Chakunyuma
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 810
- 152
Nilikuwa nasikiliza Sauti Amerika wameripoti kuwa katika kata moja huko Igunga wakati watu wanaendelea kupiga kura lilipita gari la sisiem likatangaza eti mgombea wa chadema amejitoa hivyo wakawaomba wasimpigie kura pia wameendelea kuripoti kuwa kuna kata nyingine wasimamizi walikuwa wanawaelekeza wapiga kura kukipigia sisiem, hayo yamesemwa na waangalizi wa uchanguzi mdogo wa Igunga.
Hofu yangu matokeo yanaweza kutokuwa halali kwa visa hivi na vingine ambavyo vimesharipotiwa humu, pia tunajenga au tunabomoa? Huu uchu wa kung'ang'ania madaraka utaliangamiza taifa kama tutaendelea kutumia siasa chafu kushinda. Siombei ila linaweza kujitoza watu wakaamua kudai hatima yao kama kule Ivorycoast na kwingineko.