Sentensi za kiswahili huanza na kiima kisha kiarifu. Kimuundo sentensi yako si fasaha. Ilipaswa kuwa
-Hajafika hapa tangu jana.
Na kwa muundo huo hapo kiima si dhahiri (kiima kapa) maana hakionekani bali kinafahamika, ni YEYE.
Neno TANGU ni Kihusishi cha Wakati kama yalivyo maneno-kabla ya...na baada ya...