Hii ni busara au kukata tamaa

tumpale

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
200
35
Limekuwa ni jambo linalonishangaza na kunisononesha kila mara ninapopita ubungo stendi ya daladala kwa wakazi wa kimara, mbezi, kibamba na sehemu zingine za uelekeo wa mlandizi . kutokana na tatizo la usafiri nyakati za jioni pale kituo cha daladala cha ubungo zinapaki pickup na malori kwa ajili ya kubeba abiria. namaanisha pick up na malori sasa ni usafiri uliozoeleka kwa wakazi wa maeneo hayo na hakuna anayeonyesha kujali, kuhoji au kuwa na mkakati wa kuiondoa hali hiyo. swali langu ni je tumeridhika na hali hiyo au tumekaa kimya kwa sababu viongozi wetu hawaonyeshi kujali. je viongozi hawajui kama suala la usafiri sasa hivi jijini ni zaidi ya janga, siamini kama ni busara lakini nadhani watanzania wamekata tamaa ya kila jambo. nature ya watanzania ni waoga na mabingwa wa kunung'unika, tubadili hii tabia tusimame tukemee ujinga unaofanywa na viongozi wetu kumbukeni msemo huu '' mzaha wenu mauti yangu''. viongozi wwanafanya mzaha sisi tunaumia lakini tumekaa kimya.
 

Johas

Senior Member
Feb 13, 2009
141
31
Ndaga tumpale.!
Sijui sheria ya Sumatra inasemaje kuhusu aina ya matumizi ya usafiri wa namna iyo...

Kwa uelewa wangu sheria hairuhusu kwa aina iyo ya magari,i.e Malori/pick up kutumiwa kama..
chombo cha usafirishaji kwa abiria.

Lakini sikuzote penye shida busara inakuwa ngumu sana kutawala...Watu wanatafuta njia mbadala then maisha yanakwenda..

Nadhani taarifa ziwafikie Mamlaka uhusika.
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom