kujali na kuwathamini wadau na wapenzi wa soka.

4. Kwa serikali ilipaswa itumie weledi kutengeneza mawasiliano shirikishi ili kila mdau wa soka hasa wahusika na wapenzi wote wa mpira kuelewa na kuwa na utulivu kuliko kuona serikali haikutizama hili na badala yake attention kubwa ikapelekwa kwenye zawadi ya mzee na uzinduzi wa kitabu.

Mwisho: Hii ni pesa ndefu watu/ wana chi wakiamua kulalamika mahakamani kwa kupotelewa na muda bila sababu za msingi.

Tunaomba kanuni/sheria zituongoze kulitatua jambo hili.
 
Back
Top Bottom