Hii ni mbaya na hatari kwa mustakabali wa nchi yetu

Chakunyuma

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
810
152
Nilikuwa nasikiliza Sauti Amerika wameripoti kuwa katika kata moja huko Igunga wakati watu wanaendelea kupiga kura lilipita gari la sisiem likatangaza eti mgombea wa chadema amejitoa hivyo wakawaomba wasimpigie kura pia wameendelea kuripoti kuwa kuna kata nyingine wasimamizi walikuwa wanawaelekeza wapiga kura kukipigia sisiem, hayo yamesemwa na waangalizi wa uchanguzi mdogo wa Igunga.

Hofu yangu matokeo yanaweza kutokuwa halali kwa visa hivi na vingine ambavyo vimesharipotiwa humu, pia tunajenga au tunabomoa? Huu uchu wa kung'ang'ania madaraka utaliangamiza taifa kama tutaendelea kutumia siasa chafu kushinda. Siombei ila linaweza kujitoza watu wakaamua kudai hatima yao kama kule Ivorycoast na kwingineko.
 
Nashauri tuchukue hatua je ni hatua gani hizo? Ushauri wako utasaidia sana.
 
Uchaguzi wa jimbo hili ndio umeivua nguo nchi yetu. Ukitafakari mambo yaliyojitokeza huko igunga, unapata sababu ya kumdisqualify aliyekuwa mgombea wa CCM. Hakika kwa ballot box kuing'oa CCM madarakani ni ngumu mno, labda kama tukipata KATIBA MPYA.

Nadhani huu ni wakati muafaka wa kuanzisha movement ya kudai Katiba mpya na Tume huru.
 
nimeyasoma sana mazingira ya chaguzi zetu..lakini NO! something else should be done..I don't know!! it can be a new constitution or something else..I don't have an immediate answer yet!! But, I have a feeling that people's power might take its course, whether sooner or later!!
Take my words!!...
 
A time bomb which CCM has been preparing for the last 25 years is about to explode, they can not stop it,it is over and above the point no return, just Gadafi and Mubarak could not stop such bombs though they wished they could!.

Fikiri kusingekuwa na "the hague", ccm wangefanya nini!
Jipu limesha anza kuiva,wanaliongzea usaha!
 
nimeyasoma sana mazingira ya chaguzi zetu..lakini NO! something else should be done..I don't know!! it can be a new constitution or something else..I don't have an immediate answer yet!! But, I have a feeling that people's power might take its course, whether sooner or later!!
Take my words!!...


Sasa kwa nini mnakwenda against pipoz pawa? pipo wamesema "CDM NO" bado hamtaki kukubali au mnataka pipoz pawa hiyo iwe ni kwa CCM tu?. tafuteni njia mbadala, pipoz pawa imekula kwenu.
 
Ni kweli! Kwahiyo tuendelee kusubiri mpaka hapo mambo yatakapoiva?
 
Kweli, jana taarifa hizo ziliwekwa humu jamvini. Sheria ziko kwa CDM (tu) sio kwa CCM A-E. Haileti picha nzuri wala sio afya kwa mustakabali wa uhai na umoja wa Tz. So ni vizuri dunia isikie na kuona ya ccm na serikali yao.

Mengine yalojitokeza (list iongezwe)

- CCM kununua wa shahada za kura
- Wakazi wengi (hasa vijana) kubugudhiwa na/au kuwekwa ndani kwa makosa bandia ili wasipige kura
- Watu wenye haki ya kupiga kutopiga kura kwa sababu za ki-ccm
- CCM kuendesha kampeni siku ya uchaguzi kinyume cha taratibu na sheria
- Rushwa za kila aina i.e. serikali nk
- Vitisho
- Udini

Nani atamfunga paka kengele? CCM na vibaraka wao wanataka kushinda kwa gharama yoyote.
 
Hata kama kuna mizengwe ya wazi bado unataka Cdm wakubali tu? Tubadilike kwenye ukweli tuseme ukweli.
 
Haya yote yalikuwa yanafahamika toka awali ununuzi wa shahada,kuhonga,ahadi hewa namengi tu,cdm iteni nguvu ya uma tuandamane kudai tume huru yenye mjumuiko wa vyama vyote vya siasa na kudai katiba mpya.msimamizi anatakiwa kuwa nyutro.hayo tu.
 
Mabadiliko ya katiba ndio dawa! Lakini wasiwasi wangu ni kwamba ccm inaweza kuwatumia bakwata kupinga mabadiliko ya katiba kwa kuwarubuni kwamba mabadiliko ya katiba ni kwa manufaa ya wakristo! Bado tuna safari ndefu!
 
Damn!! So much blah blah....toeni kauli hapa tunafanya nini? Tunaanza na nani? Tunaanzia wapi? I'm so sick n tired with the fu**ing situation...
 
Sababu zinazonifanya niamini ccm wamechakachua ushindi:
1)Haiwezekani nusu ya waliojiandikish a washindwe kupiga kura, under normal circumstance, wasijitokeze ku vote.
2)Magari ya Police, ambayo hayajawahi kuonekana kabisa ktk mitaa ya Igunga, yakiranda mitaani na ving'ora kutisha wana Igunga kabla ya ku vote.
3)Igunga kuna njaa, ccm walitumia balaa la njaa kugawanya vyakula kidogo kidogo na kuwalazimisha wazee, wanawake kumpigia kura mgombea wake ili waendelee kupokea misaada hiyo.
4)CUF (ccm B) kilikwenda Igunga kuwasaidia ccm A kushinda. Kabla matokea hayajatangazwa CUF walishajua wameshindwa, hivyo ccm watawatumia kusaini form kukubali matokeo na uchaguzi ulikuwa huru.
5)Lastly and most Important ni CDM watakata rufaa kupinga huu Uchaguzi na wakienda mahakamani kesi watashinda, hivyo tutegemee Uchaguzi Igunga kurudiwa tena

 
Nilikuwa nasikiliza Sauti Amerika wameripoti kuwa katika kata moja huko Igunga wakati watu wanaendelea kupiga kura lilipita gari la sisiem likatangaza eti mgombea wa chadema amejitoa hivyo wakawaomba wasimpigie kura pia wameendelea kuripoti kuwa kuna kata nyingine wasimamizi walikuwa wanawaelekeza wapiga kura kukipigia sisiem, hayo yamesemwa na waangalizi wa uchanguzi mdogo wa Igunga.
Hofu yangu matokeo yanaweza kutokuwa halali kwa visa hivi na vingine ambavyo vimesharipotiwa humu, pia tunajenga au tunabomoa? Huu uchu wa kung'ang'ania madaraka utaliangamiza taifa kama tutaendelea kutumia siasa chafu kushinda. Siombei ila linaweza kujitoza watu wakaamua kudai hatima yao kama kule Ivorycoast na kwingineko.


hakuna cha waangalizi wala nini ccm imeshinda kihalali bila ubishi
 
hakuna cha waangalizi wala nini ccm imeshinda kihalali bila ubishi
CCM kwa ulevi tu wa madaraka inafanya hujuma ikiamini haitangoka madarakani.Lakini siasa za wakati huu ni za vijana. Na vijana hawawataki hata kuwasikia.Nawatahadharisha msijidanganye katu.Mtangolewa tena vibaya maana mtakuwa ni maadui badala ya wananchi wenzao vijana hao.Kwa nini hamuoni? Mna macho lakini hamuoni?Mna masikio lakini hamsikii? Hali ya upepo ni mbaya mno kwenu CCM."Mwalimu aliwahi kusema siku wananchi watakapo amka wakakuta mmewaibia mali zao, viongozi wote wa ccm mtaishia jela."Kama hamjaishia jela lakini wananchi hawa wameanza kuamka. Umma the sleeping giant is awekening, take care.Ushauri wa bure.
1)Msifanye uonevu, hasa kutumia vyombo vya ulinzi na usalama kuwanyanyas wapinzani na wananchi wanaotaka mabadiliko kwa ujumla.
2)Anzeni kujitayarisha kupokea nafasi ya upinzani kama wenzenu, KANU, UNIP, MMD kwa kuwa hiyo ndiyo nafasi yenu mliyo nayo kiuhalisia kulingana na hali ilivyo.
3)Mikakati yenu ya ushindi inazidi kuwapalia makaa ya moto iacheni kwa sababu siyo sustainable.
4)Acheni siasa za chuki kuwenu kama baba ambaye anakosolewa na wanae.Ktk kipindi cha miaka 50 lazimz mmefanya makosa mengi na mengine kama kuhujumu uchumi kwa makusudi, yako dhahiri.
5)Undeni tume huru ya uchaguzi, tume huru itawaondoa ktk mtego mliojinasisha wenyewe,kama mna akili mnaelewa ninachokisema.
6)Tafakarini yaliyowapata kina Mubarak,Gadaffi, Laurent Gbago n.k.Linganisheni nani mwenye akili kati ya hao niliowataja hapo na na Banda wa Zambia.
7) Vijana wa kizazi hiki ni moto ulao mtaliwa. Tafakari.Propoganda haisaidii maana wana mawasiliano supa.
8)Fanyeni utafiti kwa nini vyombo kama Intelligence services na security agencies hazikuwazuia vijana kuwaondoa kina Mubarak, Ghadafi nk.
9)Kwa herini tuonane 2015.
 
Jamani kwenye ukweli hebu tuseme ukweli kwasababu kadiri mnavyokataa ukweli uliowazi ndio mnazidisha chuki dhidi yenu. Kukiri kosa ndio njia sahihi ya kujipanga upya. Japan PM/Politician anajiuzulu hata kwa mambo ambayo hawezi kuzuia kama earthquake ili kuonesha ameguswa na wajapani walivyaathirika na pia kuwapa nafasi wengine kuonesha uwezo wao katika kutafuta suluhisho la matatizo, tunatakiwa na sisi tujenge utamaduni huu ili tusonge mbele.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom