Usiku wa saa 6 kuna jambo lilinitokea la ajabu sana, nikiwa nimemaliza kuomba nikalala lakini sikuwa na usingizi nikahisi kama kuna mtu amesimama kitandani ghafla nikahisi uzito wa mwili na macho nikajitahidi kukemea ghafla nikaona kivuli cha Mwanamke na mkono wake ukishika tumbo langu nikajitahidi kukemea na kutaka kuinuka nikaweza kuinuka
Mara nikasikia tumbo likiunguruma nikakaa kitandani na kuanza kuomba hadi saa 6 na dakika 45 nikalala, kwenye saa 7 na dakika zake nikapitiwa usingizi nikaota niko mazingira ya chuo mimi na wenzangu ambao nilimaliza nao secondary akiwemo Philbeth Jacqreen pamoja na Arafa tukiwa darasani tukaona wenzetu wakicheza kwaya
Na wengine wakifanya biashara ya nguo lakini tukiwa humo darasani tukashauriana kwa sababu ya kelele tuweze kutoka na kwenda kusimama nje tukiwa tumebeba mabegi yetu tukaelekea upande wa madarasa mengine ambako kuna walinzi na hawaruhusu kuingia ila nikawaona hao mabinti watato niliokuwa nao wakiingia
Lakini hawakutoka na kufungiwa mlango ndani mabeg yao yakatupwa nje sasa mimi nikasema mbona umewafungia mlango akasema yule kijana mlinzi yakuwa huku haruhusiwi kupita mtu wala kuingia ni sehmu ya Jeshi kwa hiyo hawa hawawezi kutoka tena
Basi pembeni ya ule mlango kulikuwa na viti na mabenchi kama ya Zahanati nikaweka begi langu nikasema niende Kuwaangalia wale wanafunzi wenzangu darasani ambao tuliwaacha wakicheza kwaya lakini cha kushangaza sikuwakuta na niliwakuta wanafunzi wengne na mimi nikarudi kuchukua begi langu
Ndipo nilipowakuta vijana wengne kama wanne hivi pale nilipoacha begi langu sukuliona nikajaribu kutafta nikalipata hilo begi pembeni kwa nje limetupwa lakini nikaamka kutoka usingizini baadae nikaota tena nipo hayo maeneo ya chuo ambapo niliacha begi nikaanza kulitafta sikuliona wale vijana wakiwa wamekaa paleple wakaniambia katafute kule Porini
Nikaenda ambako kumefyekwa nikakuta mabegi mengi yametupwa mengine mapya na mengne machakavu nikawa natafuta bila mafanikio. Nikiwa nalia nikafanikiwa kuliona begi rangi ya kijeshi likiwa jipya nalo miongoni mwa yale yaliyotupwa nikajisemea akilini mwang bora nichukue begi hilo kuliko kurudi nyumbanu bila begi
Nikiwa bado natafuta la kwang bila mafanikio nikaamua kuondoka na ndipo niliposhtuka kutoka usingizini na kuitafakari hiyo ndoto ikiwa na maana gani kujirudia mara mbili nikiwa natafuta begi!
Unaweza nisaidia tafsiri hiyo ndoto mtumishi
Sent using
Jamii Forums mobile app