Forgotten
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,347
- 10,223
Habari wana-JF.
Mimi ni mpenzi mkubwa na mfuatiliaji wa soka ila ligi ya Tanzania ilinishinda kwa namna inavyoendeshwa kishkaji. No professionalism kama wanavyojinadi kwa kusaini mikataba kwa mbwembwe.
Ligi ya bongo sifuatilii maana sina hata timu ila leo nineona habari kuwa NBC wameongeza kipengele kwenye mkataba waliosaini kuwa wadhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wakipinga wachezaji kupata udhamini kutoka kwa washindani wao kibiashara.
Hapa nawaelewa kabisa NBC, uwekezaji waliofanya ni mkubwa na hawawezi kukubali washindani wao kibiashara watambe kirahisi tu ila nina wasiwasi na hii mikataba inayosainiwa kwenye hii ligi.
Hii sheria ni ya unyonyaji kwasababu wachezaji hawahusiki kwenye mkataba unaohusu udhamini wa ligi. Duniani kote wachezaji wanakuwa na Image Rights ambazo wana haki 100% kuziuza kwa makampuni au kufanya matangazo ya udhamini kupitia: jina, picha n.k.
Sasa kama NBC anapinga wachezaji kupata udhamini kupitia Image Rights wanapaswa kununua Image Rights za wachezaji wote wa Ligi Kuu bila hivyo ni haki ya mchezaji kutumia jina au picha zake kutangaza bidhaa au biashara za makampuni yanayomdhamini.
Wachezaji wa Tanzania na wa nje wanaocheza Ligi Kuu wanapaswa kufahamishwa kuhusu haki zao maana huwa naona hata wachezaji wa Simba wakifanya matangazo ya Mo ambayo nina wasiwasi hawana mikataba tofauti na ile ya ajira zao, vivyo hivyo kwa Yanga na GSM. Mikataba ya ajira inapaswa kutofautiana na mikataba ya Image Rights.
Hii ligi inakosa professionalism kila mahali hata kipindi Vodacom ni mdhamini Yanga walivunja sheria za Brand Guidelines kwa kubadili rangi za Logo za mdhamini na vilabu kadhaa kuendana na rangi zao tu.
Hii ligi inaendeshwa kishkaji sana.