Hii ni demokrasia au ghasia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ni demokrasia au ghasia?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Malisa Godlisten, Jan 27, 2010.

 1. Malisa Godlisten

  Malisa Godlisten Verified User

  #1
  Jan 27, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 803
  Trophy Points: 180
  SEPTEMBA 15 mwaka 2009 Tanzania iliungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku ya Demokrasia duniani.

  Pamoja na mengi yaliyozungumzwa lakini Tanzania ilisifiwa kuwa imekomaa kidemokrasia ukilinganisha na mataifa mengi ya kusini mwa Sahara (Sub-saharan countries). Swali la msingi tunalopaswa kujiuliza ni Je, ni kweli Tanzania ina demokrasia?? Au demokrasia yake inaonekana baada ya kulinganishwa na nchi nyingine zisizo na demokrasia.

  Utaratibu wa kufanya maamuzi ya kitu kwa kulinganisha na kingine ni hulka ya mwanadamu. Ila sikubaliani na utaraibu huu moja kwa moja,maana mtu huwezi kujiona si mwehu kwa kujilinganisha na mwehu. Yawezekana ukawa mwehu kwa kiwango kidogo kuliko huyo unayejilinganisha nae, hivyo huwezi kuona wehu wako.

  Mimi naamini hata maalbino wasingejiita walemmavu kama wangezaliwa na kujikuta peke yao huku duniani. Walijiona walemavu baada ya kujilinganisha na wasio maalbino. Ila hata wangekuwa peke yao isingeondoa ukweli kuwa wao ni walemavu (kwa kujua au bila kujua)

  Sasa ikiwa ndivyo inakuwaje Tanzania kusifiwa kwa demokrasia ilihali inalinganishwa na nchi zisizo na demokrasia?

  Tena mwenyekiti wa kituo cha demokrasia nchini (makamu mwenyekiti wa CCM-bara) Pius Msekwa akasisistiza kuwa “tupingane bila kupigana”. Napotafakari hali ya siasa nchini hasa kwa kipindi cha serikali ya awamu ya tatu nashindwa kuelewa kauli ya mwanasiasa huyu nguli aliyeongoza mhimili mmoja kati ya mihimili mitatu ya serikali kwa kipindi chote cha awamu ya tatu.

  Mwaka 2001 January 26 Watanzania kadhaa waliandamana huko Zanzibar kuelezea hisia zao (kidemokrasia) kupinga matokeo ya uchaguzi uliojaa mizengwe, uliomweka madarakani Rais Karume. Askari wa KMKM kwa kusaidiana na polisi waliwavamia kuzuia maandamano yao , na takribani watu zaidi ya 10 waliuawa huku wengine mamia wakiishia kuwa wakimbizi katika kambi ya wakimbizi Shimoni huko Mombasa Kenya.

  Hivi huko ndiko kupingana bila kupigana alikokuwa anazungumzia Msekwa? Labda hii ndiyo Demokrasia tunayosifiwa nayo. Hakuna demokrasia inayoweza kuota mizizi bila kuwepo utawala bora. Je,Tanzania ina utawala bora? Utawala unaojali maslahi ya umma?

  Mwanzoni mwa mwaka 2009 mwenyekiti wa makampuni ya IPP Bw.Reginald Mengi alitumia haki yake kikatiba [ibara ya 18(a)] kwa kuwataja watu anaowajua kama wahujumu wakuu wa rasilimali za taifa, yaani MAFISADI PAPA.

  Cha ajabu waziri mwenye dhamana ya huo “utawala bora” Mh.Sophia Simba alijitokeza hadharani kumpinga na kumkejeli Bw.Mengi eti AMECHEMSHA. Amechemsha nini? Amechemsha kutumia haki yake kikatiba au amechemsha kuwataja watu wasioafaa kutajwa?? (maana hata wakitajwa hawatachukuliwa hatua zozote) Je, huu ndio utawala bora unaohubiriwa kuwa umejaa Tanzania?

  Kwa muda mrefu sasa wananchi wa majimbo yanayoshikiliwa na upinzani, wamekuwa wakionekana wasaliti na yatima ndani ya nchi yao wenyewe. Kwa makusudi Serikali haipeleki maendeleo kwenye majimbo hayo kwa kigezo kuwa ni ya upinzani. Tena bila aibu wagombea wa CCM wamekuwa wakiwatisha wananchi katika kampeni zao kuwa eti wakichagua upinzani hawatapata maendeleo.

  Hivi mtu kutumia haki yake kikatiba kuchagua chama akipendacho umekuwa UHAINI? Hivi demokrasia iko wapi hapo?

  Labda niwakumbushe ndugu zangu wa kituo cha Demokrasia nchini kuwa Demokrasia haipimwi kwa ulinganifu (comparisons), bali hupimwa kwa vigezo dhahiri (facts). Vigezo hivyo ni pamoja na uchaguzi huru na haki, uhuru wa maoni, utekelezaji wa haki za binadamu, na utawala bora. Je,Tanzania ina vigezo vya kuitwa nchi ya kidemokrasia?

  Kama demokrasia hupimwa kwa ulinganifu (comparisons) basi Sudani ni nchi inayoongoza kwa demokrasia ukilinganisha na nchi nyingine za pembe ya Afrika kama Somalia na Djibout.

  Itaachaje kuongoza wakati machafuko ya Darfur hayafui dafu kwa maharamia wanaoteka meli kila kukicha huko Somalia? Au wababe wa kivita wanaoua mamia kila siku Mogadishu.

  Hivi iliyopo Tanzania ni Demokrasia Au Demo-ghasia?? TAFAKARI!
   
Loading...