Tanzania Nchi Yetu Sote
JF-Expert Member
- Mar 12, 2017
- 505
- 871
HATARI SANA
```Kwenye moja ya hospitali kubwa hapa mjini, kwenye chumba cha wagonjwa mahututi {I.C.U.} wagonjwa walikuwa wakifariki Dunia kwenye kitanda kimoja na muda ule ule saa 1 asubuhi kila siku bila kujali walichokuwa wanaumwa.
Jambo hili lilikuwa kitendawili kikubwa mno kwa madaktari bingwa wa hospitali hiyo. Kwa hiyo kundi la madaktari likaamua kufanya uchunguzi kwenye hicho kitanda kwa siri na walikaa kwenye hicho chumba wakisubiri muda wa mtoa roho yaani saa moja asubuhi washuhudie kinachoua watu kwenye hicho kitanda. Baadhi walishika vitabu vitakatifu ili kukemea pepo linaloua litakapotokea. Wale wasio na uoga walikuwa tayari na kamera zao smartphones tayari kwa ajili ya kupiga picha kwa kila tukio kuelekea saa moja asubuhi.
Ilipotimu saa 1:00 kamili asubuhi mlango ulifunguliwa pole pole, ukimya ulitawala kila mtu roho mkononi kuona kinachotokea baada ya mlango kufunguliwa.
Sikira ambaye ni mfanya usafi wa chumba hicho na ambaye kila siku huanza kazi yake saa moja kamili asubuhi aliingia.
Kitu cha kwanza alichofanya alichomoa chombo cha umeme kilichokuwa kinasaidia maisha ya mgonjwa na kuweka chaja ya simu yake ya NOKIA ili achaji simu yake.```
_Kama elimu ni ghali basi jaribu ujinga._