Hii ni kweli ya Magufuli au ni safisha UKAWA na visasi?

Watu wanajibu baadhi kwa mihemko,nimetoa ushauri maana hata mh.Magufuli si malaika kwamba yuko sahihi 100% kila kitu.Tunamshauri kuwa makini na tahadhari juu ya maamuzi yake.

Wote tunataka afanye hivyo lakn hatutaki mbeleni aaibike.
Mbeleni mtaaibika nyie mnao politicized kila kitu
 
hivi kweli mtu upo serious unasema aangalie taarifa anazoletewa nyingine zinaletwa kwa visasi au wivu kweli???makontena 349 yanapotea unasema taarifa aliyopelekewa ni wivu kweli??bil 80 zimepotea kwa ajili ya hayo makontena mtu anasimamishwa unasema kulipiza kisasi et kisa alikuwa ukawa kweli??inamaana nyie ukawa mnaanza kutupa picha kuwa mngeingia madarakani wale waliokuwa wanaishabikia ukawa hata kama wana madhambi mngewaachia tu waendeleee na mambo yao??
 
Nchi hii pesa nyingi inapotelea matumboni kwa wajanja wachache hasa TRA huwa kuna mianya mikubwa ya Ulaji ndiyo maana huwezi kumkuta Afsa wa TRA ambaye ni masikini wote ni matajiri wakubwa na huchukua mda mfupi tokea wanajiriwa kutajirika, pesa nyingi ya makusanyo ya kodi huliwa na wajanja wachache hakuna Afsa wa TRA ambaye ni msafi wote wakichunguzwa wataozea jela. Awamu hii kweli wanataisoma Namba sawa sawa maana walizoea kujiachia Awamu za huko nyuma.

Mkuu, siyo maafisa wa TRA ya Tanzania tu, ni hata kipindi cha Yesu......walikuwa ni noouma! Si unamkumbuka Zakayo na maafisa wengine wa TRA ya wayahudi?
 
Ubadhilifu na ufujaji wa mali za umma usifungamanishwe na itikadi. Ni bora mtumishi akafukuzwa kazi kimakosa kuliko kimakosa kumuacha mtumishi mbadhilifu kwasabb za kiitikadi
 
Mkuu Swagazetu
Uliangalia taarifa za habari Chanel mbalimbali Leo? ITV walikuwa na best coverage sababu ilikuwa na maswali na majibu kati ya Waziri Mkuu na kamishna mkuu wa TRA
 
Mkuu Inapofikia mahala pa utendaji ulio bora tunapaswa kuweka pembeni itikadi za vyama vyetu. Ukawa ipo kwasababu ya mabadiliko, Sasa kama Magufuli kaamua kuleta mabadiliko na tunaona harakati zake ni nzuri kwanini tusi msupport. Kama utendaji wako ni mbovu haita saidia kitu endapo utakuwa migongoni mwa vyama vya upindani wala CCM. Tunacho taka sisi ni watendaji wabovu wote ndani ya serikali kuwajibika. Itikadi za vyama tuweke pembeni. Tumsupport huyu bwana kwani kaanza vizuri.
 
Nimefuatilia swala la kashfa ya TRA leo iliyosababisha Kamishna wake Rished Bade kusimamishwa kazi na kukaimiwa/kuteuliwa ndugu Mpango Philip.

Hapa sileti siasa lakini timuatimua hii iangaliwe kwa jicho la tatu maana binadamu wote huwa na roho ya kisasi aidha kwa wema au ubaya.Sijasikia tume iliyoundwa kuchunguza mienendo na utendaji wa watumishi ktk nyanja kuu za serikali lakini timua timua inaendelea.

Je hizi taarifa anazofanyia kazi mh.zinapelekwa na watu waminifu au watu wa visasi?

Kama ni kweli kuna ukweli na yuko sahihi basi nafhani hata rais msitaafu wa juzi achunguzwe maana haiwezekani madudu yako jujuu inakuwaje hayakuonekana wakati alisifiwa kwa uongozi wake?

Rais wangu mh sana Dr Magufuli ni vema waleta taarifa nao ukawachunguza wasikuchonganishe na watumishi ukashindwa hata kumuamini hata mmoja mwisho wa siku ukakosa wa kukusaidia.Inawezekana Ukawa-Ccm ikawa inafanya kazi ukadhani wanakusaidia.Kwa kuwa watu tumeumbwa kila mmoja na Envy yaani wivu ni vizuri kuwa makini na taarifa kabla hujazifanyia kazi.

Nimekukubali kwa kasi na utendaji kama utaendelea na ongeza speed maana nchi ilipofikia inahitaji kiongozi mwenye busara na hekima pamoja na Udikteta wa kidemokrasia.

Pamoja na hayo ni vema ujawa makini na taarifa unazoletewa kabla ya kuzifanyia kaz maana naamini huzipati ghafla pale unaposhtukiza ila unakuwa na prio info zinazokusukuma kufanya maamuzi.

Isiwe safisha Ukawa maana inasemekana kuna watumishi waliotumia uhuru na demokrasia kumuunga mkono mgombea wanaomtaka wasivhukuliwe waasi bali wenye uhuru na nchi yao kama walioamua kuwa ccm.Kuwa ccm au Ukawa ni maamuzi ya mtu na haingiliwi katika kuchagua atakacho isipokuwa ubadhilifu.

Lakini kama wanawajibishwa kwa utovu wa nidhamu na ubafhilifu ni haki yao.

Maamuzi na taarifa unazotumia zisiwe na hata chembe ya Uchama wala siasa.maana hata wewe ni binadamu.

Kumbuka Ukawa wamesaidia kupatikana kwa taarifa za ubafhirifu mwingi na watu kuachia nyadhifa zao hvyo wanahitajika.Upinzani ni Watching dogs wa serikali yako na ukiweza usisite kuteua mawaziri wanaofaa ili wakusaifie ili serikali yako iondoe harufu ya uchama iwe ya watanzania wote.

Mungu akulinde akupe maisha marefu.

Tulia mkuu,watu wako kazini-kiongozi akipiga fair play mnamwita legelege,akiwa ngangari mnahisi visasi.Tumpe moyo na kumuunga mkono mheshimiwa Rais,binafsi siamini kama anaweza kufanya visasi,dawa ni kuwa raia mwema
 
Mh Rais kafanya maamuzi hayo baada ya kupata feedback frm PM,, kwa Ziara yake ya kushtukiza.. Sasa mambo ya UKAWA yanaingiaje hapa tena. Yaan kwa evidence zote hizi za makontena 349 kodi iliyokwepwa zaid ya bil 80, bado unaingiza mambo ya UKAWA tena.???!!!
 
Nangojea....

1: UDA...

2: LAKE GAS, LAKE OIL

3: ESCROW

4: MADAWA YA KULEVYA...

5: MASLAHI YA WATUMISHI WA UMMA na kushuka kwa PAYE

6: WACHINA wanao zurura Tz warudishwe kwao
 
kamishna bade alikiri upotevu we hayo makontena 349 na akajibu kisiasa eti wanajua na walikua wanafanyia uchunguzi ndipo Waziri mkuu akamuuliza unafanyia uchunguzi watu ambao tunao hapa hapa kwnye mkutano?
 
Mbona hili la leo wengi mmeumia sana..?
We ulitaka tume ya kazi gani wakati kila kitu kipo wazi ameulizwa na amekiri mwenyewe tume hapo ya kazi gani..? Au haujui kazi ya tume..?
 
Mkuu Swagazetu
Uliangalia taarifa za habari Chanel mbalimbali Leo? ITV walikuwa na best coverage sababu ilikuwa na maswali na majibu kati ya Waziri Mkuu na kamishna mkuu wa TRA

Ndugu nimeangalia zote star na Itv na ninachokisema si kwa hili la leo tu ila hata kwa yanayoendelea.Sijabase kwenye itikadi bali nimetoa ushauri kama mtu anaadhibiwa kusiwe na itikadi za kisiasa.

Umesoma post yangu yote kweli? Soma vzuri utanielewa mkuu.
Uchaguzi umeisha tunatoa ushauri mkuu.
 
yule mbunge wa chama "x"aliyekuwa anapenda kutumia neno "legelege" kuwaita viongozi bado yupo au keshaingia uvunguni?kama yupo je ana maswali?acheni dhahabu iitwe dhahabu.
 
Ndugu nimeangalia zote star na Itv na ninachokisema si kwa hili la leo tu ila hata kwa yanayoendelea.Sijabase kwenye itikadi bali nimetoa ushauri kama mtu anaadhibiwa kusiwe na itikadi za kisiasa.

Umesoma post yangu yote kweli? Soma vzuri utanielewa mkuu.
Uchaguzi umeisha tunatoa ushauri mkuu.

Mkuu nimesoma vizuri post yako mi sikuelewi kwanini umechanganya tukio la leo ambalo Kamishna Mkuu kakubali kuwa kuna upotevu wa kontena 300 anaujuwa na orodha aliyoitoa Waziri Mkuu ameikubali kuwa ni kweli ila wapo kwenye kushughulikia hilo tatizo na TAKUKURU! Waziri Mkuu akamuuliza mnashughulikia vipi na watuhumiwa wapo kazini? 80B anakiri do you need someone from Scotland Yard kuja kuchunguza? Amazing!!!
Unasema pengine ni figisu za kisiasa!!!
 
Nimefuatilia swala la kashfa ya TRA leo iliyosababisha Kamishna wake Rished Bade kusimamishwa kazi na kukaimiwa/kuteuliwa ndugu Mpango Philip.

Hapa sileti siasa lakini timuatimua hii iangaliwe kwa jicho la tatu maana binadamu wote huwa na roho ya kisasi aidha kwa wema au ubaya.Sijasikia tume iliyoundwa kuchunguza mienendo na utendaji wa watumishi ktk nyanja kuu za serikali lakini timua timua inaendelea.

Je hizi taarifa anazofanyia kazi mh.zinapelekwa na watu waminifu au watu wa visasi?

Kama ni kweli kuna ukweli na yuko sahihi basi nafhani hata rais msitaafu wa juzi achunguzwe maana haiwezekani madudu yako jujuu inakuwaje hayakuonekana wakati alisifiwa kwa uongozi wake?

Rais wangu mh sana Dr Magufuli ni vema waleta taarifa nao ukawachunguza wasikuchonganishe na watumishi ukashindwa hata kumuamini hata mmoja mwisho wa siku ukakosa wa kukusaidia.Inawezekana Ukawa-Ccm ikawa inafanya kazi ukadhani wanakusaidia.Kwa kuwa watu tumeumbwa kila mmoja na Envy yaani wivu ni vizuri kuwa makini na taarifa kabla hujazifanyia kazi.

Nimekukubali kwa kasi na utendaji kama utaendelea na ongeza speed maana nchi ilipofikia inahitaji kiongozi mwenye busara na hekima pamoja na Udikteta wa kidemokrasia.

Pamoja na hayo ni vema ujawa makini na taarifa unazoletewa kabla ya kuzifanyia kaz maana naamini huzipati ghafla pale unaposhtukiza ila unakuwa na prio info zinazokusukuma kufanya maamuzi.

Isiwe safisha Ukawa maana inasemekana kuna watumishi waliotumia uhuru na demokrasia kumuunga mkono mgombea wanaomtaka wasivhukuliwe waasi bali wenye uhuru na nchi yao kama walioamua kuwa ccm.Kuwa ccm au Ukawa ni maamuzi ya mtu na haingiliwi katika kuchagua atakacho isipokuwa ubadhilifu.

Lakini kama wanawajibishwa kwa utovu wa nidhamu na ubafhilifu ni haki yao.

Maamuzi na taarifa unazotumia zisiwe na hata chembe ya Uchama wala siasa.maana hata wewe ni binadamu.

Kumbuka Ukawa wamesaidia kupatikana kwa taarifa za ubafhirifu mwingi na watu kuachia nyadhifa zao hvyo wanahitajika.Upinzani ni Watching dogs wa serikali yako na ukiweza usisite kuteua mawaziri wanaofaa ili wakusaifie ili serikali yako iondoe harufu ya uchama iwe ya watanzania wote.

Mungu akulinde akupe maisha marefu.

Hizo taarifa zilikuwepo siku nyingi tu ila zilikosa mtekelezaji.
 
Ndugu nimeangalia zote star na Itv na ninachokisema si kwa hili la leo tu ila hata kwa yanayoendelea.Sijabase kwenye itikadi bali nimetoa ushauri kama mtu anaadhibiwa kusiwe na itikadi za kisiasa.

Umesoma post yangu yote kweli? Soma vzuri utanielewa mkuu.
Uchaguzi umeisha tunatoa ushauri mkuu.

Hata mwizi hujitetea...... Ndugu umechemka andaa maada nyingine.....
 
Back
Top Bottom