Hii ni Democrasia au Mabavu??

Samat

Member
Dec 20, 2009
35
1
Kwa hakika wafanyakazi wa Tanzania hatuna kiongozi, na hatutakaa tupate haki zetu hata kwa dawa. Napendekeza huyo kiongozi wetu ajiuzulu baada ya kutudanganya watanzania kama watoto. Mambo ambayo wafanyakazi walikuwa wakidai ni ya haki yanayoeleweka hata na mtoto mdogo. Kitendo cha kuyakubali matishio ya raisi ilihali mgomo ulishatangazwa kwa muda mrefu uliowezesha serikali hiyo hiyo kulitatua tatizo hilo mapema, na kungojea mpaka dakika ya mwisho na huu ni ufisadi wa aina yake.
Tanzania Tanzania! ni lini utakuwa na viongozi wenye kuwaambia watu wako jambo wakaliamini? Watanzania tutakuwa tukidanganywa hadi lini? Kiongozi asiyeaminika ni hatari sana kwa watu anaowaongoza. Kiongozi anayeongoza kwa mabavu ni hatari sana kwa ulimwengu huu wa demokrasia. Kwa nini raisi huyu alikaa kimya mpaka dakika ya mwisho? Kwa nini raisi huyu ageuke kuwa mahakama? Na kama ni kweli hawa viongozi wa TUCTA waliwadanganya wafanyakazi ni kwa nini wasichukuliwe hatua za kisheria kwa kudanganya? Je haki za wafanyakazi zilianza kudaiwa mwaka huu?
Je, kuna tofauti gani kati ya wafanyakazi hawa na viongozi wanaolipwa mamilioni ya mshahara, mamilioni ya posho, usafiri, nyumba na bahati mbaya wizi ambao kwa sasa umeshakuwa kama ni sera ya serikali? (ni sera kwa sababu wezi wanaofahamika hawachuliwi hatua kwa sababu tu ni wakubwa, na hatua chache zilizochukuliwa ni danganya toto).
Ee Tanzania umefilisika kibusara na kimaadili. Ndugu zangu wafanyakazi mpo kila kona ya Tanzania, sasa chukueni silaha ya kuwaelimisha Watanzania wa hali ya chini kuwaondoa madarakani kwa kuwanyima kura (na amesema hazitaki kura zetu), viongozi wababe na wanaowanyanyasa.
Ushauri wangu ni huu. Chagueni wapinzani wengi ambao watatumia nguvu ya hoja na kura bungeni kuondoa huu unyanyasaji. Chama tawala CCM kikiendelea kuwa na wabunge wengi mjue hamtakaa mpate haki zenu milele.
Mungu mbariki huyu aliyesoma ujumbe huu
 
Back
Top Bottom